Kilichofanywa na mchezaji Fiston Mayele ichukuliwe kama funzo kwa sajili zingine. Nafiriki viongozi wa Yanga SC hawakuwahi kujifunza juu ya baadhi ya nyota ambao hua wanawasajili kisha kuwavua nguo na baadae wanawarejesha tena klabuni.

Wapo ambao wameonyesha kufurahishwa sana katika hili tena wengine wameenda mbali kukenua mimi niwapa pole sana kwasababu mambo mabaya kama hayo hua hayadumu. Si tuliona mfano mdogo kwa Feisal Salum kisha baadae ikaibukia kwa mshambuliaji Prince Dube, kwani imechukua muda gani basi.

Upendo kwa Mayele ulikuwa mkubwa tena alipewa kila kitu, siyo kutetemesha watu kila alipokwenda alikuwa kama mfalme. Hakuna mchezaji aliyeongoza kwa kupewa zaidi kumzidi yeye. Ng’ombe alipewa, U- Chief aliupata pesa pia sasa sijui ni kipi kilimpata mchezaji huyu.

Naamini tukianza kuelezana mabaya hapa hakuna Klabu itakayosimama lakini wachezaji wanaamua kuyafukia mambo kwenye kifua. Kazini hua haya yanajitokeza sana sema ni vile watu wanayatiliza vifua kama mipira kisha maisha yanasonga.

Tuziandike takwimu na tuzidadavue kwa ukubwa lakini lazima tukubali ndugu yetu ameteleza na ameonyesha ameshindwa kuyavumilia mambo, amekubali kukiachia kifua chake kibaki wazi, kolomelo la KIUME limemponyoka hata hivyo Tanzania hatuna baya haya yote sisi tunafukia tu kisha maisha yanaendelea kama ilivyo tamaduni yetu, kwetu sisi wageni ni wetu.

Karibu tena FISTON KALALA MAYELE katika ardhi iliyobarikiwa kila kitu, amani, starehe, upendo hata na ukarimu pia, tunakupenda na wala hatukuchukii, ulichoshindwa ni kutenganisha utani wa mpira na maisha halisi.

SOMA ZAIDI:  Naamini Kuwa Mchawi wa Simba ni Wanasimba Wenyewe 

5 Comments

  1. UNCLE OCTOPUS on

    Wana soka tumsamehen n km anatafta kik yey mwenyw mamb yake ni km kashapotea hajui atendalo nisaidieni kumwambia kuna leo na kesho SISI NI PEOPLE

  2. Mayele ni binadamu ambaye kashindwa kuhimiri hisia, utani na kashifa za wanasoka ambao wameanza kupenda timu kabla ya kuujua mpira.
    ⚽⚽

    Kuna muda nashindwa kumlaumu kwani si kila mtu anaweza kuvu!ia neno hasa anapoona maneno ya ovyo yanapowavaa familia yake🖐️

    Ila nasi kama wadau wa soka, wapenzi wa kabumbu tuwe na maneno yenye staha kwani mchezaji au kiongozi ni binadamu kaumbwa na moyo anaata hisia kama binadamu mwingine🙏

    Mwisho kwa kilichotokea ni funzo kwa wachezaji na klabu pia, kutumia wanasheria wasomo kwenye kujaza mkataba maana hayo ni masilahi si kitu cha kuchezea au kujaribu✍️✍️✍️✍️✍️

  3. Ndabilenze Ndabilenze on

    Ukiwa makini utagundua tu viongozi WA azam wameshindwa kushindana na giants kwenye dakika 90 ndo mana wanajaribu trick za nje ya uwanja.. ukiwaangalia azam wanajaribu njia za out of field kucompete na yanga kwa kuitengezea roumans tofauti…

    Refer kesi ya Feisal walishinikiza wao lengo likiwa ni engenear aonekane mbaya lakini cha kuwapongeza yanga kuanzia viongozi Hadi mashabiki Zao..

    Wakaona haitoshi wakawatumia watu kama yaniq bangala n’a juma tshabani still wamefeli kuwatoa yanga kwenye reli

    Nb, yanga hawatakiwi kuingia kwenye mtego WA azam fc wao wapambane kujenga timu shindani mwisho mafanikio yatakuja yenyewe tu
    ,Azam waache mambo za nje ya uwanja kisa tu hawana pressure ya mashabiki Bali wawekeze kwenye pitch quality ya Hali ya juu washinde game Zao mashabiki watakuja wenyewe tu

    Note : mamelody ameibuka katikati ya kaezer chief na Orlando Pirates, kawekeza uwanjani zaidi n’a saivi fans wamekuja wenyewe automatically ndani na nje ya south Africa
    ✍️ ttraveller347@gmail.com

  4. Kuoneana aibu aibu na kuogopa ogopa watu wenye uwezo na wenye hela ,ndio kunawafanya watanzania waonekane wa amani na uzalendo. Kuchekea chekea vitu hata kama unaona vbaya huwezi kuvisema.

    Different culture between Congo na Tanzania n hiki kusema ukwel.

Leave A Reply


Exit mobile version