Tatizo letu sisi watu wa mpira tunapenda kuvisikia vitu tuvipendavyo sisi, mfano ukiongelea ubora walionao Yanga SC utaambiwa sijui wewe ni Mnyama.Na hata hili nalozungumzia leo kuhusu Mwigulu na Ihefu nalo wapo watakaopinga. Ngoja niwakumbushe jambo, Viongozi wa Yanga walipopitia kwenye uchungu wa zaidi ya misimu minne siyo kwamba walilala na kupata usingizi, jibu ni hapana walikesha kutaka kujua walikosea wapi.

Hivi mmesahau yale maumivu waliyoyabeba kipindi kile cha BAKULI vipi Leo wakitesa kwa haya maboresho yao. Kama wewe jirani utachukizwa na nini ndugu yako alipoamua kufanyia kazi. Si ndo sisi ambao tulikuwa tukisisitiza viongozi kuiga mfano kutoka kwenye uongozi bora chini ya Mo Dewji. Vipi Leo tumeshasahau?

Kama uongozi wa Yanga umefuata taratibu zote na timu imesheheni wachezaji wenye uwezo vipi leo tuseme ni hujuma, inamaana tunaukataa ubora wa Diarra, tunapingana na usajli wa beki kitasa Ibrahim Baka, vipi Stephanie Aziz Ki, au Pacome Zouzoua. Ndugu zangu nikiiandikia sana Yanga hamtachelewa kuniita hayo majina yenu ila ukweli ni kwamba, Yanga SC wamejipata mimi hata sina shaka na ubora wao.

Kitendo kile cha Simba SC kupoteza kwa idadi kubwa ya mabao tena goli 5-1 ile ilikuwa ni ishara kwamba Yanga SC imedhamiria kuifunga timu yoyote ile siyo tu hapa hata huko kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. Vipi nimemsahau kumtaja Maxi Nzengeli na Joseph Guede jamani naomba mnielewe tu kuwa Yanga imejipata.

Turudi nyuma miaka ya 2013 huu ilikuwa msimu wa 2013/2014 pale mdhamini bia ya Kilimanjaro Premium Lager chini ya Meneja wa bia hiyo ya Kilimanjaro, George Kavishe alipokabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya Simba SC na wenzao Yanga SC tayari Kwa kuuanza msimu wa mashindo.

Hoja yangu itasimama hapa kama tunaingia kuwatilia shaka wadhamini ambao kwa moyo wao wa dhati wameamua kuukomboa mpira wetu, basi inatubidi turudi kipindi hiki tujiulize vipi mahasimu hawa wawili walikubali vipi kudhaminiwa na mtu mmoja.

Nafiriki tusiwavunje moyo watu wanaotaka kuufanya mpira wetu kusonga mbele sisi mpira wetu bado sana na unaendelea kujitafuta ili siku moja tufikie yale malengo

Leo utaanza kuwasema vibaya Ihefu FC kwasababu tayari wamejipatia mdhamini lakini unajua ugumu wa kumpata mtu ambaye ataipatia nguvu biashara Yako ili iweze kukuaa. Tupunguze nyundo kwenye eneo linalohitaji ukuaji.

Nafiriki tuwapongeze kampuni ya Haier kwa mapenzi yao katika soka letu pengine kesho wanaweza kuleta kitu zaidi. Hii inaanza kutengenezwa ili kuifanya Yanga SC ni kama itaenda kukutana na mchezo mwepesi dhidi ya Ihefu FC, tupunguze uongo ndugu zangu.

SOMA ZAIDI: Yanga vs Ihefu Wachezaji Hatari Wa Kutazamwa Hii Leo

1 Comment

  1. Pingback: Kwanini Mdhamini Mmoja Timu 6 Ligi Moja? - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version