Klabu ya soka kutoka nchini Saudi Arabia Al Ittihad imeanza vyema kampeni zake za kuchukua ubingwa wa kombe la dunia upande wa klabu kwa kumchapa Auckland mabao 3:0.

Katika mchezo huo mabao hayo yalifungwa na Romarinho dakika ya 29 ya mchezo , Kante akifunga goli dakika ya 34 pamoja na kapteni wa timu Benzema ambaye amefunga dakika ya 40 ya mchezo na kuutamatisha mchezo kwa bao 3:0.

Katika kikosi cha sasa cha Al-Ittihad apo wachezaji ambao washawahi kuchukua ubingwa wa klabu bingwa ya dunia na miongoni mwao ni pamoja na Ngolo Kante ambaye alichukua akiwa anaitumikia Chelsea lakini pia Karim Benzema akiwa anaitumikia Real Madrid pamoja na Fabinho wakati anaitumikia Liverpool.

Katika mchezo huo Ngolo Kante ameibuka mchezaji bora wa mechi. Katika muendelezo wa michezo hiyo ratiba kamili ni kuwa Club Leon atacheza dhidi ya Urawa Red Diamonds huku Al Ahly yeye akimsubiria mshindi wa mechi ya kwanza ambaye ni Al Ittihad.

Unaweza kuendelea kusoma zaidi taarifa zetu kwa kubonyeza hapa.

Leave A Reply


Exit mobile version