Bila shaka kila ukitazama mechi za Al Ahly kwenye warmup huwa unaona wachezaji wote wamevaa jezi namba 72. Unajua maana yake!? twende sawa.

Februari Mosi, 2012 kulitokea tukio baya zaidi kwenye historia ya mpira wa Misri pale mashabiki wa Al Masry walipoingia na mapanga, visu, mawe, vilipuka na chupa waliwashambulia mashabiki wa Al Ahly na kuwadhuru.

Kiasi cha mashabiki 72 wa Al Ahly waliuawa, Polisi 1 na shabiki mmoja wa Al Masry kwenye machafuko hayo huku mashabiki zaidi ya 500 wakijeruhiwa baada ya mashabiki wa Al Masry pale Port Said kuvamia majukwaa na eneo la kuchezea.

Vifo vingi vilisababishwa na Polisi kukataa kufungua mageti ya uwanja ili mashabiki wanaojinusuru kutoka uwanjani wapite na hali hiyo ya machafuko ilidumu mpaka February 11 na siku 2 baadae ilikoma.

Siku 2 kabla ya mechi iliachiwa video kwenye You Tube ya mashabiki maarufu wa Al Masry wanaofahamika kama “Ultras Green Eagles” wakitahadharisha kuwa shabiki yoyote wa Ahly atakayeenda uwanjani atauawa na hakukuwa na utani katika hilo.

Siku ya tukio mabasi mengi ya mashabiki wa Ahly kutoka Cairo yalikataa kwenda Port Said kwa hofu ya usalama na mashabiki wakasafiri kwa treni kutoka Cairo na kufikia umbali wa dakika 15 kutoka Port Said wakisindikizwa na Polisi.

Mchezo ulichelewa kuanza kwa dakika 30 kutokana na mashabiki wa Al Masry kuingia uwanjani na baada ya kushinda goli 3 waliingia uwanjani wakirusha chupa na visu kwa wachezaji wa Al Ahly ambao walikimbilia vyumbani kwa usaidizi mkali wa Polisi.

Balaa likahamia kwa mashabiki wa Ahly ambapo uzembe wa Polisi ukasababisha mauaji hayo ya kutisha. Waliwatoa baadhi ya majeruhi kwenye ambulance na kuwaua kikatili mno.

Kocha wa Ahly Manuel Jose alishambuliwa na shabiki aliyepenya chumbani na baada ya tukio hilo baya kabisa maStaa Mohammed Aboutrika, Mohammed Barakat na Emad Moteab waliamua kustaafu soka.

Ligi ilisimamishwa na msimu kufutwa, kocha Manuel aliamua kuondoka haraka Misri na baadhi ya watu kadhaa walihukumiwa adhabu za kifo na jela.

Kwa Al Ahly shabiki ana thamani kubwa na katika kuenzi hilo mpaka sasa huvaa jezi namba 72 kwenye Warm up.

SOMA ZAIDI: Simba Na Yanga Mmejifunza Nini Ligi Ya Mabingwa?

 

1 Comment

  1. Pingback: Kufuzu AFCON 2025 Makundi Yatapangwa Kwa Vigezo Hivi

Leave A Reply


Exit mobile version