Baada ya tetesi kuvuma kuwa Kocha mkuu wa klabu ya Simba Abdelhak Benchikha ataondoka mwishoni mwa msimu kumekua na maswali mengi kwa wadau kuhusu tutegmee Simba ya aina gani msimu ujao? Kumbuka kuwa Simba imecheza michezo 21 kwenye ligi akishika nafasi ya 3 akiwa na point 46 huku akiwafikisha wekundu hao wa msimbazi hatua ya robo fainali ya CAF champions league.

Kuna kauli inasema “coaches are hired to be sacked “makocha wanaajiriwa ili kufukuzwa ila sababu za makocha hawa kufukuzwa au kuacha vibarua vyao vina sababu nyingi sitaki kutaka kusema nini nahisi kimemfanya benchika kujiuzulu nataka tu niwape tathmini ya hatima ya simba msimu ujao karibu…

Sitasema kwa kunyoosha kidole kuwa simba watakuwa bora au wabaya msimu ujao ila ninatoa  uchambuzi wa sababu ambazo zinaweza zikamfanya simba afanikiwe  tuanze kwa kujiuliza maswali haya .

Je, Simba wana tamaduni yao ya kiuchezaji (style of play) sidhani hata Yanga . Kitu hiki ni muhimu sana kwenye timu kwanini?

Inasaidia kujua unahitaji aina gani ya wachezaji ili waweze kufit katika style uitakayo sio kila mchezaji anafaa kwa kila tamaduni ya kiuchezaji ila kwa tanzania kocha ndio hutoa maamuzi ya jinsi ya timu kucheza

Hivo kocha  atachagua majina ya wachezaji anaohisi wanafaa kwa style yake swali je atapewa wachezaji hao au la asipopewa profile za wachezaji anao wahitaji its 0 work done tena

Simba inatakiwa kufanya assesment kuanzia ngazi ya management hadi ngazi ya chini kabisa kwa wachezaji kwanini ?  nitaeleza

Kuna quote inasema “Football is like life – it requires perseverance, self-denial, hard work, sacrifice, dedication, and respect for authority.” In Swahili, “Mpira wa miguu ni kama maisha – unahitaji uvumilivu, kujinyima, kazi ngumu, kujitoa, dhabihu, utayari, na kuheshimu mamlaka.”

Nikurudishe nyuma kidogo kama unajiuliza kwanini makocha 5 bila mafanikio simba basi jibu ni kujituma , kazi ngumu , kujitoa wachezaji wa simba wamekosa hiki kitu wamekosa tamaa ya kuipambania jezi nyeupe yenye nakshi nyekundu , jezi ya blue na nyekundu na ile nembo ya mnyama

Ili simba wawe bora inabidi wawe na uchungu na ile jezi kuanzia management hadi wachezaji

Ila pia recruitment ya wachezaji unao wasajili wana quality ya ku compete at international level mnaikunbuka simba yenye quality ndani na nje mfano niongelee safu ya kiungo (Mkude , lwanga , bwalya , chama ) hizi quality simba hazipo mfano tu mnajua simba wana msimu wa pili wanacheza bila kiungo mkabaji wa asili ?

Kuna quote inasema “It’s not whether you get knocked down, it’s whether you get up. Kwa kiswahili inasema sio kuhusu kupigwa chini ni kuhusu kusimama tena

Kwa nilichokieleza nakaa pande mbili za sarafu kichwa “simba ata vyema kama ata timiza niliyoyaandika “ mwenge “vice versa akishindwa kufanya hivyo vitu atakua kwenye level worse zaidi ya hii “

SOMA ZAIDI: Uwanja Wa Uhuru Ufanyiwe Marekebisho Maeneo Gani?

11 Comments

  1. Simba Ni taasisi ivyo benchika hata akiondoka tutegemee kuiona Simba bola.
    Kilicho Baki Ni viongozi kuangalia wapi wamefeli wafanye sajili za maana kuhusu swala la mwalimu kuondoka hata halinipi presha ili mradi Simba yangu ipo

  2. 𝐓𝐚𝐣𝐢𝐫𝐢 𝐀𝐁𝐀𝐒 on

    Kocha 𝗯𝗲𝗻𝗰𝗵𝗶𝗸𝗮 ni 𝗺𝘄𝗮𝗹𝗶𝗺𝘂 mzuri sana,sasa kama akiondoka
    Kwa 𝘀𝗶𝗺𝗯𝗮 hii wategemee kushuka daraja moja kwa moja
    By 𝐭𝐚𝐣𝐢𝐫𝐢 𝐀𝐁𝐀𝐒

  3. Benchika akiondoka simba hakutakua na mabadiliko makubwa kwa sababu simba shida sio kocha ni wachezaji kwa hiyo simba inabidi wawekeze pesa nyingi katika usajili ili kikosi chao kiwe bora na si vinginevyo

  4. Benchika siyo sababu ya Simba kuwa hivi ilivyo mana hâta kabla ya yeye kuja ilikuwa hivohivo me naona Simba ilifanya kosa kitambo sana kumruhusu senzo aende Yanga na manara mana hao walikuwa na mchango mkubwa WA kufanya Simba île imara …

  5. SHIDA NI BENCHIKA
    SHIDA WACHWZAJI
    SHIDA UONGOZI

    benchika anataka nni
    Wachezaji wanataka nni
    Uongozi unatakanni

    Aondoke abaki kama kinachofukuta hapo kitakua bado ivi ivi. Haina mana ya Benchika kubaki.

  6. Nadhani huu ni muda sahihi wa kujiulza kwanini Coach ajiuzulu?
    Ni kweli uongozi upo kama tunavyodhani?

    #Sio kawaida Coach kujiuzulu haswa Kwa apa Tanzania!

  7. Watajuta kwann benchika kaondoka’coz benchika ni moja kat ya walim bora baran afrika..na isitoxhe alishaanza kulizoea lig la bongo …pale simba problem ni uongoz….👈👈

Leave A Reply


Exit mobile version