Mpira wa miguu ni mchezo wa hisia sana kwani ni moyo ndio huzungumza kuliko hata mdomo lakini kubwa tunalopaswa kufahamu ni kuwa palipo na hisia kubwa kuna mstari pia wa kifo na uhai na ndio hapo hapo anaingia Henock Inonga na mashabiki wa Simba

Niseme tu kuwa soka ni kama mahusiano ya mapenzi ambayo huchipua popote na wakati mwingine mtu anaweza kupoteza hamu na kukitaka kitu kwa sekunde kadhaa tu! Ni mchezo wa kinafiki flan hivi.

Sio mbali sana kwani kuna barua iliandikwa hapa Kijiweni kuhusu Henock Inonga na nitanukuu kifupi “Inonga ni mchezaji mzuri mno… Masikhara yake au kujiamini sana akiwa na mpira vinaweza kuja kuharibu uhusiano wake na Simba SC…”

Bahati mbaya naona mada imegeuka ghafla na naona watu wanamshutumu kuwa alijivunja mechi dhidi ya Yanga SC lakini nikiri tu kuwa sifahamu sana hilo labda watu wanajua zaidi.

SOMA ZAIDI: Barua Nzito Ya Shabiki Kwa Viongozi Wa Simba Kuhusu Inonga

Wakati wa kupasha misuli moto kwa mazoezi madogomadogo siku ya dabi ya Kariakoo ni wazi kuwa alikua akionesha mashaka kwamba hawezi kumaliza ile mechi kwani alikua anaonekana kwamba hayupo ngangari zaidi kwa mchezo dhidi ya Yanga kutokana na kutokua fit

Baada ya mechi Kocha msaidizi wa Simba Seleman Matola akasema Inonga aliumia siku kadhaa mazoezini na walimchezesha wakiwa wanajua hilo Tafsiri yake!? “Aheri ya Inonga mgonjwa kuliko mabeki wengine wa Simba wazima”. Jamaa akiwa kwenye ubora wake ni daraja kubwa barani Afrika Tangu arudi AFCON anasemwa kwenye namna ngumu na ya kufikirisha huku wengine wanasema kabisa bora aondoke.

Ndio njia ya mpira wa miguu kwani wale wale walionisemea maneno mabaya na makali niliposema ana masikhara kwenye maeneo ya msingi leo wanataka aondoke na hapa ndio unaona kwamba Mpira una kijiunafiki flan ivv!

Mapenzi yakifika ukomo ndio utaanza kusikia harufu ya kibeberu kwa Bwana wako ama kusikia shombo la Samaki ozo kwa Manzi yako Mara chache Mapenzi yakaisha vyema… Muda mwingi huisha Kwa taabu

Naendelea kuamini kuwa ni Mapenzi tu ya mashabiki na Inonga yamefika mwanzo wa mwisho wao lakini Who will survive!? Henock… Ni miongoni mwa mabeki Bora wa kati waliopita nchini! Kwenye hili atatoboa!? Ni muda tu utasema kweli!

7 Comments

  1. Apoo na kubaliana na wew kabisa lakin kwa upande wangu Inonga nibeki moja safii sana ata akienda katika timu yoyote kubwa basii ata kuwa katika kikosi cha kwanza kuliko mchezaji yoyote pale Simba ni beki la viwango sana.

  2. Inonga ni mchezaji mzuri na mkubwa lakini Kuna mambo mengine anayafanya Hadi mdogo wake Salim mwenyewe anabaki anashangaa … Mpira WA siku hizi hautaki ucheze sana na jukwaa especially eneo anavocheza yeye ndo mana Ibra bacca alivowachukua chama n’a saidoo hakuwainua mashabiki Bali alifanya kuutoa mpira katika eneo lile sipati picha angekuwa Huyu mkojani…

  3. 𝗧𝗮𝗷𝗶𝗿𝗶 𝗔𝗯𝗯𝗮𝘀 on

    Unamaanisha kuwa 𝗶𝗻𝗼𝗻𝗴𝗮 ndie beki bora na bila yeye 𝘀𝗶𝗺𝗯𝗮 sii chochote?…lahasha!!! 𝗧𝗲𝗮𝗺 kiujumla ni mbovu kuanzia uongozi mpaka wachezaji wake.

    𝗧𝗮𝗷𝗶𝗿𝗶 𝗔𝗯𝗮𝗮𝗮𝘀

  4. Paul Emmanuel on

    Kiukweli henock ni beki bora sana ila aheri asiondoke ila aletewe mshindani mwingine kwenye nafasi yake kwasababu saivi akiondoka hapatakuwa na replacement yauhakika out of kazi Ko Bora
    Abaki aletewe mpinzani

  5. Hakika Inonga chuma , ila Wekundu wamezingua aisee wanatuumiza mashabiki Kuna watu wanaingizwa uwanjani kitimiza wajib tuu ila ubora ni zero percent, Kuna yule alikuwa anachangamsha team na walimuweka sub Kila match na akiingia anafanya maajabu ila wamemtoa #Moses Phiri😭

Leave A Reply


Exit mobile version