Michuano ya mataifa barani Afrika kwa mwaka 2023 inatarajiwa kuanza kufanyika kuanzia Januari 13 mwaka huu 2024 ni moja kati ya michuano ambayo inashirikisha timu nyingi zaidi na kukiwa na wachezaji wenye majina makubwa kutoka katika ligi mbalimbali barani Ulaya na wale wanaochezea ligi za ndani za bara la Afrika.

Licha ya kuwa hii ni michuano ya muda mrefu zaidi ya mpira wa miguu na ambayo kwa mara ya kwanza ilifanyika miaka 67 iliyopita lakini ni michuano migumu zaidi kubashiri nani ataibuka bingwa kwa kuvitazama tu vikosi vya timu zinazoshiriki.

Katika Makala 37 za michuano hii , nchi 15 pekee ndizo ambazo zimechukua ubingwa huu ambapo zile nchi kubwa zote zinazofahamika zimekwishachukua ubingwa huku baadhi ya nchi ndogo kama Zambia pia zikiwa miongoni mwa wale waliochukua ubingwa wakiutwaa mwaka 2012.

Kwenye miaka ya hivi karibuni AFCON imeweza kuchukuliwa na timu kubwa kama Algeria na Senegal japokua historia inaonesha kuwa katika michuano hii lolote linaweza kutokea na bingwa anaweza kuwa yoyote.

Licha ya umaarufu wake mkubwa aliokua nao na kuwa miongoni mwa wachezaji wenye rekodi za kufunga mabao mengi katika michuano hii lakini katika historia ya maisha yake hajawahi kuchukua ubingwa huu japokua alikua katika kikosi cha dhahabu cha timu ya taifa ya Ivory Coast kikiwa na wachezaji kama Yaya Toure na Gervinho na wengine wengi zaidi.

Katika moja ya mahojiano ambayo mchezaji maarufu wa kikosi cha Senegal na klabu ya Al Nasri aliwahi kunukuliwa akisema kuwa michuano hii ni moja kati ya michuano migumu ambayo amekua akishiriki kwani timu kadhaa kubwa na zile ndogo ambazo zinakua zimefuzu huwa zimekuja na malengo makubwa tofauti na kile ambacho mnakua mmekitarajia.

Ukiachilia mbali kuwa waandaaji wa michuano hii hawazungumzwi sana lakini ni moja kati ya nchi ambayo inapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ubingwa wa AFCON kwa mwaka huu kutokana na kuwa haizpigiwi chapuo la kuibuka bingwa wa michuano hii licha ya kuwa wana timu yenye wachezaji wazuri lakini pia wako katika ardhi ya nyumbani hivyo watapata mashabiki wengi wa kuwapa nguvu kupambana uwanjani.

Kinachovutia zaidi katika michuano ya mwaka huu ni namna ambavyo kila timu imejipanga kwa kuita wachezaji ambao wanadhani watafikisha mbali zaidi timu zao za taifa ambapo ukiwaangalia Senegali wao ni kama wamepania kuhakikisha kuwa wanaenelea kuutetea ubingwa wao ambao wameuchukua katika michuano iliyopita huku timu ya taifa ya Nigeria wao pia wakiwa na vipaji luluki haswa katika safu ya ushambuliaji wakitaka kuonesha kuwa wana kitu.

Hakuna ambaye hawezi kumuogopa Morocco haswa kutokana na kiwango bora ambacho amekionesha katika kombe la dunia na hapa atataka kuonesha kama ameweza kupambana na vigogo na kuwatoa katika kombe la dunia basi ni wazi anao uwezo wa kuchukua michuano hii ya AFCON kwa mwaka huu nchini Ivory Coast.

AFCON 2024: Nani Wanapewa Vipaumbele Vya Kuibuka Mabingwa?

Katika michuano ya mwaka huu zipo timu nyingi zaidi ambazo zimefuzu na zina vipaji kutoka kwa wachezaji wa timu kubwa kutoka bara la Ulaya lakini swali kubwa la kujiuliza ni nani ataibuka kuwa bingwa wa michuano hii? Hapa tunakuchambulia timu moja baada ya nyingine ambazo zinapewa kipaumbele kikubwa cha kuwa mabingwa;

Senegal :

Hawa ni mabingwa watetezi ambapo mwaka 2022 walichukua ubingwa huu kwa mara ya kwanza katika historia ya michuano hii ambapo ikawa timu ya 15 kuchukua kutoka Afrika Magharibi kuchukua ubingwa huu wa michuano ya mataifa barani Afrika. Walichukua ubingwa huu wakiwa chini ya kocha Aliou Cisse ambae ni miongoni mwa wachezaji wenye historian a kombe la dunia la mwaka 2002. Timu hii bado itakua ikimtegemea Sadio Mane kama ilivyokua msimu uliopita.

Ivory Coast:

Hawa ndio waanadaaji wa michuano hii kwa mara ya 2 katika historia ya michuano hii ya AFCON ambapo katika michuano hii wapo kundi moja na timu yay a taifa ya Nigeria, Equatorial Guinea na Guinea-Bissau ambao wote wapo kundi A.

Morocco

Bila shaka kiwango ambacho wamekionesha katika michuano ya kombe la dunia huwezi kuacha kuwaweka katika orodha hii ambapo walifika hatua ya nusu fainali ya kombe la dunia wakiwa na wachezaji ambao ndio hao hao wameenda nao katika michuano ya mataifa barani Afrika. Wana wachezaji mastaa kutoka timu mbalimbali barani ulaya ambao bila shaka wataonesha kitu katika michuano hii na sisi tusubiri kuona.

Algeria

Maswali mengi kwa wapenzi wa soka bila shaka na waalgeria ni kuwa watarudi katika kiwango chao kwani mwaka 2019 walishinda ubingwa wa AFCON kwa mara ya pili baada ya ukame wa miaka 29 bila kuchukua ubingwa huu. Licha ya hayo mwaka 2022 waliishia hatua ya makundi na kushindwa pia kufuzu kombe la dunia la Qatar wakiwa na kapteni wao Riyad Mahrez.

Nigeria

Kama ubingwa wa michuano ya AFCON ungekua unaenda kwa timu ambayo imetoa mchezaji bora wa mwaka wa CAF basi wangepewa the super eagles yaani Nigeria kwani wanaye Victor Osimhen lakini hilo haliwezekani na Nigeria wanatakiwa kutonesha katika michuano hii ubora wao kwani nao wana wachezaji wakubwa wenye majina makubwa katika bara la Ulaya.

Misri

Hii ndio timu ya taifa iliyochukua michuano hii mara nyingi zaidi ambapo wamechukua mara 7 ambapo mara ya mwisho kuchukua ilikua mwaka 2010 ambapo walichukua mara ya 3 mfululizo huu mwaka 2022 wakipoteza kwa matuta mbele ya Senegal. Katika michuano hii wanaingia na mchezaji wao mkubwa zaidi ambae ni Mo Salah anaekipiga Liverpool.

Je, Ardhi ya nyumbani itakuwa faida kwa Ivory Coast?

Ukilizungumzia bara la Afrika basi unatakiwa kujua kuwa kuna tofauti kubwa sana ya kanda ambazo nchi zinatoka kwani kuna ambao ukanda wao ni joto huku wengine ikiwa ni baridi na wengine kukiwa ni mvua hivyo baadhi ya nchi kucheza nyumbani mara nyingi imekua na faida kwao.

Kwasasa kucheza nyumbani imekua sio sababu kubwa ya kuchukua ubingwa kwani timu ya mwisho kuchukua ubingwa wakiwa nyumbani ilikua ni Misri tena ikiwa ni mwaka 2006 yaani unazungumzia makala 9 huko zilizopita na toka hapo hakuna timu ambayo ilifanikiwa kufika fainali ikiwa katika ardhi ya nyumbani.

Ukiachilia mbali Ivory Coast kuwa katika ardhi ya nyumbani lakini bado hawatajwi na kupewa nafasi ya kuibuka mabingwa wa michuano hii inayofanyikia nyumbani kwao licha ya rekodi kuwabeba kwani kwa mwaka 2023 wamepoteza mchezo mmoja pekee katika michezo 9 waliyocheza huku ushindi mkubwa zaidi ukiwa wa bao 5:1 dhidi ya Sierra Leone.

Licha ya michuano hii kutokua na timu inayopewa kipaumbele cha kuchukua ubingwa huu moja kwa moja lakini pia kuna wachezaji ambao wanatarajiwa kufanya makubwa katika michuano hii kama kutoka Nigeria ambae ni Victor Osimhen, huku Misri wakiwa na Mohamed Salah, mabingwa watetezi wa Senegal wakiwa na Sadio Mane lakini Ghana wakiwa na Mohammed Kudus na Guinea wakiwa na  Serhou Guirassy ambao wote wanacheza katika ligi kubwa duniani.

Kama ilivyo kwa wachezaji wakubwa licha ya kwamba wapo ambao wamechukua makombe makubwa barani Afrika lakini AFCON huwa ni kipaumbele kikubwa na huwavutia kupambana kwa ajili ya timu zao za taifa. Swali kubwa ni AFCON 2023 Itakua Ya Ushindani Zaidi Au Bado Hakutakua Na Jipya?

Endelea kufuatilia zaidi kuhusu AFCON kwa kugusa hapa.

Leave A Reply


Exit mobile version