Hatua ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuipa haki Tanzania kuwa moja ya nchi tatu zitakazoandaa fainali za Mataifa ya Afrika za mwaka 2027 (AFCON 2027) inatupa wasaa wa kuanza kufikiria upya viwanja vyetu vingi vilivyojengwa kwa viwango vya olimpiki, lakini havina hadhi hiyo kutokana na wamiliki kutoweka nguvu katika kumalizia ili vifikie viwango hivyo.

Tanzania, kama nchi nyingine zinazoshiriki michuano mikubwa ya mpira wa miguu barani Afrika inajitahidi kwa nguvu zake zote kuandaa na kuwa mwenyeji mzuri wa AFCON 2027 na miongoni mwa mambo muhimu yanayopewa kipaumbele ni maandalizi ya viwanja vya mpira wa miguu ambavyo ndio msingi wa mafanikio ya michuano hiyo.

Tunafahamu namna ambavyo baadhi ya viwanja vimekua vikifungiwa kutokana na changamoto mbalimbali na vikiwa ni viwanja muhimu kabisa kwa ajili ya michezo ya ligi kuu na baadhi ya mechi za FA ambapo ni hatua muhimu katika kuboresha viwanja vyake vya mpira wa miguu ili kuhakikisha wanavifanyia maboresho ili viweze kukidhi viwango vya kimataifa.

Kupitia ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi, kumekuwa na jitihada za kuboresha miundombinu ya viwanja kote nchini. Hii ni pamoja na upanuzi wa uwezo wa viwanja, kuboresha nyasi bandia au asilia, na kuhakikisha vifaa vya kisasa vinapatikana.

Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni, Tanzania inapanga kutumia viwanja kadhaa kwa ajili ya AFCON 2027. Miongoni mwa viwanja hivyo ni uwanja mkubwa wa Taifa unaofahamika kama Benjamin Mkapa Stadium uliopo jijini Dar es Salaam ambao umejulikana kwa kuwa kitovu cha matukio makubwa ya michezo nchini. Aidha, viwanja vingine vya miji mikubwa kama Arusha, Dodoma, na Mwanza pia vinaweza kuchaguliwa kama vituo vya michuano.

Pamoja na uboreshaji wa viwanja, Tanzania inaweka mkazo mkubwa kwenye mipango ya usalama na urahisi wa mashabiki watakaohudhuria michuano hiyo. Hii ni pamoja na utoaji wa huduma bora za usafiri, malazi, na mifumo madhubuti ya usalama ili kuhakikisha wageni wanajisikia salama na wanafurahia uzoefu wao wakati wa AFCON 2027.

Mbali na maandalizi ya kimuundo,mipango ya kukuza michezo na kuhamasisha vijana kushiriki katika mpira wa miguu. Programu za maendeleo ya vipaji, mashindano ya vijana, na ujenzi wa viwanja vya mpira wa miguu katika maeneo ya vijijini ni sehemu ya juhudi za nchi hiyo kuhakikisha kuwa michuano ya AFCON inaleta athari chanya kwa jamii na inaendeleza michezo kwa ujumla.

Kupitia maandalizi ya AFCON ya Pamoja ya mwaka 2027 itakayokua ya nchi ya Tanzania,Kenya na Uganda nchi zote hizi zinaonesha dhamira yake ya kuwa wenyeji bora na kuchangia kukuza mpira wa miguu barani Afrika. Uboreshaji wa viwanja, mipango ya usalama, na kukuza vipaji ni mambo muhimu yanayoonyesha azma ya AFCON PAMOJA ya 2027 katika kuandaa michuano mikubwa na kuifanya kuwa tukio la kuvutia kwa wapenzi wa mpira wa miguu duniani kote.

SOMA ZAIDI: Wachezaji Taifa Stars Hawakuutaka Ushindi

Leave A Reply


Exit mobile version