Msafara wa wachezaji, viongozi wa serikali na wa klabu ya Young Africans SC (Yanga SC) pamoja na baadhi ya mashabiki umewasili salama nchini Algeria tayari kwa mchezo wa hatua ya pili ya fainali baina ya klabu ya Yanga sc na Usm Algers ya nchini humo utakaofanyika siku ya juni 3 saa nne usiku.
Mchezo wa pili wa fainali utakua na kombe uwanjani na mshindi wa jumla atavalishwa medali ya ubingwa ambapo katika mchezo wa awali hapa jijini Dar es salaam Yanga sc ilikubali kipigo cha mabao 2-1.
Yanga sc katika msafari wameongozwa na Waziri wa Utamaduni,sanaa na michezo Mh.Balozi Dkt Pindi Chana aliyeambatana na wakuu wa Taasisi zilizochini ya wizara hiyo pamoja na Naibu Katibu mkuu Mh.Hamis Mwinjuma sambamba na mashabiki kadhaa waliochaguliwa kwenda kuwakilisha na kuongeza hamasa katika mchezo huo.
Msafara huo uliondoka majira ya mchana Juni mosi kwa ndege maalumu ya Boeng iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuongeza hamasa kwa klabu ya Young Africans SC katika ushiriki wake mzuri katika michuano hiyo ambapo baada ya kuwasili msafara huo ulipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini humo sambamba na baadhi ya watanzania wanaosoma nchini humo.