Baada ya kuona kile ambacho wamekutana nacho Chelsea katika dimba la Anfield hii leo ligi kuu ya Uingereza inaendelea ambapo Wolves anamkaribisha Man Utd katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza katika uwanja wa Molineux.
Wolves anaingia katika mchezo huu akitoka kumfunga mpinzani wake mkuu West Brom mabao 2:0 katika mchezo wa raundi ya nne ya kombe la FA huku Man Utd wao wametoka kumfunga Newport mabao 4:2 katika michuano hiyo hiyo ya AFCON.
TAKWIMU
Wolves ambae ndio mwenyeji wa mchezo anaingia katika mechi hii akiwa nafasi ya 11 katika mechi 21 amekusanya alama 29 wakati Man Utd anaingia katika mchezo huu akiwa nafasi ya 9 na pointi 32 katika mechi 21 ambazo amecheza mpaka sasa.
- Toka mwaka 2010 mpaka 2023 katika mechi 10 za ligi kuu ambazo wamekutana kumekua na ufinyu wa magoli ambapo hayajawahi kuzidi manne katika mechi 1 huku katika mechi za mashindano yote karibia mechi 112 Man Utd ameshinda mechi 55 huku Wolves wakishinda mechi 37.
- Mechi yao ya mwisho kukutana Man Utd alishinda kwa 1:0
- Wolves wako katika kiwango bora sana kwa sasa kwani hawajafungwa mechi 9 nyumbani toka mwaka jana mwezi wa 9 wakishinda 6 na kusare 3.
- Manchester ameshinda katika kipindi cha kwanza katika mechi 3 pekee kati ya 21 alizocheza msimu huu.
TUNABETIJE?
Mechi za katikati ya wiki mara nyingi huwa na matokeo ya kushangaza kama ambavyo imekua katika AFCON. Ni wazi sasa ni muhimu kufuatilia takwimu zaidi na kuweka ubashiri katika masoko ambayo ni rahisi zaidi.
- Kwa wale wa magoli tunaweza kuamua kuchagua haya
1st Half Under 3.5,
Total Goals on The Match Under 4.5
- Kuna uwezekano wa kufungana hivyo Both teams to score YES.
SOMA ZAIDI:Ligi Za Kuziepuka Wakati Wa Betting