Katika dimba la London lenye uwezo wa kuingiza mashabiki takribani elfu sitini na mbili n amia tano (62500) ndipo ambapo mchezo kati ya Westham dhidi ya Brighton utapigwa katika muendelezo wa mechi za ligi kuu ya Uingereza.
Westham akiwa nafasi ya 6 katika msimamo wa ligi ambao katika mechi 19 amejikusanyia alama 33 huku Brighton akiwa nafasi ya 8 ambapo katika mechi 19 amejikusanyia alama 30 ambapo ni tofauti ya alama 3 pekee baina ya timu hizi.
Katika mchezo huu wagonga nyundo wa jiji la London wanaingia huku wakiwa wameshinda mechi 4 na kupoteza mechi 1 pekee katika mechi 5 za mwisho za mashindano yote aliyocheza huku Brighton wao wakiingia katikamchezo huu na matokeo ya kusuasua kwani katika mechi 5 za mwisho ameshinda mechi 2 na kusare mechi 2 na kupoteza mchezo mmoja.
Licha ya muendelezo mbovu huo wa matokeo lakini Brighton ameonekana kuwa mbabe pale anapokutana na Westham kwani ameshamfunga mara kadhaa na kutoka nae sare pia licha ya kuwa mchezo huu utakua mgumu sana.
VIDOKEZO VYA UBASHIRI
Bila shaka hii ni mechi ambayo ni ngumu sana kumpa mmojawapo ushindi wa moja kwa moja licha ya viwango ambavyo wamekua wakivionesha katika michezo kadhaa iliyopita hivyo unaweza anza kwa kumpa yoyote ashinde katika mechi hii ( 12)
Lakini pia kwa wale ambao wanapenda kuweka ubashiri wa magoli ni kuwa mechi inayowakutanisha wababe hawa mara nyingi huwa na idadi ya magoli kuanzia moja na kuendelea yaani Over 1.5.
Kama ni ngumu kwa magoli basi unaweza kusema kuwa Westham wapate angalau bao moja katika mchezo huu yaani Westham Over 0.5 Goals.
Endelea kufuatilia vidokezo vya ubashiri kwa kusoma hapa.