Klabu ya West Ham United imemsajili kiungo James Ward-Prowse kutoka Southampton kwa ada inayokadiriwa kuwa karibu pauni milioni 30.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 28, amejiunga na Hammers kwa mkataba wa miaka minne.
Ward-Prowse aliungana na Southampton akiwa na umri wa miaka nane na amecheza michezo 410 ya ngazi ya juu pamoja na kuwa nahodha wa klabu hiyo, ambayo ilishushwa daraja msimu uliopita kwenda Championship.
“Nimechangamka kuwa hapa West Ham United,” alisema.
“Kutoka nje, unapoangalia, hii ni klabu ambayo imekuwa ikipanda kwa miaka kadhaa sasa na baada ya mafanikio katika Ligi ya Ulaya ya Europa msimu uliopita, unaweza kuhisi kuna msukumo halisi katika klabu hii.”
Meneja wa West Ham, David Moyes, alisema: “Amefanya vizuri sana katika Ligi Kuu kwa muongo uliopita, akiendelea kutoa matokeo mazuri msimu baada ya msimu.
“Uongozi wake ni jambo kubwa zaidi kwetu – atakuwa sauti muhimu kwetu, mtu ambaye atawaongoza wenzake kutoka katikati ya uwanja.”
Ward-Prowse alifanya debut yake na Saints akiwa na miaka 16 katika mchezo wa EFL Cup dhidi ya Crystal Palace mwezi Oktoba 2011, huku akiichezea mara ya kwanza Ligi Kuu siku ya ufunguzi wa msimu wa 2012-13.
Anajulikana kwa ustadi wake wa kupiga mipira ya seti, ni David Beckham pekee ambaye amefunga magoli zaidi ya 17 kutokana na mipira ya adhabu moja kwa moja katika Ligi Kuu.
Southampton ilisema Ward-Prowse, ambaye aliteuliwa kuwa nahodha wa klabu mnamo 2020, ni “moja ya vipaji bora kuwahi kutoka kwenye akademi ya Saints”.
Taarifa ilisema: “Uaminifu wake kwa Southampton FC kwa zaidi ya miongo miwili, uweledi wake uwanjani na nje ya uwanja, na mchango wake katika jamii unamaanisha anondoka akiwa na urithi wake kama shujaa wa Saints vema na kwa hakika umethibitishwa.”
West Ham, wamekuwa wakijaribu kumsajili Ward-Prowse kwa sehemu kubwa ya majira ya joto.
Kuwasili kwake kunafuatia kiungo wa Mexico Edson Alvarez kujiunga na Hammers kutoka Ajax kwa ada inayokadiriwa kuwa pauni milioni 35.
Soma zaidi: habari zetu kama hizi hapa