Hamu na shauku kubwa ambayo watanzania wengi walikua nayo katika michuano ya mataifa barani Afrika bila shaka ilikua kuitazama timu yao yaani Taifa Stars ambao walikua na mchezo mgumu wa kwanza wa kundi F dhidi ya Morocco kwa kupoteza kwa mabao 3:0 ambapo katika kundi hilo kuna timu zingine kama Zambia na DRC Congo.
Shida moja ambayo mashabiki wa soka kutoka Tanzania wamekua nayo ni kuingilia baadhi ya majukumu ya kocha na kutoamini uwezo wa baadhi ya wachezaji ambao wamekua wamepangwa katika kikosi kwa ajili ya mchezo husika.
Kabla ya kuanza kwa michuano hii kocha aliweka wazi kabisa kuwa katika michuano hii tunaenda kwa ajili ya kujifunza na kuona tunatengeneza vipi timu kwa ajili ya kuwa na ushindani katika michuano ambayo tutakua nyumbani lakini kwa namna nyingine wapo watanzania ambao wana hoja nzuri tu kuhusu ubora wat imu yetu.
Katika michuano hii ya AFCON kwa mwaka huu hatutegemei kufanya lolote la ajabu na hatumdai maajabu, tunajua hatuna hiyo timu ya kufanya maajabu lakini hatuwezi Kwenda uwanjani kama kuku asie na kichwa unajua tunatakiwa tufungwe huku tuone tunacho kicheza, sio tubumbe bumbe kisha tujifiche kwenye kichaka cha kujifunza.
Tatizo letu kubwa watanzania ni kwamba tushazoea sana uongo kutoka kila mahali haswa namna ambavyo wachambuzi wamekua wakichambua baadhi ya wachezaji na kuona bora huyu au yule lakini tunatakiwa kufahamu kuwa kocha ndio ambaye anakaa na wachezaji kambini lakini pia ndio anayefanya mazoezi na wachezaji. Anatambua kabisa yupi wa kuanza nae na kwanini aanze na yupi sio wa kuanza nae na kwanini asianze hii ndio tunapaswa kufahamu.
Kocha wa timu ya Taifa Stars ana jukumu kubwa la kuongoza na kuboresha kiwango cha timu ili kufikia mafanikio makubwa. Hata hivyo, mara nyingine, mashabiki na wadau wa mpira wa miguu wanaweza kuwa na shinikizo la kutaka matokeo haraka na kusahau umuhimu wa kumpa kocha muda wa kufanya kazi yake kwa ufanisi.
Mara nyingine, mafanikio ya timu ya Taifa yanaweza kutegemea sana maendeleo ya vipaji vya vijana. Kocha anahitaji muda wa kuona matunda ya juhudi zake katika kuendeleza wachezaji chipukizi. Subira kutoka kwa mashabiki ni muhimu katika kipindi hiki cha mabadiliko.
Kuna wakati shinikizo kutoka kwa mashabiki na vyombo vya habari kunaweza kusababisha mazingira yenye msongo wa mawazo kwa timu na kocha. Kumpa kocha muda wa kufanya kazi yake kwa amani kunaweza kuzuia kuvuruga mazingira na kusaidia kujenga umoja ndani ya timu.
Ni muhimu kuelewa kuwa mafanikio ya timu ya Taifa Stars hayawezi kutokea mara moja. Subira, imani, na msaada kutoka kwa mashabiki, uongozi, na vyombo vya habari ni muhimu kwa mafanikio ya muda mrefu. Kumpa kocha nafasi ya kufanya kazi yake kwa amani ni uwekezaji muhimu kuelekea kufikia malengo ya muda mrefu ya timu.
Endelea kusoma makala mbalimali kutoka Kijiweni kwa kubonyeza hapa.
1 Comment
Pingback: Huu Ni Wakati Sahihi Wa Kuruhusu Uraia Pacha Taifa Stars - Kijiweni