Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu kiasi kuizungumzia klabu ya Simba moj kati ya mashabiki wakubwa na mbunge Hamisi Kigwangalla ameibuka na waraka mzito kuhusiana na yale yanayoendelea ndni ya viunga vya Msimbazi na waraka huo kauandika hivi,
โLabda mpeni timu Kigwangallaโฆโ ni kauli ya mwanaYanga mmoja kwenye clip inayozunguka โvirallyโ mitandaoni. Mwishoni wanacheka kwa mzaha na dharau kama vile mimi kupewa timu Ya Simba ni mzaha fulani hivi!
Iko hivi; siyo kwamba sina uwezo wa kuiongoza Simba kwa mafanikio makubwa zaidi ya haya, ama sina uwezo wa kuinunua Simba ama kununua hisa za Simba. NAWEZA SANA!
Inawezekana sina hiyo pesa kwenye akaunti zangu, lakini nina taarifa na maarifa ya wapi naweza kupata hizo pesa na kuinunua Simba! Ukiwa na โmindsetโ ya kimaskini na hauna maarifa utaona mtu kama mimi siwezi kununua mali ya TZS 20bn. Waswahili huwa tunajidharau sana kwa sababu utumwa umegoma kutoka vichwani mwetu.
Binafsi, niliikataa hii โslavery mindsetโ nikiwa mdogo sana, ndiyo maana mimi na wenzangu tuliweza kununua kampuni kubwa kabisa ya kununua mazao yenye thamani ya zaidi ya bilioni 7 wakati ule (mwaka 2007), nikiwa na umri wa miaka 32, tena nikiwa โnobodyโ na sina โnetworkโ yoyote ile (kama nilivyo leo!).
Sema kwa sasa hivi siwezi kusema nanunua Simba, siyo kwa sababu sina uwezo wa kuinunua lakini ni kwa sababu ya kuepuka โconflict of interestโ (mgongano wa kimaslahi) maana nimekuwa mkosoaji mkubwa wa jinsi mchakato huu ulivyoendeshwa, na kimaadili siyo sawa kutamani kuwa na hisa maana itaonekana kumbe kelele zangu zote ni kwa sababu nilikuwa nina wivu na mwekezaji wa sasa.
Halafu, niwaambieni kitu Simba ni brand kubwa nchini na Afrika kwa sasa. Na inazidi kukua. Ikiwekwa mifumo mizuri ya usimamizi na ya kifedha, wanunuzi wa Simba hawawezi kukosa kujitokeza.
Sasa hivi kila mtu anaogopa kuingia humo, haswa baada ya kuona figisu figisu zilizopo na kutokamilika kwa โtransactionโ ya manunuzi na huyu mwekezaji wetu kwa zaidi ya miaka 6 leo!
Ukitaka kuona Simba inapata wawekezaji wengi na wazuri ni lazima uweke โMUUNDOโ mzuri wa utawala na usimamizi wa club; aidha uwe na โMUUNDOโ mzuri wa umiliki wa hisa za Simba.
Mfano: kwa nini Mwenyekiti wa Club (anayetokana na wanachama) na Mwenyekiti wa Bodi (anayeteuliwa na mwekezaji) wasiwe wanapokezana cheo Cha Rais wa Club na Makamu wa Rais wa Club (say kila baada ya miaka mitatu)? Na kwamba Rais akiwa ni Mwenyekiti wa Club ya wanachama basi Mwenzake automatically anakuwa Makamu na vice versa! Na kwa vyovyote vile anayekuwa Rais anakuwa na mamlaka yote!
Ama, ni kwa nini mwekezaji awe mmoja? Kwa nini tusiseme – asilimia 49 ya hisa za Simba ni lazima zimilikiwe na wawekezaji wasiopungua watatu na kwamba hakuna mwekezaji mmoja kuwa na hisa zinazozidi 20%, na wawekezaji pengine wasizidi idadi fulani?!
Ukirekebisha haya na ukasema hisa hizi zitauzwa kwa zabuni za siri za โUSHINDANIโ, utaona watajitokeza wawekezaji wengi na hisa zitauzwa kwa bei kubwa zaidi maana watapigana vikumbo pale!
Na ukisema unaweka wazi mikataba yote ya matangazo ya bidhaa, mauzo ya merchandise, migao ya viingilio, manunuzi ya wachezaji, makocha na waajiriwa wengine! Unachapisha hesabu kwenye majarida ya wazi; utaona watu wengi watajitokeza kuwekeza!
Muhimu: kuwe na nia njema na ya kweli ya kutaka kuleta mageuzi ya kweli ya uendeshaji wa club na siyo janja janja ya wachache waliogeuza club chanzo chao cha kujipatia โmaishaโ ama kukuza โbrandโ zao binafsi.
Mdau wa KIJIWENI wewe una lipi la kusema? Tuambie kwenye comment hapa chini
22 Comments
good broodah
Daaah kweli wawekezajii wawe hataa zaid ya wawilii kama vp kweliii
always yuko sahihi ila shda inakuja tu pale wabongo hatupend kuambiwa ukwel ndo tatz letu
Ni akili kubwa sana inatakiwa kutumika ili Simba wamweleee huyu jamaa tangu zamani alishaona vile ambavyo Simba inapotea alipouliza tyu akaambiwa msaliti sisi watu weusi bado hatuaminiani wewe jaribu kuanzisha mchakato wote wa mabadiliko mahali Fulani utaambiwa unataka jambo Fulani
Mm Imani yangu Africa tungemua kutumia akilizi zetu halisia hakika hao tunaowaita weupe Kila siku wangekuwa kwetu kujifunza
Unaenda marekani kujifunza mfumo Fulani unakuta waalimu hasa ama waanzilishi ni watu kutoka bara la Africa
Angalia wacheza soka, angalia viongozi mashuhuri wengi ni weusi, Nenda kwenye Vipaji vikubwa vya Music why tuna akili ya kubebewa
Uhalisia alichokisema kigwangala hakuwezi kutekelezwa kwa sababu wengi wanataka faida kwanza kuliko manufaa ya timu kwa miaka mia mbili ijayo
Bora timu apewe kigwangwala maana ana maono mapana zaidi
Nimemuelewa sana hisa zipambaniwe na watu kama mnada na mwekezaji asiwe mmoja right kabisa
Huo ni ukweli mtupu na usio pingika
Yupo sawa apewe tu simba
Sema kigwangala ana point sana, muundo wa simba sc sio rafiki kabisa, leo hii mangungu ni Mwenyekiti wa wanachama wanaomiliki hisa asilimia 51% lakini wanaoonekana na kupewa heshima ni viongozi wa mwekezaji, Mangungu apewe heshima yake please, mambo ya rais wa heshima ๐๐ tungeachana na mambo ya uchawa, watu wapewe majukumu wachape kazi.
Afu pia kuhusu uwekezaji Yanga wamefanya vizuri sana, sio vibaya kuiga mambo mazuri ๐๐ Simba nao waige tu, systems yaku recruit wachezaji nayo ibadilishwe, kila mwaka wanaleta wachezaji ambao hawana input kwenye timu mwisho wa mwaka wanaanza kubanana kuvunja mikataba ๐ โโ๏ธ๐ โโ๏ธ
Alichoandika kigwangala yupo sahihi kabisa lakini kwawasio na uelewa bado wataponda tatizo lililopo hao viongozj hapo waliopo kula yao ipo hapo haiwezekani mwenyekiti wa club hana PAWA kwenye anakua kama mtumwa nawakati yeye kashikilia hisa asilimia 51 za wanachama huyu mwenye asilimia 49 ndio mwenye nguvu
Mwamba kanena vizuri sana…ishu n utekelezaji2 wabongo hatupnd kuambiwa ukweli๐๐
Simba sc kuna shida kubwa tena sana..upande wa viongozi…hata mhindi wetu nae n mjanja mjanja tu..na huwa anaibuka wakati wa changamoto ya matokeo anapoozesha upepo kwa maneno then anapiga kimya..inawezekana hata pesa ya usajili hatoi ya kueleweka..lakn pia udalali ni mwingi ndani ya timu
Ni kweli yaani hicho unacho ongea simba wajipange kwa msimu ujao ili waboreshe timu
Uko sawa mkuu ๐๐
Naitamani sana simba ya manara na babra irudi kisha mangungu na jaribu tena ( try again ) waondoke simba tena wasiruhusiwe hata kuingia uwanjani wakati simba inacheza๐
Angeongea kiingereza ndo wabongo tungemzingatia ila point hata iwe nzito kivipi ila ukawa tu kwa kiswahili wabongo hatunaga muda nayo ๐๐๐
” Kitu cha hovyo kikisemwa kwa lugha ya kigeni kitaonekana cha maana sana ” alisikika baba WA taifa Mwl Nyerere J. K
Daaah kweli wawekezajii wawe hataa zaid ya wawilii kama vp kweliii
Kigwangara Hana uwezo wa kuimiliki ๐ฆ๐๐ ๐๐. Wala ๐๐ถ๐บ๐ฏ๐ฎ haina matatizo saaaaana sema tu ni suala la mda watajipata tu wasife moyo,kinachotakiwa warekebishe pale wanapoona panavuja ๐บ๐๐ถ๐บ๐ ujao na wao wafanye vizuri.
by ๐๐ฎ๐ท๐ถ๐ฟ๐ถ ๐๐๐๐๐ฆ.
Pingback: Pale Simba Shida Sio Mangungu Ni Wachezaji Hawa - Kijiweni
Pingback: Mchezaji Gani Wa Nje Hapa Ligi Kuu Amekuwa Bora Zaidi Kwako? - Kijiweni
Pingback: Viongozi Simba Wanajiroga Wenyewe Na Kujitega Mtego Mbaya - Kijiweni
Shida hipo pande zote mbili:
*Kwanza upande ea muwekezaji, yani huyu MO cjui tuseme hajui majukumu yake au lah mana amewaamini xana hao viongoz wake kina mangungu na amewaachia mamlaka yote ya usimamizi wa timu yeye akiwa bize na biashara zake binafsi.
*Pili ni hawa viongozi, mangungu na mwenzake “try again” wanautumia vibaya uhuru waliopewa na kugeuza taasisi kama sehemu yao ya kuingiza vipato vyao binafsi ndo mana wanaondoka wachezaji wazuri kina baleke na kina phiri tunaletewa kina jobe.