Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania Adel Amrouche ameteua wachezaji 53 kwa ajili ya kikosi cha awali cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kuelekea Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika kuanzia Januari 13 hadi Februari 11 mwakani nchini Ivory Coast.
Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), idadi hiyo itapunguzwa hadi kubaki wachezaji 27, ingawa ni 23 tu watakaoruhusiwa kucheza Fainali hizo za tatu kwa Taifa Stars baada yam waka 1980 nchini Nigeria na 2019 nchini Misri, kote wakitolewa hatua ya makundi.
Taifa Stars imepangwa Kundi F pamoja na Morocco, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Makipa; Beno David Kakolanya (Singida Fountain Gate), Aishi Salum Manula (Simba SC), Aboutwaleeb Mshery (Yanga), Kwesi Zion Pira Kawawa (IFK Haninge, Sweden) na Metacha Borniphace Mnata (Yanga SC).
Mabeki; Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ (Simba SC), Kennedy Wilson Juma (Simba SC), Dickson Nickson Job (Yanga SC), Bakari Nondo Mwamnyeto (Yanga SC), Ibrahim Abdallah Hamad ‘Bacca’ (Yanga SC), Lusajo Elukaga Mwaikenda (Azam FC), Nickson Clement Kibabage (Yanga SC), Haji Mnoga (Aldershot Town, England), Abdi Hassan Banda (Richards Bay FC, Afrika Kusini), Zion Chebe Alban Nditi (Aldershot Town, England).
Viungo; Novatus Dismas (FC Shakhar Donetsk, Ukraine), Edwin Charles Balua (Tanzania Prisons), Abdulmalik Adam Zakaria (Namungo FC), Omar Abbas Mvungi (Nantes B, Ufaransa), Muzamil Yassin Said (Simba SC), Sospeter Israel Bajana (Azam FC), Baraka Gamba Majogoro (Chippa United, Afrika Kusini), Feisal Salum Abdallah (Azam FC), Mudathir Yahya Abbas (Yanga SC), Morice Michael Abraham (RFK Novi Sad, Serbia), Himid Mao Mkami (Talaea El Gish, Misri) na Ladaki Juma Chasambi (Mtibwa Sugar).
Washambulaji; Mbwana Ally Samatta (PAOK FC, Ugiriki), Saimon Happygod Msuva (JS Kabylie, Algeria), Roberto Yohana Nditi (Forfar Athletic FC, Scotland), Kibu Denis Prosper (Simba SC), Abdul Hamisi Suleiman ‘Sopu’ (Azam FC), Ben Anthony Starkie (Basford United FC, England), Matheo Anthon Simon (Mtibwa Sugar), Kokola Charles M’mombwa (Macarthur FC, Australia), Joshua Ibrahim Mwakasaba (Tusker FC, Kenya), Clement Francis Mzize (Yanga SC).
Endelea kusoma zaidi habari zetu kwa kugusa hapa.