Ukizungumzia miundombinu ya michezo basi huwezi kuacha kutaja Bara la Afrika kwani lina viwanja vikubwa kadhaa ambavyo huvutia idadi kubwa ya watazamaji pale yanapofanyika matukio mbalimbali ya kimichezo na burudani.
Viwanja hivi vimejengwa katika nchi kadha wa kadha za barani Afrika na makala hii itatazama viwanja kutoka nchi kadhaa na kuangalia ukubwa wake kwa idadi ya watazamaji wanaoingia katika viwanja hivyo na tutaanza na:
Stade Olympique de Radès – Tunisia
Uwanja huu unapatikana nchini Tunisia na una uwezo wa kuchukua watazamaji takribani elfu sitini na tano (65,000). Ulijengwa mwaka 2001 na umekua ukitumiwa na timu ya taifa ya Tunisia lakini pia na matukio mengine ya kimichezo.
Cairo International Stadium – Misri
Kama ulikua hufahamu tu ni kuwa huu upo katika orodha ya dunia kikishika namba 69 kwa ukubwa duniani. Lakini pia ni miongoni mwa viwanja vikubwa barani Afrika ikiwa na uwezo wa kuchukua takribani watazamaji 75,000. Uwanja huu unatumiwa na timu ya taifa ya Misri Pamoja na mechi za vilabu barani Afrika.
FNB Stadium (Soccer City) – Afrika Kusini
Ni uwanja unaopatikana katika jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini. Una uwezo wa kuingiza watazamaji takribani 94,700. Kumbukumbu kubwa kuhusu uwanja huu ni Pamoja na kutumika kwake katika michuano ya Kombe la Dunia la FIFA mwaka 2010.
Stade 5 Juillet 1962 – Algeria
Uwanja huu unatumika na timu ya Taifa ya Algeria na una uwezo wa kuchukua watazamaji takribani 95,000. Ulijengwa mwaka 1972 na ni miongoni mwa viwanja vikubwa vinavyopatikana nchini Algeria lakini pia umekua ukitumika katika shughuli za michezo Algeria.
Stade Mohammed V – Morocco
Huu unapatikana katika jiji la Casablanca nchini Morocco. Mara nyingi hutumiwa na timu ya taifa ya Morocco na mechi nyingine za ligi kuu nchini humo. Una uwezo wa kuingiza takribani watazamaji 67,000.
Unaijua michezo nane (8) hatari zaidi duniani? Gusa hapa kusoma Makala hii sasa
1 Comment
Pingback: YANGA Yatakiwa Kulipa Uharibifu Kwa Mkapa Kijiweni Ligi Kuu | Soka la Bongo -