Serikali ya Tanzania imeingia mkataba na kampuni ya ukandarasi kutoka China kukarabati uwanja wa Uhuru uliopo Dar es salaam kwa gharama ya shilingi bilioni 19.7.
Ukarabati wa uwanja huo utatumia miezi 12 ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika #AFCON2027
Mdau Wa KIJIWENI unatamani maeneo gani yafanyiwe marekebisho makubwa zaidi kwa gharama hizo ambazo zimetajwa za kuukarabati uwanja huu?
CHANGIA MADA HII PIA: Mchezaji Gani Wa Nje Hapa Ligi Kuu Amekuwa Bora Zaidi Kwako?
17 Comments
Ulekebiswe pitch, na majukwaa pia ili idadi ya washabiki tuwe na eneo kubwa la kupoa kuchek gemu
Pitch na majukwaa afu mamb ya kapet kizaman hyo wenzetu wameachaga hzo bhna sema nn uwanja wa uhuru sjawah ukubali😁
Unahitaji maboresho Sana hususani pale kwenye jukwaa la mashabiki,, inabidi kuwapo kwa eneo kubwa kwa mashabiki pia katika eneo la bench la ufundi. Yote na yote ,lazmza kuboresha taa ,, pitch pamoja na viti .
Utengenezwe sehemu ya kuchezea yani pitch
Sehemu ya kukaa Bench la ufundi. Pamoja na majukwa
wauezeke yaani inyeshe, liwake apo kipigwe tu.
Majukwaa ya sie watu wa kijiwen yaongezeke yawe mengi
Nasubir mualiko admin
Wanarekebisha viwanja wachezaji wazawa hawasaidiwi kwenda popote sasa viwanja vya nini😒
Kama mchezaji anatoka yanga kwenda azam unafkir ana malengo ya kwenda mbali huyo? Sametime wachezaji wenyew hawatak kujtuma viwanja vitengenezwe hvo hvo
Eneo la pitch na pia eneo la mashabiki wajaribu kufanya ukarabati uwanja uwe level ya New Amaan Complex
Uwekwe tas
Kiufupi uwanja wa uhuru sio wa kisasa, ulihitaji marekebisho makubwa mno. Kuanzia kwenye pitch, majukwaa, vyooni dressing room na ikiwezekana uwekwe hadi taa
Ngoja nikazie kwenye camera 📸 maan uwanja una camera chache pia zipo mbali
Uwekwe vigae kwenye pitch
Waweke VAR na cam za azam humohumo tuone wanavyo fanya kazi yasije yale ya masandawana goli lina ingia VAR inakataa … Inaonekana wanajalidiligi humo ndani kutoa video za uongo…. tunataka tuwaone wanavyo fanya kazi zao
Kaka tupe updates za derby ya wanawake
Pingback: Akiondoka Benchika , Tutegemee Simba Gani Msimu Ujao? - Kijiweni