Kwa dakika 90 za Mzizima Derby unaweza kusema kuwa Azam FC walikuwa bora sana kwenye mipir ya kushtukiza huku wakiwa na kasi kubwa sana katika kushambulia na hiyo ni kutokana na wao kuwa bora pamoja na wachezaji vijana wenye kasi katika timu yao.
Goli la kwanza la mchezo lilipatikana kutokana na kasi ya Azam FC kuwa kubwa kwa “movement” ya beki wa kushoto Pascal Gaudence Msindo pia Abdul Sopu, Feisal Salum pamoja na Gibril Sillah wakiwa ni wachezaji waliyokuwa na kasi ndani ya mchezo huu ambao umechezwa katika uwanja wa CCM Kirumba.
Kwa ujumla kabisa timu zote mbili kwa nyakati tofauti walionekana kuwa watulivu sana hususa ni kikosi cha Simba SC licha ya kuwa nyuma kwa goli 1-0 ila walikuwa watulivu sana mpaka pale walipopata njia sahihi za kuwafungua Azam na kupata bao la pigo huru katika dakika za nyongeza zilizowapa bao klabu ya Simba.
Utulivu huo uliifanya Simba SC kuendelea kucheza kwenye mbinu yake na hata goli lao la kusawazisha lilichangiwa na utulivu wao kuanzia nyuma kwenda mbele kufanya shambulizi naamini kuwa kama Azam FC wangekuwa watulivu kwenye mchezo huu wangefanikiwa kuondoka na ushindi kwani ni nafasi nyingi wamepata tofauti na Simba SC.
Kwa nyakati tofauti tofauti makipa wa pande zote mbili waliibuka mashujaa kwa timu zao kwa kuokoa mipira “Save” ambazo ziliendelea kuwaweka mchezoni.Ukiutazama mchezo wote kwa ujumla wake umetoa Save 6 za hatari ambapo 2 zimepatikana kwa upande wa Simba SC na 4 kwa upande wa Azam FC, huku makipa wote wakionyesha utulivu langoni mwao na kuwa sehemu ya mchezo kwa kuhusika kuanzisha mashambulizi.
Mwamuzi wa mchezo huu Ramadhani Kayoko alikuwa na mchezo mzuri kuanzia mwanzo mpaka mwisho na wasaidizi wake na hilo linahitaji pongezi kwao japokua kuna makosa madogo yaliyojitokeza ambayo yangeweza kuwapa nafasi ya ushindi klabu ya Simba SC, tukio la mshambuliaji Pa Omar Jobe kuchezewa faulo na Lusajo Mwaikenda ni zahiri kuwa ilipaswa kuwa penalti kwa mujibu wa picha marejeo zjnaonyesha Lusajo alicheza mguu badala ya mpira tukio ilo ni sawa na lililotokea kwenye mchezo wa AFCON kwa goli la kusawazisha la Afrika Kusini.
Timu zote zilifanya mabadiliko ambapo Simba SC walifanya mabadiliko 4 na Azam FC wakifanya 5. Hata hivyo mabadiliko hayo yalikuwa na faida zaidi kwa Simba SC kuliko Azam FC. Kuingia kwa Kennedy Juma kulisaidia zaidi kuziba “Counter Attack” za Azam FC kwa kiasi kikubwa huku Pa Omar Jobe nayo ikiwafanya mabeki wa Azam FC kutokuwa huru tofauti na kipindi cha kwanza. Huku mabadiliko ya Kapombe yakisaidia zaidi eneo la kiungo na kupandisha mashambulizi.
Upande wa Azam FC mabadiliko yao kwa kiasi kikubwa yalikuja kuwafanya kuwa chini tofauti na kipindi cha kwanza walikuwa kwenye nusu yao kwa muda mrefu na ilipelekea mashambulizi mengi upande wao.
Mabadiliko ya kumtoa Pascal Msindo yalipunguza presha ya mashambulizi ya kushtukiza kwenye lango la Simba SC pamoja na Kiungo Yahya Zayd kutoka kwake kulikuwa na hadhari kubwa zaidi kwa upande wao kwani pasi za “Counter attack” zilikosekana ukilinganisha na muda ambao alikuwa kiwanjani.
SOMA ZAIDI: Azam Sio Timu Ya Kugombea Ubingwa Tanzania