Safari ya soka ya Afrika Kusini imejaa mafanikio makubwa na changamoto kubwa kwenye michuano ya soka barani Afrika. Kilele cha mafanikio yao kilifikia mwaka 1996 walipokuwa wenyeji na washindi wa AFCON ambapo waliweka jina lao miongoni mwa mataifa ambayo yametwaa ubingwa wa kombe la mataifa barani Afrika.
Tangu mwaka 1996 baada ya kung’ara kwa kiwango juu na kuchukua ubingwa wa AFCON hawakuhaki kutwaa tena kombe hili na wamekua hawana kiwango bora cha kuridhisha katika michuano ya mataifa barani Afrika licha ya wao kuamini kuwa msimu wa mwaka huu nchini Ivory Coast ndio njia ya wao kuonesha kile walichonacho na kurudisha upya sura ya soka la Afrika Kusini katika cha bara la Afrika.
Historia inayokumbukwa zaidi kutoka katika soka la Afrika Kusini ni mtindo wao wa kucheza ambao ulifahamika kama Kasi Flavour ambao uliwapa ubingwa lakini safari hii wanaingia katika michuano hii kama washindani wa dhati kabisa na hii inachangiwa na uwepo wa wahezaji wakubwa ndani ya kikosi cha Bafana Bafana ambao wengi wanatoka katika timu kubwa ya Mamelodi Sundowns.
Timu ya taifa ya Afrika Kusini pia imechukua medali za fedha na shaba katika mashindano haya, lakini hawajafika nusu fainali tangu mwaka 2002 lakini pia wamefuzu mwaka huu baada ya kushindwa kufuzu katika michuano ya mataifa barani Afrika msimu uliopita.
Je, Afrika Kusini Inaweza Kusimama Imara?
Bila shaka hili ni swali litakalokua linaulizwa na mashabiki wengi wa soka barani Afrika kwani kila mmoja anatamani kuiona Afrika Kusini ile hatari zaidi. Mwaka 1996 ikiwa kama nchi mwenyeji licha ya kutozungumzwa zaidi lakini walichukua ubingwa katika ushindi wa kihistoria licha ya kutopewa nafasi kubwa ya kuwa mabingwa. Mashindano hayo daima yatakumbukwa kwa picha za kipekee za umoja wakati Nahodha Neil Tovey alipoinua kombe pamoja na Nelson Mandela, wakiashiria ladha ya kwanza ya utukufu wa bara lao.
Katika nyakati za hivi karibuni kwenye kampeni ya AFCON ya mwaka 2019 iliyofanyika nchini Misri, ilishuhudia Afrika Kusini wakiwa hawana kiwango bora lakini safari yao ikiishia hatua ya robo fainali, wakipoteza kwa Nigeria katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa.
Wakati huu, Bafana Bafana wanaonekana wameunda mojawapo ya timu bora ambazo wameweza kuunda katika miaka mingi, wakiwa chini ya uongozi wa Percy Tau kutoka Al Ahly. Hata hivyo, upande huo hautaweza kutegemea huduma za mshambuliaji wa Burnley, Lyle Foster, ambaye alikuwa mfungaji bora wakati wa kufuzu.
Kutokana na Zimbabwe kuondolewa kwenye mashindano, Bafana Bafana walikuwa sehemu ya kundi la timu tatu katika kufuzu pamoja na Morocco na Liberia. Afrika Kusini walimaliza wa pili kwenye kundi hilo wakiwa na pointi saba katika mechi zao nne, wakipoteza mara moja tu dhidi ya Morocco ugenini, ingawa walifanikiwa kuwashinda The Atlas Lions katika mchezo wa kurudi huko FNB Stadium jijini Johannesburg.
Tangu wakati huo, Afrika Kusini wamefuzu kwa nafasi ya tatu katika Kombe la COSAFA na wamepoteza mara moja tu kati ya mechi zao sita zilizopita, huku wakipata droo tatu na kushinda mbili kati ya tano iliyosalia. Pia wako nafasi ya pili katika kundi lao la kufuzu Kombe la Dunia la CAF, wakiwa nyuma ya Rwanda kwa pointi moja tu baada ya mechi mbili za kwanza.
AFCON 2024 – Ratiba ya Afrika Kusini
Afrika Kusini wamepangwa katika kundi ambalo wengi wanachukulia kuwa ni lenye faida katika mashindano. Kundi E lina Mali, Namibia, na Tunisia, na timu zitakazomaliza nafasi ya kwanza na ya pili zitapata moja kwa moja tiketi ya kuingia hatua ya mchujo ya mashindano. Aidha, timu nne kati ya sita zitakazomaliza nafasi ya tatu katika kundi zao pia zitakuwa na uwezo wa kufuzu kwa hatua inayofuata kulingana na utendaji wao yaani Best Loosers.
Hebu tuangalie haraka ratiba ya Bafana Bafana katika hatua ya makundi:
– Jumanne, Januari 16 – Mali vs Afrika Kusini – Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly
– Jumapili, Januari 21 – Afrika Kusini vs Namibia – Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly
– Jumatano, Januari 24 – Afrika Kusini vs Tunisia – Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly
Afrika Kusini wanaingia katika michuano ya mataifa barani Afrika Msimu huu wakiwa nafasi ya 66 ulimwenguni kulingana na viwango vya FIFA vilivyopita. Ingawa hii inaweza isisikike kama kitu cha kuvutia mwanzoni, ni muhimu kuzingatia kuwa Bafana Bafana wamepanda hadi nafasi ya 12 kati ya mataifa 53 ya soka barani Afrika.
Yapo mengi ambayo unaweza kusoma zaidi kuhusu AFCON kwa kugusa hapa.