Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Adel Amrouche hii leo ametangaza kikosi cha wachezaji 30 watakaojiunga na kambi ya maandalizi ya AFCON nchini Ivory Coast ambapo ameweka bayana maamuzi ya uchaguzi wa kikosi hicho.
Zimebaki siku chache sana kabla ya kuanza kwa fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) ambazo zitafanyika huko Ivory Coast, kuanzia Januari 13 hadi Februari 11 na tayari timu zote 24 zitakazoshiriki mashindano hayo zimeshatoa vikosi vyake vya awali na baadhi zimeshaamua kuweka hadharani vikosi vyao vya mwisho ambavyo vitapeperusha bendera kwenye hayo mashindano.
Taifa Stars ambayo imepangwa Kundi F pamoja na Morocco, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imeondoka leo Dar es Salaam kwenda Cairo, Misri kuweka kambi ya wiki moja kabla ya kwenda Ivory Coast.
Kwa Taifa Stars hizo zitakuwa Fainali za tatu za AFCON kucheza baada ya mwaka 1980 nchini Nigeria na 2019 nchini Misri, kote wakitolewa hatua ya makundi.
Kwa Taifa Stars hizo zitakuwa Fainali za tatu za AFCON kucheza baada ya mwaka 1980 nchini Nigeria na 2019 nchini Misri, kote wakitolewa hatua ya makundi.
Endelea kusoma zaidi kuhusu michuano ya AFCON kwa kugusa hapa.
1 Comment
Pingback: Wachezaji wa Kutazamwa AFCON 2023 - Kijiweni