Unaweza kuwa staili mbili tofauti ukiwa na mpira unaanzaje , kutokana na mpinzani wako anafanya nini dhidi yako , Simba SC hawakujibana na staili moja pale walipoamua kuanza nyuma na mpira
Kuna wakati waliamua kuanza nyuma zaidi wakiwa na muundo wa 2-4 ( Inonga na Onyango nyuma ) huku mbele yao katika mstari mmoja Fullbacks wawili na viungo wawili wa kati ( Kapombe Kanoute Mzamiru na Zimbwe Jr ) . Walifanya pale ambapo Horoya waliamua kukabia chini
Lakini pale ambapo Horoya waliamua kukabia juu kwa kutumia washambuliaji wao wawili juu ( 4-4-2 ) Simba waliamua kupiga mipira mirefu na kuwania mipira ya pili inayoanguka hasa kwenye zone ya Horoya na kuanzia mashambulizi yao hapo
Nafikiri kipindi cha kwanza walichokosa Horoya ni ufanisi wa pasi ya mwisho na kulenga lango lakini wakiwa kwenye 4-3-3 yenye namba 8 wawili , walikuwa wanafikiwa pasi za mbele , tena nyuma ya kiungo cha Simba walichokosa ni ubora kama wa Simba , na kipindi cha pili walipoamua kufunguka kuufukuza mchezo wakakutana na dhoruba
Kipindi cha pili Simba SC wamecheza kwa mamlaka zaidi , kwa hesabu zaidi , kwamba haina haja ya kuharakisha vitu , hakuna haja ya kukimbizana sana , miliki mpira , tanua uwanja , na niliona mabadiliko ya nafasi uwanjani , Kibu Denis kuingia ndani sambamba na Baleke huku Chama na Saido wakiwa pembeni kama ” Wide playmakers” na wakaamua kuwasubiri Horoya FC kwenye counter attacks maana space zilifunguka sana kwa timu ya Horoya
Uwanjani ni kujua space ipo wapi na muda unaupata wapi : Chama Jr na Saido positions ambazo walikuwa wanasimama kabla ya kupokea mpira ilikuwa inawapa tabu fullbacks na kiungo wa ulinzi wa Horoya … hawakuwa pembeni sana bali katikati ya kiungo na fullbacks wao ( Half Spaces ) iliwaumiza sana Horoya