Denis Kitambi, aliyefanya mahojiano na Gift Macha, ameleta mwangaza wa kipekee kuhusu mechi iliyopita ya Simba dhidi ya Namungo.
Kitambi ameelezea jinsi Namungo walivyodhibiti mechi, akisema, “Kabla ya mechi, ungenipa alama moja naichukua, lakini kwa jinsi mechi ilivyokuwa na nafasi alizopata kwenye counter attacks, amehuzunika kutoshinda mechi.”
Hii inaonyesha jinsi Namungo walivyokuwa wanajiachia na jinsi walivyotumia fursa zilizojitokeza.
Simba, kwa upande mwingine, ilionekana kuwa dhaifu na kushindwa kufanya ushindani vizuri.
Namungo hawakulazimika kutumia nguvu nyingi, kwani Simba haikuwawekea presha.
Hata hivyo, kuna mambo kadhaa yaliyosababisha Simba kuruhusu bao
Kukosa umakini wakati wa mashambulizi muhimu.
Kutokuwa na imani ya kufunga zaidi ya goli moja.
Wachezaji wengine kukosa kujiamini na kuharakisha maamuzi.
Simba SC ilionyesha ishara za kuchanganyikiwa kisaikolojia, hali iliyosababisha mchezo kuonekana dhaifu.
Ni dhahiri kwamba mpira huwa unachezwa kichwani, na Simba ilionekana kukosa mwelekeo wa kisaikolojia.
Lugha ya mwili ya wachezaji wa Simba ilionyesha ukosefu wa uharaka, pasi zilipotea kirahisi, na hawakufiki kugombania mipira.
Hii inaweza kuwa ni matokeo ya hasira binafsi kutokana na matokeo mabaya ya mechi iliyopita.
Inaonekana kwamba Simba inahitaji kurejesha haraka hali yao ya kisaikolojia.
Mchambuzi wa Wasafi (George Anbagile) anatoa maelezo kuhusu baadhi ya wachezaji, akiwapongeza wengine kama Jean Baleke na Moses Phiri, na kutoa matumaini kwa mustakabali wa timu.
Kwasasa, Simba inahitaji kufanya marekebisho ya haraka mnoo na kujiandaa vizuri kwa mechi zijazo ili kurudisha heshima yao na kurejesha mwelekeo wa kisaikolojia na kimwili kua tayari kupambania nembo ya klabu yao
Soma zaidi: Habari zetu kama hizi hapa