Pamoja na umwamba wake wote timu Al Ahly mbele ya Simba SC haina rekodi ya kutisha ambayo inaweza kumfanya Mnyama Simba awe mnyonge. Takwimu zinazungumza lakini rekodi pia zipo wazi. Ndani ya mechi 6 Simba SC ameshinda 2 na Al Ahly pia ameshinda mechi 2 na michuano ya African Football League ambayo imazifanya timu hizi kwenda sare ya mechi mbili.
Michezo miwili inayofuata inaenda kuweka rekodi nyingine yakufikisha jumla ya michezo 8 kwahiyo hakuna kinachoweza kuwafanya wanalunyasi kuwa waoga mbele ya Al Ahly.
REKODI ZA MABAO
Sadio Kanoute – ⚽⚽
Karim Nedved – Al Ahly ⚽⚽
Kahraba – Al Ahly ⚽⚽
Reda Slim – Al Ahly ⚽
Kibu Denis – ⚽
Wakati hayo yanaendelea ni wazi kuwa mashabiki na wafuasi wa klabu ya Simba wameona mchezaji wao Aubin Kramo ambaye amerejea kwenye mazoezi na timu lakini swali kubwa likawa vipi kuhusu mchezo dhidi ya Al Ahly na ile ya Ligi Kuu?
Hakuna ambaye hafahamu kuhusu majeraha ambayo aliyapata na kumfanya kuwa nje ya soka kwa muda sasa lakini kwa sasa amepona lakini ni wazi kuwa katika msimu huu hajasajiliwa kwenye dirisha la mashindano maana baada ya kufika dirisha dogo la usajili klabu ya Simba iliona kuwa anahitaji kukaa nje kwa muda mrefu kwa hivyo Jina lake likaondolewa kwa wachezaji waliosajiliwa kwenye ligi ya ndani na hata Kimataifa ila akabaki kama muajiriwa wa Simba kwa hiyo akaendelea kupata stahiki zake kwa maana mishahara na mambo mengine.
SOMA ZAIDI: Takwimu Zinaibeba Yanga Mbele Ya Mamelodi Sundowns?
1 Comment
Pingback: Kuhusu IHEFU Na Umiliki Wa Siri ,TFF Mnaniwazisha Mno - Kijiweni