Hayawi hayawi mwisho yamekua baada ya timu mbili za Tanzania kufika Robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa pamoja, Leo tarehe 12 March 2024 imepangwa droo ya hatua ya robo fainali na mabingwa wa Tanzania Yanga wamepewa wababe toka pande za kusini mwa Afrika Mamelodi Sundown… Huku wekundu wa Msimbazi wakipewa Bingwa mtetezi Al ahly…. Je timu zetu hizi za Tanzania zina nafasi ya kusonga mbele kwenda Nusu fainali?
Kwa mtazamo wangu Game ya Simba na Al ahly Kwa Mkapa Simba ana matumaini ya kushinda au kutoa Sare maana amekua akimbana mbavu Sana Al ahly lakini kashehe itakua kule Cairo.
Wengi tumekua tukijidanganya kuwa Al Ahly wako unga na hawana kiwango bora msimu huu lakini wamesahau ndio bingwa mtetezi na ametoka kushiriki michuano mikubwa ya kombe la dunia la FIFA kwa ngazi ya klabu kwahiyo sio timu ya kawaida kama tunavyojidanganya.
Karata yangu naiweka Kati 50/50 na Simba atakua na nafasi ya kufuzu endapo atashinda Kwa mkapa walau Bao mbili bila.
Kwa upande wa game ya Yanga na Mamelodi bado nafasi ipo Mamelodi Sundowns kutokana na ubora wao moja kwa moja japo na yeye kwenye upande wa mabeki sio mzuri Sana na hapa Yanga pia anatakiwa apambane zaidi game ya nyumbani walau ashinde Kwa Bao mbili bila…. Inawezekana kabisa karata yangu pia naiweka 50/50.
RATIBA KAMILI:
Simba Sports Club vs Al Ahly
TP Mazembe Vs Petróleos de Luanda
Espérance Tunis Vs ASEC Mimosas
Young Africans Vs Mamelodi Sundowns
MECHI ZA SIMBA NA YANGA:
Wawakilishi wa Tanzania Simba na Yanga kila mmoja ataanzia nyumbani kutokana na kumaliza nafasi ya pili katika kundi lao na michezo ya mkondo wa kwanza itachezwa tarehe 29 na 30 March 2024 huku marudiano yakiwa ni April 5 na April 6, 2024.
SOMA ZAIDI: Droo Ya Robo Fainali Ligi Ya Mabingwa Afrika Itavyofanyika