Hii leo ni wazi kuwa klabu ya Yanga watakua wakiutazama kwa karibu kabisa mchezo wa CR Belouizdad vs Al Ahly ili kuona kama ndoto yao ya kufika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika inatimia kumbuka kuwa mchezo huu kwa asilimia kubwa umebeba ramani ya kundi ambalo yupo Yanga kwani inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Kundi D, sawa na vinara wa kundi hilo Al Ahly, lakini mabingwa hao watetezi wa Ligi ya Mabingwa wana mchezo mmoja mkononi dhidi ya Belouzidad ambayo ina pointi tatu utakaochezwa Algeria leo.
Ijumaa 16th Feb22:00
- CR Belouizdad vs Al Ahly
Ijumaa 23rd Feb19:00
- Medeama vs Al Ahly
- Al-Hilal Omdurman vs Petro de Luanda
- ASEC Mimosas vs Simba SC 22:00
Jumamosi 24th Feb16:00
- Jwaneng Galaxy vs Wydad Casablanca
- TP Mazembe vs Pyramids FC
Jumamosi 24th Feb19:00
- Nouadhibou vs Mamelodi Sundowns
- Young Africans vs CR Belouizdad
Jumamosi 24th Feb22:00
- Étoile du Sahel vs ES Tunis
Yanga watakutana na CR Belouizdad ya Algeria katika mchezo wa Raundi ya Tano wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam, Februari 24 huku klabu ya Simba wao watasafiri mpaka katika nchi ya mabingwa wa AFCON Ivory Coast ili kucheza mchezo wao dhidi ya ASEC Mimosas tarehe 23 ya mwzi huu.
SOMA ZAIDI: Takwimu Na Rekodi Zote AFCON Unazopaswa Kuzifahamu
2 Comments
Pingback: Simba Na Yanga Wapo Katika Kesi Kubwa Ya Dunia Sasa - Kijiweni
Pingback: Msimamo Wa Makundi Yote Ligi Ya Mabingwa Afrika - Kijiweni