Ilipoishia “Usijali Jacklin nipo kwa ajili yako mara zote” alisema Mosses na kunifanya nitabasamu kwa uchovu, shughuli ilikuwa pevu na vile nimetoka kuumwa basi nilichoka sana nikalala palepale.
Osman alipofika ofisini alihitaji kuniona ila aliambiwa kuwa nimetoka, akiwa kama Bosi wangu alihitaji kujuwa niko wapi, alinipigia sana simu lakini haikupokelewa maana nilikuwa nimelala chakali, basi alipiga kwa Mama na kumuuliza kama nitakuwa nimeenda nyumbani, Mama alimwambia Osman kuwa sipo nyumbani. Endelea
SEHEMU YA TANO
“Haya Mama nitaendelea kumtafuta” Alisema Osman, alipokata simu alijiuliza nilikuwa nimeenda wapi, alishikwa na wivu fulani hata kazi hakufanya naye aliondoka. Mida ya Jioni kama saa moja kasoro hivi ndiyo niliamka, nilikuta Mosses ameniandalia supu, nilikunywa kisha aliniuliza
“Osman ndiyo Nani? Amepiga sana simu, ilipokata yake iliingia ya Mama yako, walikuwa wakipiga kwa kupokezana” Aliniuliza na kuelezea kuhusu simu zilizokuwa zimeingia
“Osman ni Bosi wangu labda amenipigia sababu kuna faili zipo kwangu, ngoja nimpigie Mama” Nilisema, alinisogezea simu mara moja kisha nilimpigia Mama, alipokea na kinishushia swali juu
“Jacklin uko wapi?” Aliuliza kwa sauti iliyoonesha kuwa alikuwa na shahuku ya kujuwa nilipo
“Mama mimi siyo Mtoto sasa swali gani hilo alafu kama vile una hasira na Mimi!”
“Ndiyo wewe siyo Mtoto lakini kwanini uondoke kazini kabla ya muda wa kazi kuisha? Osman amenipigia simu kujuwa kama upo sawa na upo wapi”
“Ulimjibuje Mama”
“Nilimwambia kuwa sijui ulipo sasa kwanini niwe muongo kwa kijana wa Watu, mwisho wote tuje kuonekana hatuna maana?”
“Ok Mama usiongee sana nipo kwa Mosses hata hivyo narudi muda siyo mrefu” Nilisema, Mama alikata simu.
“Huyo Mama yako jinsi anavyonichukia usikute amekasirika huko kisa wewe kuja kwangu” Alisema Mosses
“Ah! Mama yangu nimeshamzoea love, ngoja nirudi tu nyumbani ila fanya kama tulivyoongea tafuta nyumba kesho unipe jibu” Nilisema kisha nilizama kwenye waleti yangu nikampa Mosses laki na nusu
“Hiyo itakusaidia” Nilisema kisha niliondoka zangu pale.
Nilipofika nyumbani nilimkuta Mama akiwa amefura kama chura mwenye njaa, alikuwa amekaa nje akinisubiria. Nilipomfikia aliniuliza swali gumu sana
“Umesahau kila kitu sababu leo upo hai, huyo Mosses alikataa kusaidia Maisha yako, alinijibu jeuri lakini wewe unamuona wa maana sana kwako, nimefanya makosa kukupigania Jacklin?”
Lilikuwa ni swali gumu kuwahi kuulizwa katika Maisha yangu, Mama alidondosha chozi lililochuruzika hadi kwenye mashavu yake, ilinibidi nikae kwanza
“Mama ndiyo maneno gani hayo? Binadamu tunakosea na kujirekebisha, usimuhukumu Mosses kwa kosa moja tu yule ni Binadamu hajakamilika Mama, hilo haliwezi kuuondoa uthamani wake kwangu” Nilimjibu Mama kwa kujikaza sana, hakuna kitu nilikuwa sipendi kama kumuona Mama akilia kwa ajili yangu, anagalau ningekuwa mgonjwa lakini ni mzima na analia kwa ajili yangu
“Mama yako nilisemewa vibaya, Kijana wa Watu alikusaidia hakuangalia nyuma. Bila Osman ingekuwa inasimuliwa hadithi yako Jacklin, lakini leo Mtu aliyekusaidia akabadilisha na Maisha yetu kututoa kwenye umasikini hadi kwenye hali hii haupokei simu zake, unaacha kazi yake na kwenda kwa Mosses?” Alisema Mama, nilihema kwa uchungu na maumivu, ni kweli Osman alisaidia Maisha yangu lakini hakusaidia ili niwe mtumwa kwake
“Mama msaada ambao unakuwa Mtumwa ni msaada wa kizandiki tuu, kama alinisaidia kwa moyo wake hakupaswa kuhitaji malipo, mbona anajuwa kila kitu sasa kwanini apige simu kwako? Amenikosea sana”
“Unajisikiliza Jacklin au unaongea kwasababu unayo nafasi ya kufanya hivyo? Hajakusaidia tu bali ameweka maisha yake rehani, anatembea na figo moja kwa ajili yako, hupaswi kumsumbua hivi kijana wa Watu na kama huitaji kazi basi mwambie ili amtafute Mtu mwingine” Mama alisema kwa hisia kali
“Sawa Mama sipendi ukwazike kwa ajili yangu. Nitamuomba msamaha Osman, kuwa na amani Mama nakupenda sana” Nilisema kisha nilinyanyuka na kuingia ndani, nilimuacha Mama akiwa amekaa nje peke yake, najuwa jinsi alivyokuwa anajisikia ila ningefanya nini wakati moyo wangu upo kwa mwingine? Niliziona ishara zote kuwa Osman ananipenda ila tayari hisia zangu zipo kwa Mosses.
Nilipofika chumbani kwangu niliyatafakari maneno ya Mama ambayo ni wazi aliyasema kutoka ndani ya nafsi yake, nilijisikia vibaya, nilitamani kumtumia meseji Osman nimuombe msamaha ila niliona ni bora nimuombe msamaha kesho yake Ofisini, nilizitazama Missed Calls zake nilimuonea huruma Kijana wa Watu, nilifunua shati langu nikaangalia eneo la tumbo, nilitabasamu tu hata sijui kwanini nilifanya hivyo.
Kesho yake kabla ya kwenda ofisini nilipitia duka la Maua nikanunua ua zuri kwa ajili ya kumpatia Osman ili anisamehe kwa kilichotokea. Nilichagua ua zuri ambalo niliamini litampa furaha Osman, mvua zilikuwa zinaendelea kunyesha, hali ya hewa ilikuwa nzuri sana ikanikumbusha siku ya kwanza Nilipoanza kuumwa nikasaidiwa na Osman, nilianza kutabasamu tu hadi Muuza Maua alinishtukia akasema
“Inaelekea unampenda sana Mtu ambaye unampelekea ua hili, Nawaombea penzi lenu lichipue mithiri ya Mtende jangwani” Alisema kisha alinitazama usoni, ghafla sura yangu ilikosa uchangamfu. Sijui kwanini kila nilipomfikiria Osman nilijikuta nikiishia kwenye huzuni. Mara muda huo huo Osman alipiga simu kama vile alikuwa akijuwa nilikuwa nikimuwaza, niliiacha iite kidogo kisha niliipokea huku yule Muuza duka akinitazama tu
“Hello Osman” Nilimsalimia Osman mara baada ya kuwa nimeshapokea simu na kusikia sauti yake
“Jacklin, leo sijisikii vizuri naomba usimamie kazi zako vizuri” Alisema Osman, ni kweli hata sauti yake haikuwa na uchangamfu
“Una shida gani Osman?” Nilimuuliza
“Nahisi hali ya Homa tuu Jacklin” Alisema tena Osman
“Haya nitafanya hivyo lakini baadaye….” Nilitaka kumwambia kuwa nahitaji kuonana naye ila nilisita nikamwambia
“Ugua pole Osman” Nilisema kisha simu ilikatika, nilirudi kulipia ua lile kisha niliondoka nalo hadi kazini.
Mdada wa mapokezi aliponiona alinisimamisha, alinifuata niliposimama akaniuliza
“Umempa nini Bosi Osman? Yaani alivyo mkali yule lakini jana alinywea kabisa, aliposikia haupo naye aliondoka na alionekana hana raha” Alisema, dakika moja tu ilitosha kumtambua alikuwa ni Mtu wa aina gani, alionekana kuwa mshakunaku, nilitabasamu kisha nikamwambia
“Kazi njema” nilimuacha akiwa ameduwaa, pengine alitegemea ningemwambua Mimi ni Mwanamke wa Osman nahisi ndicho alichokuwa anataka kukisikia.
Niliketi kwenye kiti, nilishusha pumzi zangu, niliona jinsi maisha yangu yalivyobadilika. Mara simu yangu iliita, aliyekuwa akinipigia alikuwa ni Mosses, aliniambia kuwa amepata nyumba hivyo ilikuwa ikihitaji pesa kiasi cha Milioni 14, nilimwambia jioni nitampatia pesa hiyo.
Siku hiyo, Osman alienda Hospitalini kuangalia afya yake, alienda kwenye Hospitali ya Dokta Simon, Wawili hawa walikuwa wakifahamiana sana. Alipofika Dokta Simon alimfanyia uchunguzi, kwakuwa alikuwa akimfahamu vizuri Osman alijuwa ni kitu gani kilikuwa kikimsumbua Osman, waliketi baada ya vipimo
“Osman! Nilikuonya kuhusu kutoa figo yako hukutaka kunisikia” Alisema Dokta Simon, Osman alikaa kimya kumsikiliza Dokta Simon
“Nilikataa usifanye vile sababu ya tatizo lako, figo moja ilikuwa na matatizo hivyo ulikuwa ukitumia zaidi figo moja tuu, sasa ile nzima umeiondoa hii iliyobakia inafanya kazi kwa kiwango kidogo sana na haitokuwa na muda mrefu nayo itakufa” Alisema Dokta Simon
“Kwanini umeamua kuhatarisha Maisha yako Osman? Wewe ni Bilionea mkubwa hapa Nchini, una pesa ya kutosha, unaheshimika kila kona” Aliendelea kusema Dokta Simon
“Nilifanya vile kwasababu ya upendo wangu kwa Jacklin, nilikuwa na Maisha yaliyojaa huzuni sana baada ya Zahra kunitenda vibaya, ghafla sura yangu ilijawa tabasamu mara baada ya kumuona Jacklin, niliapa sitopenda tena ila baada ya Jacklin kuja katika Maisha yangu nimejihisi tofauti kabisa” Alisema Osman kisha alishusha pumzi zake
“Kwa mara ya kwanza namuona Bilionea dhahifu zaidi katika Maisha yangu, unahatarisha Maisha yako kwa ajili ya Mwanamke ambaye unajuwa fika ana Mwanaume wake? Unahatarisha Maisha kwa ajili ya Mwanamke ambaye hata hujawahi kumtamkia chochote? Hiyo ni akili yako Osman?? Laiti kama Mzee Dhabi akilijuwa hili ulilofanya ataipoteza familia ya Jacklin na haitokuja ionekane tena, wewe ni Mtoto wa pekee wa yule Mzee, siku akiligundua hili anaweza hata akaniuwa Mimi” Alisema Dokta Simon
“Sikia Dokta Simon, naomba hili jambo liwe siri Baina yetu. Baba yangu asijuwe chochote wakati ambao tunatafuta Figo kwa ajili ya kunipandikiza” Alisema Osman
“Naweza kulificha lakini hali yako inaweza ikaniumbua mbele ya Baba yako, vyote nitafanya lakini vipi kama Jacklin akazikataa hisia zako huoni kama utakuwa umekula hasara wewe?” Alimuuliza swali gumu sana, Osman alikunbuka namna tukivyogombana kule Dubai, aliona Swali la Dokta Simon lilikuwa na mashiko sana.
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya SITA Ya PUMZI YA MWISHO
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx
8 Comments
Asante mtunzi, endelea kutupa burudani
Huyu demu ovyoo sana🙌🙌
Mungu naomb jackline atambue kuw mosses hampend arudi kwa osman
Ivi ni kweli kina mwanamke wa ivi
Noma nomaa…..dis iz goin to be bad🥲🥲 osman his going to lose his life🥺🥺
Asitisha mapenzi Kwa Jacklin bn me nakadirishwa na uyu dada duuh
Jacklin hakir hana
endelezen bas