Ilipoishia “Unaweza ukapata figo, ukapata kila kitu lakini huwezi kuuondoa mfadhahiko alionao Mwanao. Kitu cha kwanza ni kumuondolea mfadhahiko Osman ili kumuandaa kwa ajili ya upasuaji wa kupandikiza figo” Alisema Dokta Simon
“Pesa siyo tatizo Simon, niambie hiyo huduma inapatikana Hospitali gani Duniani, kiasi gani kinahitajika?” Aliuliza Bilionea Dhabi, walionesha kumpenda sana Mtoto wao.
“Mfadhahiko huondolewa na kilichosababisha mfadhahiko, tumaini alilokuwa nalo ndilo lenye kuuondoa huo mfadhahiko wa Osman”
“Unamaanisha nini?” Endelea
SEHEMU YA NANE
“Tumaini la Osman lilikuwa kwa Jacklin, aliweka moyo na akili yake kwenye tukio la kumvisha pete, ili apone ni lazima atimize lengo hilo, akili yake haifanyi kazi sawa sawa, analitaja jina la Jacklin tu” Alisema
“Oooh Mungu wangu, sasa Binti hamuhitaji Osman, amemkataa mbele za Watu unafikiria ni rahisi kukubali?” Aliuliza Mama yake na Osman
“Hakuna jambo zuri linaloweza kuja kirahisi Mzee Dhabi, wewe ni shahidi hata kwenye ubilionea wako haukuja kirahisi, ulihangaika, mtafuteni Jacklin, kama Osman aliweza kuokoa Maisha ya Jacklin kwa kumtolea figo basi Jacklin aokoe Maisha ya Osman kwa kukubali kufunga ndoa na Osman” Alisema Dokta Simon kisha aliongeza
“Kisaikolojia Osman anahitaji kuona alichokiwaza kinakuwa kweli, tunaweza kumsaidia kupandikiza figo lakini tukampoteza kwa mfadhahiko, ni lazima tuuwe ndege wawili kwa jiwe moja”
“Kwenye hili jambo sidhani hata kama pesa niliyonayo inaweza nisaidia, nitajaribu kufanya hivyo Dokta lakini kwa upande wako hakikisha unafanya kila liwezekanalo zipatikane figo mbili au moja kwanza” Alisema Bilionea Dhabi kisha waliondoka Hospitalini sababu hawakuruhusiwa kumuona Osman kwa wakati huo hadi kesho yake asubuhi.
Usiku huo ulikuwa ni Usiku wenye Hekaheka sana, Bilionea Dhabi alimpeleka Mke wake Nyumbani kwa Osman kisha alitoka na Mlinzi wake akaenda nyumbani kwetu, alihitaji kuniona Mimi.
Alimkuta Mama akiwa bado yupo macho, ilikuwa ni mishale ya saa 7 Usiku, Mama alipomuona Bilionea Dhabi alijuwa tu alikuja kwa ajili yangu Mimi. Waliketi na kuanza kuzungumza, swali la kwanza alilouliza Bilionea Dhabi lilikuwa
“Jacklin yupo hapa nyumbani?” Aliuliza kwa sauti iliyopoa sana, Mama alitikisa kichwa kuashiria kuwa sipo nyumbani
“Tangu alipoondoka ule muda hajarudi tena” Alijibu Mama kwa sauti iliyopoa iliyojaa maumivu ndani yake
“Ulijaribu kumpigia simu?” Aliuliza Bilionea Dhabi
“Amezima simu yake” Alijibu Mama, Bilionea Dhabi alishusha pumzi zake
“Ulikuwa unamuhitaji? Vipi hali ya Osman?”
“Hali ya Osman ipo katika hatari sana, Alikuwa na tatizo la figo moja, figo hilo hilo lililokuwa zima alilitoa kwa ajili ya kunusuru Maisha ya Binti yako Jacklin, hivyo anakabiriwa na tatizo la figo na mfadhahiko ambao ameupata baada ya kilichotokea, anahitajika Binti yako kwa ajili ya kuokoa uhai wa Osman” Alisema Bilionea Dhabi
“Jacklin anatakiwa kulitoa hilo figo ampe Osman?” Aliuliza Mama huku akiwa mwenye wasiwasi sana
“Hapana, anatakiwa kuondoa mfadhahiko wa Osman vinginevyo tunaweza kumpoteza. Jacklin anatakiwa kukubali kuolewa na Osman ili Osman aamke tena” Alisema Bilionea Dhabi
Mama alikuwa kinywa wazi kwa alichokisikia, alishusha pumzi zake alizozivuta kwa mkupuo.
“Kwanini Maisha yananipa machaguo magumu hivi? Jacklin uko wapi Mwanangu” alijiuliza Mama yangu.
Muda huo nilikuwa nimekumbatiwa na Mosses ambaye alikuwa ndiyo Mwanaume niliyempenda sana. Akili yangu ilikuwa ikimuwaza sana Mama yangu sababu ndiye Mzazi pekee aliyenizaa na kunilea kwa shida sana, kwa ajinsi anavyonipenda kwa vyovyote atakuwa analia Usiku kucha, nilimuamsha Mosses nikamwambia
“Nahisi Mama ananiita Mosses” Nilisema nikiwa nimekaa kitandani
“Unahisi anakuita kwani wewe ni jini au, unaweza kuhisi jambo ambalo huna uhakika nalo, jinsi ulivyoondoka pale unafikiria Watu wanakuchukuliaje? Bado wana hasira na wewe Jacklin hebu tulale” Alisema Mosses, basi nilijilaza kitandani.
Sikujuwa kilichokuwa kinaendelea huko nje, sikujuwa kuhusu hali ya Osman na jinsi ambavyo Mimi nilikuwa nikitafutwa na Familia ya Bilionea Dhabi, Asubuhi Mapema nilimuuliza Mosses alikuwa anataka kuniambia nini kutakapo pambazuka, alikuwa na usingizi hivyo nilimuacha alale hadi atakapo amka, Mama na Bilionea Dhabi walinitafuta kila kona bila mafanikio yoyote, hakuna aliyekuwa anapajuwa mahali ambapo Mimi na Mosses tulikuwa tumepanga nyumba
Mosses alipoamka tuliketi ili tuongee, Mosses alinipa wazo la kuacha kazi kwa Osman kwasababu pesa ilikuwepo kisha aliniambia kuwa tuishi pamoja kama Mke na Mume tena ikiwezekana tufunge ndoa haraka sana ili kumkata tumaini Osman, wazo lake lilikuwa zuri ila nilimuwaza sana Mama yangu, alikuwa akinipenda sana na kwa vyovyote alikuwa akilia tu, nilishusha pumzi nikamjibu Mosses
“Najuwa unanipenda nami nakupenda sana Mosses, kufunga ndoa na kuishi na wewe ni jambo zuri na ndiyo ndoto yangu ila nikimfikiria Mama yangu huko alipo naishiwa nguvu. Naomba niwashe simu kwanza” Nilisema, Mosses alinisogezea simu yangu, niliiwasha, ilikuwa ni majira ya saa mbili asubuhi njua angalau siku hiyo lilikuwa limechomoza maana kilikuwa kipindi cha masika, jua lilikuwa likionekana kwa nadra sana
Sekunde chache za kuwasha simu ziliingia meseji nyingi sana, papo hapo Mama alinipigia simu. Mosses alikuwa amekasirika, nilipomtazama aliondoka pale chumbani. Niliisikilizia simu ya Mama kwa sekunde kadhaa kisha niliipokea, niliisikia sauti ya Mama akiwa analia akiniuliza nipo wapi tena alikuwa akiniuliza kwa kilugha chetu, ilitosha kutambuwa kuwa Mama yangu alikuwa katika hali ya huzuni sana
“Mama nipo” Nilisema
“Upo wapi Jacklin, kwanini unanitesa Mama yako?” Aliuliza Mama akiwa analia, taratibu chozi lilikuwa likinidondoka kwenye macho yangu.
“Mama usilie sasa Mimi nipo salama tu wala Usijali” Nilisema huku nami nikiwa ninalia, jinsi ambavyo niliishi Maisha na Mama yangu ilikuwa ni rahisi sana kuhisi maumivu yake ndani ya Moyo wangu, niliumia sana kujuwa Mama alikuwa akilia
“Sasa Jacklin huwezi hata kunionea huruma Mimi Mama yako? Nimehangaika tokea jana usiku, simu yako ilikuwa haipatikani, nimekutafuta kila kona bila Mafanikio yoyote, sijala tokea jana…” nilimkatisha Mama ili asizidi kuongea Maneno ambayo yangeongeza maumivu katika Moyo wangu, Jamani Mama alikuwa akilia kwa kwikwi
“Nakuja Mama” nilisema kisha nilikata simu, nilijiinamia huku moyo ukizidi kuniuma, Mama yangu alikuwa ndiye Mzazi pekee niliyebakiwa naye, alinilea katika mazingira magumu sana ambayo yalinifanya nimpende sana Mama yangu. Nilinyanyuka nikatafuta kibanio cha nywele kilipo, Mara alikuja Mosses akiwa katika hali ya hasira
“Unaondoka si ndiyo?” Aliniuliza
“Ndiyo Mpenzi kwa ajili ya Mama ila nitarudi” Nilimjibu nikiwa mbele ya kioo nikiwa nabana nywele zangu.
“Unaenda kuolewa na huyo Mjinga eee?” Aliuliza Mosses, ilinibidi niache kubana nywele maana nilijuwa ana hasira zaidi
“Hapana Mosses! Mama yangu alikuwa akiongea kwa kilio, nimeumia sana, naenda kuweka mambo sawa ili tufunge ndoa” Nilisema
“Sawa nenda lakini kumbuka nina video zako Jacklin, chochote utakachoamua kufanya nami nitafanya kwa upande wangu” Alisema Mosses, nilijuwa ni video gani alikuwa akizizungumzia, ni zile ambazo alinirekodi tukiwa tunafanya Mapenzi
“Nakuahidi Mosses siwezi fanya ujinga, siyo kwasababu ya video bali ni kwasababu Nakupenda sana” Nilisema kisha nilimbusu shavuni nikaondoka zangu.
Hali ya Osman ilizidi kuwa mbaya alikuwa akiendelea kutaja jina langu kila wakati, alikuwa akichomwa sindano za usingizi ndipo anaacha kunitaja. Bilionea Dhabi aliitwa Hospitalini
Dokta Simon alimueleza Bilionea Dhabi kuwa kuna hatari ya kumpoteza Osman kutokana na hali yake sababu kadili anavyozidi kunitaja Mimi ndivyo mfadhahiko unavyoongezeka kwake
“Sasa tufanye nini Dokta, tumehangaika Kumtafuta Jacklin tokea jana usiku hadi sasa hakuna dalili ya kupatikana kwake” Alielezea Mzee Dhabi
“Cha msingi mjitahidi apatikane huyo msichana, muongee naye ikiwezekana haraka iwezekanavyo aletwe” Alisema Dokta Simon, Ubilionea wa Mzee Dhabi haukuwa na kazi ili kuokoa Maisha ya Mtoto wake Osman, Mimi niligeuka kuwa Lulu, mara simu ya Bilionea Dhabi iliita, aliyempigia alikuwa ni Mama yangu, alimpa taarifa kuwa nimerudi nyumbani.
“Dokta nimeelezwa kuwa Jacklin amerudi nyumbani kwao, sasa cha Msingi ngoja niwahi huko kusudi nipate kumueleza hili jambo, nina imani atatusaidia” Alisema Mzee Dhabi, mara moja aliondoka Hospitalini akaja nyumbani
Muda huo nilikuwa nimekaa na Mama akiwa ananiuliza kuhusu kilichotokea
“Mama mimi sikuwa na kosa lolote lile, kama wewe ulijuwa uwepo wa tukio lile kwanini usinishirikishe na Mimi? Mlijuwa fika siwezi kukubali ndiyo maana mlifanya kuwa siri” Nilisema
“Sawa Jacklin hilo limeshatokea lakini hali ya Osman tokea jana hadi hivi sasa nilipozungumza na Baba yake bado ni mbaya mno, ipo hatari akapoteza Maisha yake” Mama alinieleza kwa mara ya kwanza kuhusu hali ya Osman
“Osman anaumwa? ” nilimuuliza Mama
“Ndiyo baada ya tukio la jana alipelekwa Hospitalini na kugundulika kuwa amepata mfadhahiko, ila kibaya zaidi ni kuwa alikuwa na matatizo ya figo moja, alilolitoa kwa ajili yako ndilo lilikuwa zima hivyo anapaswa kufanyiwa upasuaji ila Daktari ameshauri utoe msaada katika hali ya Osman” Alisema Mama, ilinibidi nikae vizuri ili nipate kumuelewa
“Unamaanisha nini kusema Msaada!” Nilimuuliza Mama
“Mfadhahiko wa Osman unapaswa kuondolewa, muondoaji wa mfadhahiko wa Osman ni wewe hapo Jacklin”
“Mimi nitaweza kuondoa vipi Mama” Nilimuuliza Mama, alisogea kisha alinishika mikono yangu.
“Kukubali kuolewa na Osman” Alisema Mama
“Nini?” Niliuliza
“Ndiyo! Unapaswa kukubali kuolewa na Osman ili apone na afanyiwe upasuaji wa kupandikiza figo” Mama alirudia kauli yake, akili yangu ilihama na kumuwaza Mosses, maneno aliyoyasema wakati naondoka kwake, achilia mapenzi yangu kwake
“Mama naweza vipi kuolewa na Osman, siyo chaguo langu lile, wala siyo aina ya Mwanaume ninayemtaka katika Maisha yangu, Mama nina Mtu wangu….Siwezi” Nilisema huku nikiwa ninalia, chozi lilikuwa likinivuja.
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya TISA Ya PUMZI YA MWISHO
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx
14 Comments
Asimin kunasiku uliluka tuma viwili leo
Jana kashabikia ubaya ubwela
https://whatsapp.com/channel/0029VarTsGt1t90TiJVyWi0J
Pumzi ya mwisho iko sawa mtunz yuko sawa
Admin tunaruhusiwa kumtukana huyu Binti mpuudhi?🤣🤣
Binti kama bintina
Kusoma tu story kumchangia admin aaaanh..
Kaz nzuri💪💪💪
Usimwamini mwanamke utakuja nishukuru baadae
Admin fanya kipande kingine jion mana ulituacha kinyonge siku mojaa
Admin weka part nyngn leo make juz ulituach….af ziwe ndef ndef kdg
Mambo ni moto🔥🔥🔥…!admin rusha kingine maaana siku hukurusha simulizi jaman huyu dada mbona ni muuaji aiseee karne ya sasa itokeee mie naopoa nitaenda kumpenda mbele kwa mbele hivi wapo kama kina osman sikuhizi kweli maaaana naona hawapoooo kabisaaaa
Nipo hapa osman ni wewe tu jacklin
Nimecheka kwanguvu
Hili lidada bonge la kiazi