Ilipoishia “Mama umemyoosha sana”Β
“Ndiyo dawa yake, mwache tu. Hawezi kufanya chochote kileΒ sababu anajua una ujauzito wake, atakapo kuja kufungukaΒ kiakili utakua umemaliza kila kitu, cha Msingi huyo MsichanaΒ Mshikilie hadi mwisho.”Β
“Asante Mama kwa ushauri wako unanisaidia mno”Β
“Nisipokusaidia wewe nimsaidie Nani tena”Β
“Nahitaji kujisaidia” Matilda alipaza sauti yake, mara kiatuΒ kikasikika kikija chumba alichokua amefungiwa, kikafunguliwa,Β akaingia Mwanaume mmoja.. EndeleaΒ
SEHEMU YA TISA
“Nimebwana, naomba kujisaidia” Akasema Matilda huku akianzaΒ kujikojolea, Mlinzi akamwambia MatildaΒ
“Nenda haraka” Akasema na kumsindikiza hadi chooni, chooΒ hicho kilikua cha ndani.Β
Alipoingia huko alikua tayari ameshasoma ni namna ganiΒ anaweza akaondoka hapo, akapanda juu ya sinki kisha akapitaΒ katika kitundu kidogo ambacho kilikua juu kilichotumika kamaΒ Dirisha la Choo, akadondokea chini, yule Mlinzi akaendeleaΒ kusubiria hapo huku mwenzake akiwa anamwita. Matilda akapataΒ maumivu kadhaa, jua lilikua linaanza kuzama, akatazama mbeleΒ yake akaona ukuta ambao haukua mrefu sana, akafikiria kutumiaΒ ukuta ili atimke hapo, akaparamia ukuta.Β
Mlinzi akaona dakika zinasogea akagonga mlango, akajibiwa naΒ ukimya huku akianza kupata mashaka juu ya uwepo wa Matilda,Β ikabidi afungue mlango, hakumkuta Matilda, akatazama paleΒ kwenye kitundu akaona dalili za Mtu kupitia hapo, akapandaΒ kwenye sinki akamwona Matilda akiwa anamalizia kuteremkaΒ ukuta, akagongana naye macho. Matilda akajiachia, Yule MlinziΒ akatoka chooni akampa taarifa yule Mlinzi mwingine kishaΒ wakaelekea nje kwa ajili ya kuhakikisha wanamkamata MatildaΒ jioni hiyo.Β
Matilda akajikuta yupo Msituni, akaanza kukata nyikaΒ kuwakimbia walinzi hao ili asalimishe maisha yake, WalinziΒ wakiwa na mbwa wakawa wanamfukuzia Matilda ambaye alionekanaΒ kua na spidi kubwa sana, alikua kilomita kadhaa kutoka walipoΒ walinzi. Akaendelea kukata nyika huku giza likiwa linaingia,Β akawa amechoka sana, alikua hajui ni mahali gani alipo, hivyoΒ alikua akikimbia kama mwendawazimu tu.
“Mama nilitereza naomba unisamehe kwa hili, nilikosea kabisa,Β nipo tayari kulipa kwa hili, nakiri Mimi ni Mtoto mpumbavuΒ sana” Alisema James akiwa mbele ya Mama yake ambaye alikuaΒ amekunja uso wake, watu kadhaa walikua wameshafika hapo kwaΒ ajili ya Msiba wa Patra. Chozi na makamasi yalikua yakimtoka,Β Mama Naomi akamwonea huruma sana, akamtazama Mama JamesΒ lakini hakua na nguvu ya kusema chochoteΒ
“Mamaaaaa!” akaita James huku akizidi kudondosha chozi, MamaΒ yake alikua kimya sana akiwa anatazama pembeni, kwa hasiraΒ aliyokua nayo hakutaka kabisa kumtazama JamesΒ
“Mama James, rudisha moyo wako nyuma, huyu ni Mtoto,Β ameteleza” Akasema Mchungaji George ambaye alikua bega kwaΒ bega na familiaΒ
“Tunazungumzia Maisha ambayo hayawezi kurudi, yule Binti,Β hawezi kurudi kwa namna yoyote ile, na Mama yake piaΒ asirudi?” akauliza Mama yake James huku akiwa amekaza machoΒ yake kwa Mchungaji George, Mchungaji akameza funda la mate,Β swali aliloulizwa lilimfanya akae kimya.Β
Chozi na jasho vilikua vikivuja kwa pamoja, James alijitahidiΒ sana kumwomba Mama yake amsamehe lakini Mama JamesΒ akashikilia msimamo kua hawezi kumsamehe hadi MatildaΒ aonekane. James akaondoka hapo Usiku
Hekaheka ndani ya Msitu ilikua ikiendelea, Matilda aliendeleaΒ kuwakimbia wale walinzi wa Neema, alichoka akaamua kujibanzaΒ nyuma ya Jiwe kubwa, walinzi nao walikua wameshachoka hukuΒ wakihimizana kua kabla ya jua kuchomoza wahakikishe kuaΒ wamempata Matilda.Β
Matilda akalala hapo Msituni hadi siku iliyofuata, alipoamkaΒ akaendelea na safari ya kutafuta msaada wa kutoka hapoΒ Msituni, akakatiza vijito na majabari makubwa na madogo hukuΒ akiwa hajui ni wapi anaelekea.Β
Moyoni mwake akawa anasema na Mungu wake kua amlinde BintiΒ yake, Masikini hakujua kua Binti yake alikua ameshafariki,Β ghafla akasikia sauti za Mbwa akajua anapaswa kuongeza mwendoΒ wa kuendelea kuutafuta Msaada, akakimbia umbali mrefu akiwaΒ na njaa na kiu ya Maji akajikuta akianguka baada ya kuhisiΒ kizunguzungu.Β
“Eee Mungu nilinde” Akasema Matilda, akahisi giza kishaΒ akapoteza fahamu.Β
“Babu kinachofuata ni kitu gani?” Akauliza Neema, Babu naΒ Mama yake wakiwa mbele yakeΒ
“Mtoto akizikwa habari yake itakua imeisha pia, James anaendaΒ kua mali yako bila kipingamizi chochote kile, hili ndiyoΒ jambo kubwa” Akasema Babu yake Neema, wakafurahi sanaΒ
“Yaani Babu kama tutafanikisha hili nakuahidi kua nitakupaΒ zawadi ambayo hutonisahau” Akasema NeemaΒ
“Huna haja ya kuahidi sababu wewe ni Mjukuu wangu Neema,Β kikubwa upate unachohitaji, ukipata wewe Mama yako amepata,Β basi ndiyo furaha yangu hiyo”Β
“Pamoja na hayo Babu nitahakikisha nakujengea nyumba yaΒ kifahari, nitakua na pesa nyingi” Alisema Neema. Mama NeemaΒ alikua Mtu wa kutabasamu tu akimwangalia Mwanaye na Babu yakeΒ wakiwa wanazungumza, kicheko chao kilikua kilio upande waΒ Mama James ambaye kila alipofikiria jinsi mambo yalivyoendaΒ alijikuta akiangusha kilio cha Mtu mzima.Β
Moyoni alijua kua kuendelea kuzuia Mtoto kuzikwa ni sawa naΒ kumtesa Mtoto huyo lakini moyoni pia alikua akiumia MtotoΒ kuzikwa bila Mama yake kuwepo, aliona ni sawa na kuzuia hakiΒ ya Msingi ya Mama Patra, lakini hakuna aliyejua kilichokuaΒ kikiendelea, Matilda alikua akipigana vita Msituni.
“Nipo wapi?” Akauliza Matilda baada ya kujikuta akiwa kwenyeΒ nyumba moja ambayo ilikua imeezekwa makuti, hakuna aliyeΒ mbele yake bali kitanda na ukuta uliojengwa kwa udongo waΒ kugandika. Akakohoa kidogo, haraka akaingia Mzee Mmoja ambayeΒ alikua na ndevu ndefu, chafu zenye Mg’ao wa fedha, alikua naΒ rasta pia, Matilda akaogopa sana, wakati anajisogeza pembeniΒ akajikuta shuka ikiwa inamvuka, ndipo akagundua kua alikuaΒ hana nguo yoyote ile, akarudisha macho kwa mzee kwa MshangaoΒ
Mara, akaingia Bibi mmoja ambaye alionekana wazi kua ni MkeΒ wa Mzee huyo.Β
“Usiogope Binti, Nilikukuta ukiwa hujitambui nikakusaidia”Β Akasema Mzee huyo, Bibi akaketi pembeniΒ
“Na wale watu waliokua wakinifukuzia?” Kwanza Bibi akacheka “Walishambuliwa na jeshi langu” Akasema Mzee huyo “Jeshi lako, unamaanisha nini?”Β
“Siafu waliwashambulia walipotaka kukuchukua, wakakimbiaΒ ndipo nikakusaidia” Hadithi hiyo ikamshtua sana Matilda.Β
“Umepoteza fahamu kwa zaidi ya masaa matano, unahitajikaΒ kupumzika zaidi ili kuvuta nguvu, lakini kwanini wale WatuΒ walikua wakikufukuzia?” Akauliza BibiΒ
“Ni stori ndefu sana” Akasema Matilda baada ya kuona watu haoΒ si wabaya kwake, akawasimulia kilichotokeaΒ
“Pole lakini unaonekana bado una tumaini kwa hayo unayopitia,Β bado una Muda wa kurekebisha mengi” Akasema Babu huyo,Β Matilda akaketi vizuriΒ
“Unamaanisha nini Babu”Β
“Ulipokua umelala nilifanikiwa kuyaona yanayokuzunguka,Β usishtuke sababu ipo Dunia isiyoonekana, ni Dunia ambayoΒ mambo huenda haraka mno, huyo Mtoto unayemzungumzia hapa yupoΒ kwenye usingizi mzito sana, hawezi kuamka kirahisi sababuΒ nguvu kubwa imetumika kumlaza” Akasema Babu huyo, MatildaΒ akashtuka sana
“Usingizi?, kwanza niko wapi hapa nataka kwenda kumwona BintiΒ yangu”Β
“Hapa ni Mkata”Β
“Mkata?”Β
“Ndiyo, kilomita kadhaa kutoka hapa kuna barabara ambayoΒ inaelekea huko ulikotoka”Β
“Umesema kuhusu Usingizi, sijakuelewa”Β
“Namaanisha Mtoto wako amekufa katika Dunia hii lakiniΒ anaishi kuzimu” Matilda akazidi kushtuka, aliyokua akiambiwaΒ yalimpa Mshtuko mkubwa sana, chozi likaanza kumtokaΒ
“Mtoto wangu amekufa?”Β
“Ndiyo lakini usilie sababu bado hajaondoka, mwili umekufaΒ lakini nafsi inaishi kuzimu, kikubwa unatakiwa kuwahi kablaΒ hajazikwa”Β
Wazee hao wakamwambia mengi sana Matilda, wakampa chupa yaΒ Maji, wakamwambia kua akifika anyunyize maji kwenye mwili waΒ Binti yake, ataamka na kua sawa kabisa.Β
Haikuishia hapo, wakampa nauli ya kurejea Dar.
“Mchungaji, naona namtesa Mjukuu wangu, hakuwa na kosa loloteΒ sitaki aendelee kuteseka zaidi. Kesho Patra azikwe” AkasemaΒ Mama yake James, alizungumza mbele ya JamesΒ
“Asante Mama, najiona nimepoteza thamani kubwa sana katikaΒ Maisha yangu. Nitamtafuta Matilda kadiri ya uwezo wangu Mama”Β Akasema James, Siku iliyofuataΒ
Taratibu za Mazishi zikafanyika, mwili wa Patra ukawekwaΒ kwenda sanduku, vilio vilitawala, familia ilizizima, JamesΒ alilia sana mbele ya sanduku la Patra, alijutia sanaΒ kumkataa, akatamani hata aamke ili amuombe msamaha BintiΒ yake, kila aliyefika aliona ni jinsi gani James alikua katikaΒ hali mbaya sanaΒ
Mchungaji George akaongoza maombi ya ibada ya mazishi yaΒ Patra, hatimaye sanduka la Patra likawa linashuka taratibuΒ kuelekea chini, ikasikika sauti ikisema
“Patraaaaaaaa” Ilikua ni sauti iliyotambulika kwenye masikioΒ ya walio wengi, vilio vilikoma, hakuna aliyeamini, walimwonaΒ Matilda akiwa ameshikilia chupa aliyopewa kule MsituniΒ
“Msimzike Binti yangu bila kumwona” Alisema Matilda,Β Mchungaji akawaamuru waliokua wakishusha sanduku kulirudishaΒ juu, Matilda akakimbia hadi kwenye sanduku la Patra, kishaΒ akageuka na kuwaambiaΒ
“Patra hajafa msimzike” Alisema akiwa anatokwa na mchoziΒ
Ni kama watu walipigwa Bumbuwazi, hakuna aliyesema chochoteΒ zaidi ya Mchungaji George ambaye alimuuliza MatildaΒ
“Unasema nini Matilda, Mtoto amekaa kwenye jokofu kwa sikuΒ tatu. Ulikua wapi?” AkaulizaΒ
“Mchungaji, moyo wangu unaniambia nimwone kwanza Mtoto ndipoΒ nieleze kilichotokea, chozi la James lilijikuta likikaukaΒ lenyewe kutokana na Mshangao ambao alikua nao, minong’onoΒ ikaanza kusambaa miongoni mwa waliofika Kwenye mazishi.Β
Mchungaji akawaambia walifungue sanduku ili Matilda amwoneΒ Mtoto wake, sanduku likafunguliwa, Matilda akafungua chupa yaΒ Maji akanyunyiza kwenye sandukuΒ
“Unafanya nini?” Akauliza Mchungaji GeorgeΒ
“Patra ataamka sasa hivi” Alisema Matilda, Mchungaji akaonaΒ Matilda amechanganikiwa, akawaamuru wannaume kumshika MatildaΒ ili Sanduku lifungweΒ
“Mchungaji mwanangu ni mzima naomba Msimzike” alisemaΒ Matilda, ukimya ukatawala kwenye sanduku, alichotegemeaΒ Matilda kilikua ni sawa na njozi ya mchana, Patra hakuamkaΒ kama alivyofikiria, akaanza kuona wale wazee walikuaΒ wamemuongopea, alilia sana huku utaratibu wa kulifungaΒ Sanduku ukifanyika, Mama Naomi akamwambia MatildaΒ
“Mtoto amekufa Matilda hawezi kurudi” Mchungaji akamsogeleaΒ Matilda akamwambiaΒ
“Huu ni mwisho wa Patra lakini siyo mwisho wa Maisha yako,Β pole kwa msiba”Β
Katika hali ambayo kila mmoja alistaajabu, Patra akaamkaΒ kwenye sanduku na kukaa kitako kitu ambacho si tuΒ kilimfurahisha Matilda bali kilimshtua, tokea amezaliwaΒ hakuwahi hata kukaa lakini aliamka na kuketi kiisha akaanzaΒ kushangaa watu. Wasio na moyo wa ujasiri walikimbizanaΒ Makuburini, wachache wakabakia.Β
Muda huo Babu yake Neema alikua amepata ishara mbayaΒ akamwambia NeemaΒ
“Nenda Muhimbili kaokote kile kitu kakitupe jalalani harakaΒ sana”Β
“Babu kwanini unasema hivyo?” Akauliza NeemaΒ
“Nenda Neema fanya haraka sana” Akasistiza Babu yake Neema,Β haraka Neema akakodi Pikipiki ili awahi Muhimbili,Β haikuchukua muda mrefu, akawa amefika Muhimbili, akakimbiliaΒ mahali ambapo alitupa kile kitu, kabla hata hajakiokotaΒ kikawaka na kumwingia machoni, akawa anapiga keleleΒ akilalamika kua haoni, haraka akasadiwa kupelekwa KwaΒ Daktari.Β
Familia ikawa imekaa, kila mmoja akistaajabu maajabu ya MtuΒ aliyekufa kurejea tena kwenye Maisha, ukimya ukawa mwingiΒ sana. Matilda akaanza kuwasimulia kila kitu, siku hiyo ndiyoΒ ikawa siku ya kumwona Mama yake James, huwezi amini PatraΒ alikua ni Mtoto mrembo sana, akitabasamu ni James Mtupu,Β James akaomba Msamaha na kuahidi kua atafunga ndoa na MatildaΒ na kumlea Mtoto.Β
Zikapita siku tatu mambo yakawa shwari, furaha na amaniΒ ikazidi kutamaraki, kwa shukurani, James akampatia Mama NaomiΒ ile nyumba aliyokua akiishi Matilda, akampa pesa pia kwaΒ ajili ya kuanza Biashara. Siku moja akiwa ofisini akapokeaΒ simu ya Mama Neema, alivyopokea akaambiwa kua Neema amepofukaΒ macho, James akamwambia kua ataenda kumwona.Β
Baada ya kazi akaenda Hospitalini kumwona Neema, Mama NeemaΒ akiwa analia sana kwa kile kilichomfika Binti yake.Β
“Mama huna haja ya kulia, Mimi nimelia sana, Matilda ameliaΒ sana, Mama yangu amelia sana. Siku zote Mshahara wa dhambi niΒ umauti Mama”Β
“Lakini James, Neema ana Mtoto wako tumboni, hupaswiΒ kumhukumu moja kwa moja”
“Namshukuru Mungu sababu amefumbua fumbo zito sana, sikuwahiΒ kuwa na thamani kwenu hata kwa yale makubwa niliyowafanyia,Β nilikua mjinga sijui hata nilikwama wapi hadi nikamkataaΒ Mtoto wangu wa damu” Akasema James kisha akataka kuondokaΒ
“James, naomba msaada kama Mama, Neema anatakiwa kwendaΒ kutibiwa India, sina pesa hiyo Mwanangu, msaidie kwa hilo tu”Β
“Siwezi kumsadia adui anayewinda Maisha yangu, alie mbele yaΒ Mungu wake, amwombe amsamehe” Akasema James kisha akaondoka,Β Mama Neema akalia sana huku akijilaumu kwa kusema ni ujingaΒ wake kwani yeye ndiye aliyekua akimshauri vibaya Binti yake,Β akaona ni bora kufa kuliko kuendelea kumwona Neema akiwaΒ kipofu, akaondoka Hospitalini na kumwacha Neema akitesekaΒ kwenye kutanda cha Hospitalini ya Muhimbili.Β
MWISHO
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMΒ Β
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx
Β
18 Comments
Adminiiiiiiiii hongera sanaaa π₯³π₯³π₯³π₯³π₯³π₯³π₯³π₯³π₯³π₯³ dah mwisho mzuri ..kesho anza riwaya nyingine
Kama move kabisa yaani dah nyingine ije mbio basi
Kali sana
Safi sana mwisho nzur riwaya ilikuwa π₯π₯π₯
Daah riwaya nzuri Sana
dah story moja nzuri sana
Asante Mungu wamepata wanachostahiliπ₯π₯π₯
Mmmmmmm,, mbona imeisha kama inaendelea????????!!?????
Big up Admin!
Riwaya unazotupatia zinatupa fundisho katika maisha halisi yanayotuzunguka.
Hongera sana mkuu kwa story nzuri sana
Dah hatari sanaaaaa
Kama move kabisa yaani dah nyingine ije mbio basi
π₯π₯ sio powa imeisha kama utani
Hongera san kiongozi πππ
Tujitahid kumtunza admin asivunjike moyo wakutupa madini mazuri kma hya
ππβ€οΈ
Admini safi kesho anza nyengine
Imeisha vibaya wazaz wake ma patra je