Ilipoishia “James!! tumepima DNA na majibu unayajua kua Patra ni Mtoto wako, kwanini damu yako unaiacha iteseke kisa ulemavu?” alisema Matilda, alipigwa kofi hadi waliokua karibu walishtuka
“Wewe Mshenzi sitaki urudie hiyo kauli, nakwambia nitakufanya kitu kibaya endapo utaendelea kusema kua yule kiwete ni Mtoto wangu, Mtoto halali kwangu atazaliwa kwa Neema na siyo vinginevyo, kwanini unapenda kuniharibia siku Mjinga wewe?” alifoka James, japo alikua kijana mtanashati lakini alikua na hasira sana.
Matilda alikasirika, sababu alipigwa mbele za Watu, Mama Naomi alikua akiona pia japo alikua kwa mbali kidogo lakini ilikua ni aibu kubwa, alikimbilia Hospitalini. James naye aliondoka huku akiacha minong’ono kwa kilichotokea hapo, aliondoa gari haraka sana. Endelea
SEHEMU YA TATU
Mama Naomi akamkimbilia Matilda kujua kwanini James alifikia uamuzi wa kumpiga, hakuna alichokizungumza Matilda sababu bado alikua akilia kutokana na kilichotokea, Mwanaume aliyesababisha akatoroka kwao, akawapa Mawazo wazazi wake aliishia kumpiga na siyo kujali hali ya Mtoto kisa tu ulemavu
“Matilda usilie hebu nieleze kimetokea nini hadi akakupiga?” aliuliza Mama Naomi
“Niache Mama Naomi, ilipofikia nimechoka na mateso ya hii Dunia ni bora hata nife tu” Alisema kwa hasira Sana Matilda huku akilia kwa uchungu sana.
“Huo ni uamuzi wa kijinga sana Matilda, ukifa Patra atazidi kuteseka, angalia jinsi anavyoteseka sasa hivi je ukifa itakuwaje?”
“Sasa nitakaa nikimwangalia Binti yangu akifa mbele ya macho yangu alafu Baba yake akiwa na uwezo wa kumsaidia lakini hafanyi hivyo, ni bora kufa kuliko kumwangalia Patra akifa” Alisema Matilda.
“Nakuomba Matilda kwasasa turudi nyumbani tutafakari jinsi ya kuipata pesa ya Matibabu, hebu nyanyuka” Mama Naomi alimnyanyua Matilda kisha aliondoka naye.
********
“Mimi nina wao wazo Matilda, kwanini usiende kanisani kwenu ukaomba Msaada kwa waumini wakakusaidia?” alisema Mama Naomi, yalipita Masaa matatu baada ya kurejea nyumbani
“Wataweza nisaidia kweli?”
“Ndiyo nina imani kubwa watakusaidia sababu wewe ni Muumini mwenzao”
Ushauri wa Mama Naomi aliufanyia kazi, jioni ilipoingia alienda kanisani, wengi walimshangaa maana baada ya kujifungua hakuonekana tena kanisani, aliofahamiana nao walikua wakimuuliza jinsia ya Mtoto, Maswali ya kuhusu Mtoto yalizidi kumfanya Matilda ajisikie vibaya sana.
“Mbona unalia?” aliuliza Mchungaji mara baada ya Matilda kufika ofisini kwa mchungaji wa kanisa
“Mchungaji Mtoto wangu” Alisema Matilda, Mchungaji alishtuka akamuuliza
“Mtoto wako amefanyaje?”
“Mchungaji Mtoto wangu Mimi” Sauti ya kilio ya Matilda ilisikikika na kumfanya Mchungaji aingiwe na maswali mengi kichwani
“Matilda Mtoto wako amefanya nini, hebu punguza kulia uniambie” Alisema Mchungaji kwa sauti iliyojaa upole wa Hali ya juu sana, kwikwi ilimshika sana Matilda kila alipotaka kusema alijikuta akishindwa, kilio kilimuandama katika kila neno alilohitaji kuzungumza, Mtandio wake aliutumia kufuta chozi lililomiminika kwa wingi, moyo wake ulijawa na simanzi ya hali ya juu sana.
“Matilda tambua unanichanganya sana Mimi, sielewi hata nini unataka kuzungumza. Nakuomba acha kulia sababu ukilia Mimi siwezi kujua kilichokusibu” Alisema tena Mchungaji wakati huo Matilda akiwa ameegemea Meza akiwa analia, hata Mchungaji alilengwa na Mchozi kwa jinsi ambavyo Matilda alikua akilia kwa uchungu, dakika tano zilikatika Matilda akishindwa kusema chochote
“Unasikia Matilda, kua na imani hakuna kinachomshinda Mungu aliye hai, nijuze Mimi ili tujue tunakusaidia
vipi….Unasikia….” Mchungaji alirudia kumbembeleza Matilda, angalau kilio kilianza kupungua
“Na hapo shavuni umekumbwa na nini?” Aliuliza Mchungaji, shavuni Matilda alikua na alama ya kofi alilopigwa na James kule Hospitalini.
“Mchungaji napitia wakati Mgumu sana katika Maisha yangu, Mtoto wangu yupo Hospitalini..” Matilda alijikaza akazungumza
“Ulipotea kanisani kila Mtu akawa anajiuliza upo wapi Matilda, kumbe ulijifungua….Enhee nini kinamsumbua Mtoto wako?” Aliuliza Mchungaji ambaye alionekana kua na umri mkubwa, ngozi nyeusi na mvi iliyokolea vizuri kichwani, akiwa amevalia mavazi ya kanisa na msalaba mkononi.
“Mtoto wangu ni Mlemavu, anasumbuliwa na Mapafu, anahitajika kufanyiwa upasuaji na kibaya zaidi Baba yake Amemkana” Alisema Matilda, kilio kilianza upya baada ya kumaliza kumuelewesha Mchungaji ambaye alishikwa na butwaa, Matilda alikua Muumini wa kabisa hilo sababu hata kwao alikotoka alikua Binti wa kanisa hivyo alivyofika Dar alijiunga na kanisa pia.
“Yesu kristo! pole Binti yangu Matilda, hakuna linalomshinda Mungu wetu aliye hai, yeye halali kwa ajili yetu, Mtoto yupo Hospitali gani?”
“JM Hospital, inahitajika Milioni nane aweze kufanyiwa upasuaji, hapa nilipo sina hata senti tano na kadiri siku zinavyozidi kwenda tumaini la Binti yangu kua hai linazidi kupotea” Alisema Matilda akizidi kulia kaa uchungu sana.
“Twende kwanza Hospitali kwa ajili ya maombi, baada ya hapo kanisa litaangalia utaratibu wa kukusaidia” Alisema Mchungaji akiwa ameshasimama,
“Asante Mchungaji George” Alisema Matilda, waliondoka hapo kanisani kuelekea Magomeni Mapipa ilipo Hospitali ya JM, waliondoka kwa gari maalum ya kanisa, Wakiwa barabarani Mchungaji alimwambia Matilda
“Hili jambo litaisha kwa namna nzuri Matilda, kua na imani thabiti usitetereke. Kupitia Mtihani huu shetani anaweza akajipenyeza na kukuingiza kubaya zaidi endapo hautojiimarisha kiimani” Matilda aliitikia kwa kichwa kisha alijishika tama.
********
“Una uhakika?” lilikua ni swali aliloulizwa Neema, alikua kituo cha polisi.
“Ndiyo sababu yeye ndiye anayeishi pale” alisema Neema kwa kujiamini kisha akatoa kitita kidogo cha pesa kwa siri sana, Polisi akatabasamu sababu ilikua ni ishara kua alichokua akikizungumza Neema kilihitaji kutengenezwa zaidi ili kiwe kikubwa.
“Jina lako?” Aliuliza Polisi akiwa anaandika jalada la kesi “Neema Ngushi, Miaka 32”
“Mshtakiwa?”
“Matilda John, Miaka 28” Alisema Neema
“Vitu vilivyopotea vina thamani gani?”
“Milioni 16” Alisema tena Neema
Baada ya kumaliza kuandika maelezo marefu aliyoyatoa, alipewa RB ya kumkamata Matilda, alichofanya Neema ni kwenda kumfungulia kesi ya upotevu wa vitu kwenye nyumba anayoishi Matilda, hakutaka kuendelea kumwona Matilda katika Maisha yake, pembeni alikua amesimama Mwanaume mmoja ambaye kazi yake ilikua ni kutingisha kichwa tu.
Alipohakikisha amemfungulia kesi, walitoka na Mwanaume huyo wakaingia kwenye gari, wakaondoka kituo cha polisi.
“Unajua huyu Mwanamke anaweza kua kikwazo kikubwa sababu James alikiri kua Mtoto ni wake lakini anaona aibu kulea Mtoto ambaye ni kiwete, sasa hofu yangu ni kwamba akili ya Matilda ikifunguka alalfu akaenda kudai haki, huwenda James akajirudi kwake sababu atatakiwa kumtunza Mtoto kwa lazima na pengine akachukuliwa hatua za kisheria alafu Mimi nikahangaika” Alisema Neema akiwa anaendesha gari
“Hapo usiwe na huruma hakikisha unamsotesha hadi akili imkae sawa, James akijua itakuaje?”
“Hata akijua hawezi kufanya chochote sababu nimeshamwambia kua nataka nitengeneze mchezo ili Matilda akubali kurudi kwao Njombe” Alisema Neema
“Bingoo!!! Sasa tunaenda wapi?”
“Naenda kukuacha kwako Sadam alafu Mimi nirudi nyumbani, kesho tunamkamata Matilda, naamini kitisho hiki kitamfanya akubali kurudi kwao”
“Umetisha sana hakika wewe ni jembe la kujivunia Neema” Alisema Mwanaume huyo kisha akaweka Mkono wake kwenye paja la Neema ambaye alikua na Ujauzito wa Miezi mitatu tu.
*****
Saa 12 Jioni, Gari ya kanisa ilikua ikiingia kwenye geti la Hospitali ya JM Magomeni Mapipa, Matilda alikua amelia sana hadi macho yalimvimba, wakashuka na kuelekea Nje ya chumba ambacho Patra alikua amelazwa, Macho ya Mchungaji na Macho ya Matilda yaligongana na macho ya Daktari ambaye alikua akitoka ndani ya Chumba hicho.
“Dokta samahani hali ya Mwanangu inaendeleaje?” aliuliza Matilda kwa presha.
“Matilda Mtoto anaendelea vizuri kwasasa, aliamka kisha akalala hadi sasa hivi”
“Tunaweza kumwona?”
“Ndiyo lakini hampaswi kumsumbua” Alisema Dokta akiwa anaondoka
“Asante Dokta, Mchungaji twende” Alisema Matilda kisha alifungua mlango wa chumba hicho
“Mwanangu!!” Alisema Matilda baada ya kumwona Binti yake akiwa anapumulia Mashine, Roho ilimuuma sana.
“Oooh Jesus” Alisema Mchungaji, Chozi likaanza kumbubujika tena Matilda, alikua Mtu wa kulia kila dakika kwa namna ambavyo hali ya Binti yake ilikua, Mchungaji akamwambia Matilda
“Kulia hakusaidii chochote, ngoja tufanye kwanza Maombi ili tumkabidhi Mtoto huyu na hali yake mbele za Mungu” Alisema Mchungaji George
Alianza kufanya Maombezi kwa Mtoto Patra, aliomba kwa imani kubwa sana, Matilda naye alizama kwenye Maombi akisaidiana na Mchungaji huyo, maombi yalifanyika kwa sauti ya chini sana ili wasimsumbue Mtoto kama ambavyo Daktari alikua amewaambia. Zilitumika dakika arobaini na tano hadi kumaliza kumwombea Patra, Jasho lilikua likimvuja Mchungaji huyo ambaye kila alivyomwangalia Patra alijiskia vibaya sana kwa jinsi hli ya Mtoto huyo ilivyokua.
“Mungu amepokea Maombi Matilda, anaenda kutenda kwa ajili yako na Mtoto, atafungua minyororo ya mateso kwa Mtoto huyu, amini kua amekwisha kombolewa” Ilikua ni kauli ya kutia moyo ya Mchungaji huyo ambaye alikua amemshika bega Matilda, mara aliingia Daktari akawaambia Muda umeisha.
“Baby leo nimefanya kitu ambacho kitakuondolea hasira sana” Alisema Neema akiwa anakula embe bichi, alikua akimwambia James wakiwa chumbani Usiku.
“Jambo gani hilo?”
“Ni kuhusu Matilda”
“Sitaki hata kumsikia huyo Mwanamke Neema, katika Maisha yangu sijawahi pata ona Mwanamke King’ang’anizi kama Matilda” Alisema kwa hasira James, alionesha wazi hataki kusikia kuhusu Matilda ambaye alitoka kumpiga Kule Hospitalini.
“Usikasirike sababu hili jambo litaenda kumfanya aondoke hapa Dar bila kupenda Bby”
“Nakusikiliza”
“Hii hapa ni RB ya kumkamata kwa kosa la wizi wa vitu kwenye ile nyumba, naamini akilala polisi siku moja akili itamkaa sawa” Alisema Neema kisha alimpatia Karatasi kutoka polisi, James akaisoma kwanza kabla ya kusema Chochote, kisha akamtazama Neema
“Umemfungulia kesi?”
“Ndiyo!! lengo langu apate kitisho kitakachomfanya aiyone Dar chungu, nimefanya hivyo sababu sitaki kumwona Baba Mtoto wangu mtarajiwa anakosa raha” Alisema Neema, James alitabasamu sababu aliitwa Baba Mtoto, alihitaji sana Mtoto
“Mbinu yako ni bora sana Neema, naamini kwenye hili hachomoki, ataondoka hapa Dar atake asitake, tena kwa kuondoa kero nitampatia na pesa ya kuanzia Maisha huko aendapo” Alisema James kwa furaha
“Umeona jinsi gani nakupenda, nakuhitaji na pia nakuthamini, furaha yako ndiyo furaha yangu Mpenzi” Alisema Neema akiendelea kula embe kwa chumvi.
Neema alishajua udhaifu wa James, wala hakutumia nguvu nyingi kumfanya James afurahi, ni kumweleza tu kuhusu ujauzito, alichotaka alipewa bila hata kulazimisha.
Siku iliyofuata, Neema alienda kituo cha polisi akaonana na yule polisi ambaye aliandika jarada la kesi ya Matilda, akaomba askari kwa ajili ya kwenda kumkamata Matilda, akapewa askari polisi wawili akaenda nao moja kwa moja JM Hospital.
Muda huo Matilda alikua kanisani, zoezi la kukusanya pesa kwa ajili ya kuratibu matibabu ya Patra lilikua likiendelea kanisani hapo chini ya uangalizi wa karibu wa Mchungaji George ambayo alimwambia Matilda kua atasimama naye bega kwa bega hadi Patra apone, Mama Naomi alikua miongoni mwa Watu waliofika kanisani hapo baada ya kupewa taarifa na Matilda kua litaendeshwa zoezi la Uchangiaji wa matibabu ya Patra.
Chozi halikuacha kutoka kwenye macho ya Matilda baada ya kuona uchangwaji wa pesa hiyo, muitikio ulikua mkubwa sana kiasi cha kumtia moyo hata Mchungaji wa kanisa hilo ambaye ni Mchungaji George. Nyimbo za kusifu zilikua zikiimbwa, kila mwenye kua nacho alitoa kidogo alicho nacho kwa moyo wote bila kujali
Waumini waliungana kwa pamoja ili kurejesha furaha ya Matilda ambaye alikua haamini macho yake jinsi kapu lilivyokua linajaa noti. Mikono ya Matilda ilikua kwenye mdomo wake huku chozi likiendelea kuvuja, tabasamu pana lilionekana kwenye sura ya Mama Naomi ambaye alitoa wazo la Matilda kurejea kanisani. Mchungaji George alimtia moyo sana Matilda katika kila hatua ambayo walikuwepo, baadaye Mchungaji alikabidhiwa kapu lenye fedha hizo.
Watu maalum wa kuzihesabu walianza kazi hiyo huku Mchungaji George akitoa neno kanisani hapo
“Hakika leo Bwana ameinuliwa, kwa moyo huu uliooneshwa hakika roho mtakatifu yupo ndani yetu, kusimama na Mwenye matatizo kunaongeza Baraka, hamjui ni kiasi gani Mungu anaenda kuongeza kilichopungua kwenu. Mungu awabariki sana kwa jina la yesu” Alisema Mchungaji huku kanisa likiitika haswa kwa kusema
“Aaameen” Matilda alizidi kulia kwa uchungu sana, kilichomliza siyo tu kuumwa kwa Binti yake bali ni maisha anayopitia baada ya kuitwa Mama, jinsi watu baki wanavyosimama na yeye wakati Mwanaume aliyemfanya akatoroka kwao hajigusi kwa lolote lile, alipiga magoti na kusema
“Asante Yesu” Mikono yake ikiwa juu, Mchungaji akaja na kumwinua
“Matilda, kanisa linakuhitaji useme neno” Mchungaji George alimsogeza Matilda hadi Madhabauni, akampa kipaza sauti. Aseme nini? ndicho ambacho Matilda alikua akiwaza, umati ulikua mwingi hapo kanisani, macho yote yakawa kwa Matilda Msichana wa miaka 28
Alikua akitetemeka kwa kila alichofikiria kukisema, alikua kama amepigwa shoti vile, alimtazama Mama Naomi ambaye alimpa ishara ya kumtia moyo kua aseme chochote hapo kanisani
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya NNE Ya PIGO TAKATIFU Msisahau COMMENTS Ziwe Nyingi
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx
9 Comments
Daaaah jmn
Kama naangalia tamthia vileee😭😭
Wakati wa Mungu ukifika Kila lililoshindikana litafanyika kwani hakuna jambo gumu kwake
Mungu hakosei kwakweli
Mambo Yazidi kuwa motooo
God’s ears are not deaf that he cannot hear your 😭 cry ..
Kuna funzo apa
Mamb ni moto
Am I crying too 😭
Daah pole san kam wap