Ilipoishia “Kwahiyo umeanza kua na huruma si ndiyo? Basi hakuna sababu ya kujificha, jitokeze hadharani ujitangaze kua Bilionea mwenye Mtoto Mlemavu, si una shida sana ya Mtoto basi hakuna sababu ya Mimi kubeba huu mzigo wakati una Mtoto unaye muonea huruma” Alisema Neema kwa hasira zaidi, akanyanyuka ili aondoke lakini James akamshika mkono kwa lengo la kumzuia asiondoke
“Mpenzi hupaswi kua na hasira sababu wewe ni Mama mtarajiwa, natamani haya mambo yaishe kwa namna nzuri, basi nitaenda Polisi kwa ajili ya kuzungumza na Matilda ili aondoke hapa Mjini” Alisema James lakini Neema akatoa Mkono wa James akaelekea chumbani. Endelea
SEHEMU YA TANO
“Nifanye nini sasa?” Alijiuliza James akiwa ametulizana kochini, moyoni alikaa kikao akakubali kua Patra ni Mtoto wake lakini aibu ya kuonekana Bilionea ana Mtoto mlemavu hakutaka kuipata kabisa ndiyo maana alitumia nguvu zote kumkana Mtoto lakini upande wa pili moyo wake ulijawa na maumivu makali sana, akanyanyua simu yake akampigia rafiki yake
“Chilo naomba tuonane Muda huu, tuonane palepale” Alisema James kisha akanyanyuka na kuvuta kitasa cha mlango akatoka, akaingia kwenye gari yake ya kifahari kisha akaondoka nyumbani hapo na kuelekea Sinza Vatcan, akaingiza gari maegesho ya Pub moja yenye hadhi kisha akaelekea mahali ambapo alipanga kuonana na rafiki yake anayeitwa Chilo.
Alimkuta rafiki yake akiwa hapo anamsubiria, alipomwona aligundua kuna jambo lililomsibu, licha ya kua rafiki yake pia alikua mshauri wake wa mambo mengi binafsi, alijitupa kwenye kiti
“Niambie James” Alikaribishwa na neno hilo kabla ya salam “Mambo si shwari Chilo” Alisema James
“Unamaanisha nini?”
“Ni kuhusu Matilda”
“Enhee….”
“Neema ameenda kumfungulia kesi ya wizi lengo likiwa kumtisha ili aondoke hapa Dar, lakini moyo wangu nahisi unaumia sana kwa hili” Alisema James akiwa ameshika kichwa chake
“Oooh imefikia huko Babuu…Kwanini unampa mamlaka makubwa Neema kiasi hicho James….Huoni kama Mtoto atateseka?”
“Nifanye nini Chilo na unajua nahitaji sana Mtoto kutoka kwa Neema, sina sauti sababu ana mimba ya Miezi mitatu na anatishia kuitoa endapo nitafanya makosa, nakiri Kuumia sana kuhusu Matilda na ambacho Mtoto anapitia, unajua wakati mwingine natamani hata Mtoto angekufa tu”
“Unasema nini James, Mtoto afe kisa ulemavu alionao, bado Patra ni Mtoto wako hata ufanye nini hakuna
kitakachobadilika, zaidi hapo unamtesa tu, Bro kubali hali halisi kua Patra ni Mtoto wako wa kwanza” Alisistiza Chilo
“Bilionea nawezaje kukubali aibu ya kua na Mtoto Mlemavu Chilo? nitaweka wapi sura yangu endapo Watu watajua….nakosa amani kabisa, Mimi nataka kufanya jambo fulani ili niwe na amani, nataka kumpatia pesa ya kutosha Matilda arudi Njombe na Mtoto alafu baada ya hapo nitakubali rasmi kua Baba wa Patra lakini kwa siri sana” Alisema James akiwa anatokwa na jasho
“Katika vitu ambavyo utakuja kujuta mbele ya safari ni kumtelekeza yule Mtoto, ya Mungu mengi alafu la mbele wewe hulijui James, Hujui ni maumivu kiasi gani anayapata Matilda, kumbuka amekupa heshima ya wewe kuitwa Baba, ametoroka kwao kwa ajili yako bado huoni thamani na heshima aliyokupa ikikufanya ujione ni Mwanaume uliye kamilika?” Maneno ya Chilo yalimfanya James amimine Unywaji kwenye glasi kisha akanywa, koo ikawa lahini sana huku akiugulia maumivu ya kinywaji alichokunywa, alikunja sura kama anayehisi maumivu, akapangusa mkono wake kinywani alafu akamwambia Chilo
“Tatizo ni aibu nitakayokumbana nayo Chilo, najua Patra ni Binti yangu lakini siwezi kulea Mtoto mlemavu” Alisema kisha akanyanyuka kwa ajili ya kuondoka
“Unasimamia hilo hadi mwisho?” Akauliza Chilo akiwa naye ameinuka
“Huwenda” Akajibu James huku akiingia kwenye gari yake, Macho ya Chilo yakamsindikiza Bilionea Kijana akitokomea zake
Usiku uliingia, Mchungaji George alisubiria hadi alichoka, hakupewa nafasi ya kuingia na kujua maendeleo ya Matilda, akainuka huku sauti fulani ikimsindikiza nyuma yake
“Mtu wa Mungu unafanya nini hapa hadi muda huu?” Mchungaji George akageuka, ilikua ni sauti ya mmoja wa polisi aliyekua lindo, Mchungaji akajipangusa vumbi kisha akamjibu
“Mungu aliye hai amenipa kibali cha kuondoka sasa hivi, nasikitika naondoka bila kujua Binti anaendeleaje” Alisema Mchungaji George kwa sauti iliyojaa upole na maumivu makubwa sana, Polisi mwenye Buduki akasogea na kumwambia
“Dunia uliyopo na Dunia tunayoishi sisi ni vitu viwili tofauti kabisa, unafikiria utashinda?”
“Mimi siwezi kua Mshindi sababu yupo anayejua namna ya kushinda kwenye nyakati ngumu, Kijana nakutakia Usiku mwema” Alisema kwa mafumbo mchungaji George kisha akaingia kwenye gari ya kanisa akaondoka mahala hapo taratibu huku akiwa mwingi wa kutafakari.
“Mnataka nini kwangu?” aliuliza Matilda usiku huo akiwa kwenye chumba maalum kilichoandaliwa kwa ajili ya mateso yake, kilikua ni chumba chenye kiza la kutosha, akamulikwa tochi usoni, masikini alikua ameumia vibaya, alichanika mdomo huku damu ikimvuja
“Nimekueleza mara nyingi kua unapaswa kuondoka Hapa Mjini vinginevyo utazidi kuteseka kisha utafungwa na kumkosa Binti yako mazima” Alisema Polisi ambaye alikua akimpa mteso Matilda, ilionesha polisi huyo alimtesa Matilda kwa muda mrefu hadi alichoka, akawa anahema kwa uchovu
“Kama mnaweza kuniuwa ni Bora mfanye hivyo lakini siko tayari kubeba msalaba wa dhambi kwa Binti yangu, siwezi kuondoka hapa” Alisema Matilda kwa ujasiri, sauti ya rungu kuanguka ikasikika kisha geti likafungwa, polisi aliondoka na kumwacha Matilda akiwa hoi sana. Muda huo Bilionea James alikua akifika nyumbani kwake, jumba lilikua giza tofuati na alivyotegemea, Mlinzi alipomfungulia geti ikabidi amuulize
“Kwanini jumba lipo giza?” aliuliza akiwa ameshashuka kwenye gari
“Madam hayupo tokea jioni, hata hivyo wafanyakazi wengine amewapa likizo isipokua Mimi tu” Alisema Mlinzi huyo,
“Hayupo tokea jioni!?”
“Ndiyo Bosi kwani hakukuaga maana alitoka na begi dogo hivi” Alisema tena Mlinzi, James akaelewa,
“Ok! endelea na kazi” Akasema James kisha akaelekea kufungua mlango, akawasha taa, kisha akampigia simu Neema lakini simu haikupokelewa usiku huo.
Asubuhi ya siku iliyofuata, James hakutaka kufanya chochote zaidi ya kutaka kujua Neema alikua ameenda wapi, akakumbuka ile kauli kua anaweza akatoa Mimba, akazidi kuingiwa na wasiwasi, akapiga simu mahali akiwa ameegemea gari yake
“Hello Mama” Alisema James mara baada ya simu kupokelewa “Unasemaje James” Ikasikika sauti upande wa pili “Nakuja sasa hivi kuna jambo ambalo halipo sawa Mama”
“Sawa…Karibu!” ukasikika tena simu upande wa pili kisha simu ikakatwa, Alikua ameshajiandaa hivyo kilichobakia kwake kilikua ni kutoka tu, akapanda kwenye gari yake kisha akatoka kuelekea mahali alipopiga simu.
Haikuchukua muda mrefu sana kufika alipokusudia, alikua tayari yupo mbele ya nyumba moja iliyo na hadhi kubwa, akapiga Honi, mara geti likasukumwa na kumpa nafasi aingize gari humo, akiwa anaingia maegesho ya Magari akaliona gari la Neema likiwa limekwisha paki eneo hilo, ikampa ishara kua Neema yupo hapo,
Alionekana kua ni Mtu aliyesongwa na mawazo sana James, akashuka kisha akaelekea ndani ya nyumba hiyo, akamkuta Neema akiwa ameweka Miguu yake kwenye miguu ya Mwanaume mmoja aliyekua akichezea simu, hakuna aliyeshtuka kati yao hata baada ya kumwona James, mshangao ukawa mkubwa kwa James, Mara Mama mmoja akafika hapo akitokea chumbani
“James karibu!” Alisema Mama huyo ambaye naye aliketi kabla ya James kuketi, James akaketi taratibu huku akimtazama Mwanaume huyo
“Oooh ni Masudi huyo, Kaka yake Neema ametokea Dodoma” Alitambulisha Mama huyo ambaye alionekana kua ni Mama yake Neema, angalau kidogo sura ya James ikaingia uchangamfu, Neema alionekana kumkasirikia kabisa James, hakutaka kusema naye chochote kile
“Mama tunaweza kuongea?” alisema James
“Hakuna shaka nakusikiliza James” Alisema Mama huyo, James akanyanyuka na kumpa ishara kua alikua akihitaji kuzungumza wakiwa wawili tu. Wakatoka ndani wakaelekea nje kuzungumza
“Mama, Neema alilala hapa?” aliuliza James
“Ndiyo alilala hapa”
“Amekueleza chochote?”
“Nilihitaji kwanza ufike James, hebu fikiria kwa akili yako, Mwanamke ambaye anaenda kukupa heshima ya kuitwa Baba unamtendea hivi, hujui kama Mjamzito anapaswa kupewa malezi ya utofauti?” Alisema Mama huyo
“Lakini Mama, lilikua ni jambo la Mimi na Yeye kuelewana tu na hakua na sababu ya kuja huku”
“Amekuja huku sababu ni kwao, hukumkuta shimoni, Neema ana kwao na Mimi ni Mama yake, kila Mama katika Dunia hii anapigania Mtoto wake aishi vizuri sasa Mtoto wa Neema atakua katika hali gani ikiwa tayari una Mtoto mwingine na hutaki yeye afanye maamuzi?”
“Siyo hivyo Mama yote nimezungumza na Neema, ilikua ni Mimi kuanza kutekeleza, Mama nisingewanunulia hii nyumba kama nisingekua na nia na Neema, nimefanya yote sababu ya upendo wangu, najua Neema anaenda kua Mama miezi michache ijayo, jukumu langu ni kuhakikisha natekeleza ahadi zangu…”
“Ikiwemo na kumrudisha kwao Matilda si ndiyo?” alihoji Mama Neema akionekana kuutambua vizuri mgogoro wa James na Neema, kigugumizi kikamjaa James
“Unaona unajiuma uma sababu bado una mapenzi na huyo Mwanamke, hukua na sababu ya kuhitaji Mtoto kutoka kwa Neema wakati tayari una Mtoto wako James…”
“Mama, yote yanazungumzwa sababu naonekana Mimi kama vile sitaki Matilda aondoke, kinachonipa wakati mgumu ni hali ya Mtoto wake, laiti kama angelikua mzima basi angeondoka muda mrefu. Kwasasa yupo kwenye matibabu, akipona ataondoka Mama”
“Hivyo Eee? sasa akishaondoka ndipo utamchukua Neema, kwasasa Mwache aishi Hapa” Alisema Mama Neema kisha haraka akaingia na kufunga mlango, James akajaribu kufungua na kuita Lakini hakuna aliyefungua mlango.
“Mimi ni Mama Naomi” Alisema Mama Naomi, simu ikiwa sikioni akiwa anamnyonyesha Naomi, alikua amekaa kwenye gogo chini ya Mti nje kidogo ya eneo analoishi, Sauti ya Jack ikasikika
“Oooh!! uko wapi?” alihoji Jack ambaye ni mfanyakazi katika ofisi ya James
“Nipo nyumbani hata hivyo najiandaa kuelekea Hospitalini” Alisema Mama Naomi akiwa anaweka titi vizuri baada ya Naomi kushiba
“Tunaweza kuonana?”
“Hakuna shida sijui tutaonana wapi?”
“Nielekeze hiyo Hospitali, mchana nitakuja hapo” “Ni MJ Hospital, Magomeni Mapipa”
“Sawa Naijua hiyo Hospitali, naomba ubaki hadi mchana”
“Haya sawa!” alisema Mama Naomi kisha alikata simu hiyo, haraka akamweka Naomi mgongoni, akaelekea kituo cha Daladala kwa ajili ya kuelekea Hospitali, lakini alihitaji kujua kwanza kuhusu Matilda, akapiga tena simu kwa Mchungaji, akaambiwa kua hadi kufikia muda huo hakukua na taarifa nyingine kuhusu Matilda, alinyimwa hata haki ya kumwona. Majibu hayo yalimfanya Mama Naomi amuonee huruma sana Matilda, akaweka simu kwenye sidiria kisha akazidi kuelekea kituo cha daladala.
Mwendo wa masaa mawili, Mama Naomi alikua akiingia viunga vya Hospitali ya JM, alikua amechoka kutokana na purukushani za hapa na pale katika Daladala, moja kwa moja safari yake ikaelekea hadi kwa Daktari ambaye alikua akimwangalia Patra.
“Dokta…..Hali ya Mtoto inaendeleaje?” akauliza Mama Naomi akiwa anafuta jasho lililokua likimtiririka, hakukua na hali ya uchangamfu kwa daktari huyo kisha akasema
“Ni Mungu pekee aliyeishikilia pumzi ya Mtoto, tumaini lipo kwake. Ina maana hadi sasa hamjafanikisha chochote, vipi kuhusu Mama wa Mtoto?” akahoji Daktari huku akiwa amemkazia Macho Mama Naomi
“Mama wa Mtoto yupo polisi, amekamatwa tokea jana mchana, pesa zilikua zimekwisha patikana na kibaya zaidi amekamatiwa hapa” Alisema Mama Naomi huku akiweka kituo
“Amekamatwa na Polisi, kwa kosa gani?”
“Kwa Madai ya polisi ni kua ametuhumiwa kwa wizi” “Ina maana Pesa ya matibabu ya Mtoto alienda kuiba Mahali?”
“Hapana, pesa zilichangwa kanisani Mimi nikiwa shahidi wa hilo hata Mchungaji wa kanisa akiwepo, lakini cha kushangaza amekamatwa akipewa shutuma hizo za wizi kitu ambacho si kweli, namjua vizuri Matilda si Mtu wa kuchukua kitu cha Mtu hata mara moja” Alisema Mama Naomi
“Unajua hali ya Mtoto inazidi kua mbaya pengine siku chache zijazo tunaweza kumpoteza, kiasi cha pesa kinachohitajika ni kingi mno, hakuna namna nyingine zaidi ya kupatikana ili Mtoto atibiwe, vinginevyo mtamkosa kabisa” Akasema daktari huyo
“Eeeh Mungu sasa tunfanye nini waja wako, huu mtihani mzito sana Jamani” Akasema Mama Naomi
“Nenda kahangaike, pesa ya Matibabu madogo madogo na dawa za kupoza ugonjwa naendelea kuzilipa Mimi lakini haitosaidia kwani matibabu makubwa yanahitajika” Alisema Daktari.
“Sawa Dokta, sijui hata niingilie wapi….Eeeh na Mchungaji huyo anapiga” Akasema Mama Naomi, akapokea simu aliyokua ameishikilia mkononi, sauti ya Mchungaji ikasikika
*********
Masaa kadhaa baadaye yalimkuta Mama Naomi akiwa ameketi nje ya Hospitali akisubiria simu ya Jack ambaye aliahdi angefika hapo Hospitalini kwa lengo la kuzungumza naye, njaa ilikua ikimtafuna Mama Naomi, alikua akinyonyesha hivyo ni kawaida kwa Mama kama huyo kua na njaa muda wote, Naomi alikua tayari amelala akiwa amemlaza mgongoni, Mara simu yake ikaita, mpigaji alikua ni Jack
“Eeh Mungu asante anapiga” Alisema Mama Naomi akiwa anahangaika kuipokea
“Habari” ilisikika sauti ya Jack mara baada ya simu kupokelewa
“Nzuri tu sijui wewe siku yako imeendaje?”
“Namshukuru Mungu, nakuja hapo Hospitalini, si bado upo?” “Ndiyo nipo utanikuta”
“Haya ndiyo natoka ofisini” Akasema Jack na kukata simu.
“Mama huwenda James ameamua kukaa mbali na Mimi kwasababu ya ulichomwonesha?” Ilikua ni sauti nyororo ya Neema akiwa ameketi kwenye Bustani, alikua akizungumza Na Mama yake
“Hivi unajua thamani ya Mtoto wewe kwa hawa matajiri, hawezi kabisa sababu anajua unaenda kumpatia Mtoto siku chache zijazo, Mtoto ambaye atarithi kila kitu chake. Najivunia kukuzaa Neema, pasi na wewe ningekua naishi kule Uswahilini nauza vitumbua lakini leo nipo hapa kwenye Bangaloo” Alisema Mama yake Neema akiwa anatabasamu
“Lakini Mama mimi nina hofu sana maana tokea asubuhi hadi muda huu James hajapiga simu, au amekasirika?
“Wasiwasi wako unatokana na nini kwani James ndiye Baba wa Mtoto?”
“Hata kama Mimba siyo yake lakini ameniahidi vingi ambavyo sitaki kuvikosa ndiyo maana nimehonga pesa kwa askari ili matilda akubali kurudi kwao”
“Basi Mimi Mama yako nakuhakikishia kua James hana ujanja mbele yako sababu ni Mama mtarajiwa!! ila tu punguza ukaribu na Masudi pale unapokua karibu na James vinginevyo utaharibu mambo, bado hatujafaidika na utajiri wake, ndiyo kwanza tunaanza kula” Alisema Mama huyo kisha akapeana mikono na Neema
Ulikua ni Mpango wa Mama huyo ili wapate pesa kutoka kwa James ambaye alikua na shida sana ya kupata Mtoto atakayerithi mali zake zote siku zijazo.
Matilda alionekana kua kikwazo sababu alikua na Mtoto wa James japo Mtoto huyo alikataliwa na James kisa ulemavu.
Ndani ya kituo cha polisi, Matilda akiwa amekaa sakafuni ndani ya Mahabusu aliyohifdhiwa baada ya kupigwa usiku kucha, alikua hoi sana akiwa anataja jina la Binti yake Patra, Chozi lilikua likimbubujika, alikua amechoka hawezi hata kunyanyuka. Mchungaji George alikua amekaa nje ya kituo hicho, Mara gari nyeusi iliyoonesha kua haikua gari ya thamani ndogo iliingia ndani ya Uzio wa kituo cha polisi.
Akashuka James akiwa amevalia Miwani nyeusi, akaongoza moja kwa moja hadi mapokezi, hakuhitaji kujitambulisha sana sababu mwonekano wake pekee ulionesha yeye ni Mtu wa Namna gani
“Nahitaji kumwona Matilda” Alisema James akiwa ameegemea meza ya mapokezi, mbele yake kulikua na polisi wa kike ambaye alikua akimsikiliza
“Zunguka” Akasema Polisi huyo huyo akiuangalia utanashati wa James, Haraka James alizunguka akamfuata Polisi huyo ambaye alimpeleka James hadi Mahabusu aliyohifadhiwa Matilda
“Wewe Hebu nyanyuka” Akasema Polisi huyo akiwa anagonga nondo za Mahabusu kwa kutumia kiatu chake, Matilda akaamka na kugeuka, akamwona James akiwa hapo, taratibu akajikokota hadi karibu na James, katika hali isiyo ya kawaida kutokana na hasira akapeleka mkono na kumshika shingoni James, akaing’ang’ania shingo ya James kwa nguvu na kumfanya James akose pumzi, yule polisi akasogea haraka na kupiga Mikono ya Matilda.
James akawa anakohoa baada ya Matilda kumwacha James, kilichowatengenisha kilikua ni geti la Mahabusu hiyo
“Uko sawa?” akauliza polisi huyo
“Aaah Usijali nipo sawa” Akasema James akiwa anajifuta uso kwa kutumia kitambaa, wakati hayo yote yanatokea kulikua na polisi mmoja ambaye alikua amekula pesa ya Neema kwa ajili ya kumshikilia Matilda kwa kesi bandia, akawa anafwatilia kujua kitakachoendelea hapo
“Matilda huna haja ya kunionesha chuki kiasi hiki, Mimi siye niliyesababisha ukawa hapo leo hii” Alisema James
“Kama si wewe Mwanamke wako anapata wapi ujasiri wa kuyafanya yote haya?, sijui wewe ni Binadamu katili kiasi gani, Uko tayari Mtoto afe kwa kukosa pesa ambayo ingeweza kumtibia, James Mtoto yupo Hospitali alafu unashiriki kunichezea Mchezo mchafu namna hii?” Alisema kwa hasira Matilda, moyo wa James uliumia sana kwa jinsi ambavyo Matilda alikua ameumizwa vya kutosha
“Matilda huwezi nielewa lakini kwasasa kubali tu kurudi nyumbani, nakuhakikishia nitamtunza Mtoto wako, nitahakikisha unaishi Maisha mazuri lakini kwasasa nenda ili kuepusha shari” Alisema James
“James!! kama unafikiria nitamsaliti Mtoto wangu hilo litoe katika akili yako, nitapambana hadi tone la mwisho, siku Mtoto wangu anaingia Kaburini ndiyo siku ambayo nitakata tamaa, nitawaambia nini Wazazi wangu,….( Anacheka kidogo) au niwaambie Baba yake alikufa?” Chozi la maumivu lilikua linavuja kwenye macho ya Matilda
“Natamani ufumbue macho yako uone ni jinsi gani nipo katika wakati Mgumu Matilda, nenda tu nyumbani yasije kutokea mambo mengine, ukikubali nitamtibu Patra”
“James! kumtibu Mtoto wako siyo jambo la hiyari hilo ni jambo la lazima, ni lazima umtibie patra, na laiti kama hutofanya hivyo nitahakikisha unafirisika” Alisema kwa hasira Matilda hadi James akashtuka, mara polisi akamwambia James
“Muda umekwisha” Alisema akiwa anamtoa James ambaye alikua akitafakari kauli ya Matilda kua atahakikisha ana firisika
“Matilda kubali kuondoka hapa Mjini nakuomba, rudi Njombe” Alisema James akiwa anaondolewa hapo, yule polisi akampigia simu Neema akamwambia kua James alikua hapo kuzungumza na Matilda.
“Nipo kwenye maegesho ya Magari” Ilikua ni sauti ya Jack ambaye alikua ameshafika kwenye Hospitali aliyolazwa Patra, Mara moja Mama Naomi akaelekea Maegesho kuonana Na Jack, alijisikia faraja sana kumwona Jack ambaye pengine angekua Msaada
“Poleni kwa matatizo, Mtoto yupo wapi?” akauliza Jack “Wodini”
“Ooh naomba nimwone”
“Haya twende kwakua wamesharuhusu kwa leo” Akasema Mama Naomi kisha akaongoza kuelekea wodini kwa ajili ya kunwona Mtoto Patra, wakapewa mavazi maalum kwa ajili ya kuingia kwenye wodi hiyo ambayo ilikua chini ya Uangalizi maalum, Patra alikua amelala juu ya kitanda, alikua hawezi kula mwenyewe bali kulishwa kwa mipira, alikua mdhaifu mno, macho yalimtoka Jack, ilikua ni jambo ambalo lilimshangaza sana kwa Bilionea kama James amtelekeze Mtoto ambaye anateseka kiasi hicho, akasogea na kumtazama vizuri Patra
Chozi lilimbubujika Jack huku akiishiwa hata aseme nini, mshangao mkubwa ulimjaa Jack, akamtazama Mama Naomi
“Hiyo ndiyo hali halisi Dada, Mtoto anateseka Mno, hakuna tumaini” Alisema Mama Naomi akitoa tabasamu la maumivu, japo hakua Mtoto wake lakini Maisha ya Patra na Mama yake Matilda yalimgusa mno.
“Masikini….hebu tuzungumze vizuri nje” Akasema Jack akionekana wazi hawezi kuvumilia kuangalia namna Patra alivyokua akiteseka na homa ya Mapafu.
“Jamani roho imeniuma sana, siamini kama Bosi wangu anaweza kufanya hivi, unajua huu ni zaidi ya Unyama?” akasema Jack akiwa ameketi, Mama Naomi akiwa amesimama
“Hatuwezi kumsingizia, Patra ni Binti yake wa kumzaa, ni damu yake lakini kwakua ni Mlemavu ameamua kumkataa kabisa” Akasema Mama Naomi lakini moyo na akili ya Jack haikutaka kuamini kabisa kwa namna ambavyo Bosi wake alikua akiishi naye ofisini
“Yupo kituo gani Mama yake?” akauliza
“Ukihitaji nitakupeleka hata sasa hivi”
“Basi twende huko” akasema Jack kisha wakaelekea kwenye gari, safari ya kutoka Hospitali kuelekea kituo cha polisi ilianza
Masaa kadhaa baadaye walifika Kituo cha Polisi, ilikua ni majira ya jioni, jua likiwa linaangaza Ulimwengu dakika za mwisho. Waliposhuka walikutana na Mchungaji George ambaye alishinda hapo kituoni kutwa nzima hadi mida hiyo ya Jioni
“Shikamoo Baba” Akasalimia Jack
“Marhaba….Vipi hali ya Mtoto?” akauliza Mchungaji
“Hakuna tumaini Mchungaji, tumehangaika mno huku na kule bado ngoma ngumu, bahati nzuri yule Daktari analipia gharama za matibabu ya Patra japo kidogo kidogo ili kusogeza hizi siku maana bila hivyo tungekua na simulizi nyingine kabisa” Akasema Mama Naomi
“Hata hapa ngoma bado ngumu, sijamwona Matilda tokea asubuhi nimefika hapa hadi muda huu. Umeongozana na Nani?”
“Huyu ni Mfanyakazi kwenye ofisi ya James Mwanaume aliyezaa na Matilda”
“Ooh karibu Sana”
“Asante Baba, sijui wataniruhusu kumwona Huyo Matilda?”
“Mh! sina hakika labda ukajaribu bahati yako tu” Akasema Mchungaji, Jack akakitazama kituo cha polisi kisha akaelekea huko huku Mchunagaji akiendelea kupewa maelezo kuhusu Jack
Kiatu kirefu cha Jack kikagusa ngazi na kuanza kupandisha kuelekea mapokezi yalipo, alipofika akamkuta askari aliyekua zamu hapo.
“Nikusaidie nini?” aliuliza
“Naitwa Jack! nimekuja kumwona Matilda” Alisema, yule polisi akamtazama kwa sekunde chache kisha akashusha pumzi na kumweleza kua
“Ni dakika mbili tu, huyu Mtu hapaswi kuonwa na yeyote, nafanya hivi sababu wewe ni Mwanamke mwenzangu” Alisema kisha akaongezea
“Fanya haraka” Akaelekezwa mahali ambapo angemwona Matilda, japo dakika mbili zisingetoshea kuzungumza naye ila alihitaji kumwona na kupata uhakika kua ana Mtoto na Bosi wake, akapelekwa chumba kimoja ambacho kilikua rasmi kwa ajili ya kuonana na Mahabusu, akasubiria hapo Matilda aletwe, sekunde chache Matilda akafika hapo akiwa ameongozana na yule Polisi
Hakumkumbuka Jack sababu alimwona kwa Mara ya kwanza pale ofisini kwa James hivyo ilikua rahisi kwake kukubali kuonana na Jack, akaketi huku akiwa anamtazama sana Jack
“Samahani na pole Matilda, Naitwa Jack” Alijitambulisha Jack
“Unanifahamu Mimi?” akauliza Matilda akionekana alikua ameteswa sana, uso ulikua na majeraha kadhaa
“Ndiyo nakufahamu japo si sana”
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya TANO Ya PIGO TAKATIFU Msisahau COMMENTS Ziwe Nyingi
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx
9 Comments
Daaah! Yamoto
Duhhh 🥺mpunguzie adhabu jmn
Balaa
Inahuzunisha na kufundisha ,hongera kwa utunzi mzuri
Kwa kweri
Hongereni ni kijiwe kizuri sana hiki
Nzuri sana ase, Inatufunza katika maisha haya damu ni nzito kuliko maji, Af polisi ni kiumbe hatar sana
Next please😍🙏
dah oya ni huzuni sana