Ilipoishia “Muda huo Magari mawili yalikua yakiingia Hospitalini hapo kwa kupishana dakika tano, aliyekua wa kwanza kuingia alikua ni James, alipotoka tu kwa Chilo aliona ni bora alekee Hospitali kumwona Patra sababu nafsi ilikua ikimsuta sana. Akaketi kwenye gari iliyo Paking kwa dakika kadhaa akitafakari namna mambo yalivyokua yakiendelea, Gari ya pili ilikua ni gari ya Neema, kila mmoja aliegesha gari kwa upande wake lakini James alikua na nafasi ya kumwona Neena sababu alikua amepaki sehemu yenye magari mengi, akaliona gari la Neema likiingia akajiuliza Neema amefuata nini pale Hospitalini. Endelea
SEHEMU YA NANE
Hofu ikatanda kwenye moyo wake sababu Neema alishasema kua atamuuwa Patra, katika hali isiyo ya kawaida James akajikuta akiumia ndani ya moyo wake, akatamani kushuka ili amfwatilie lakini moyo wake ukawa unamsuta mara kadhaa huku akimshuhudia Neema akishuka na kuanza kutembea kwa Mguu kuelekea ndani zaidi. Akawa kwenye vita kubwa sana ndani yake hadi aliposhinda na kuamua kushuka kisha akaanza kumfwatilia Neema, kumbuka Neema alikua amepewa ile dawa na Babu yake akaiweke katikati ya Hospitali ya Muhimbili ili Mtoto Patra aonekane kusudi auawe
“Huyu amefwata nini hapa Hospitalini?” akajiuliza James akiwa anaendelea kumfwatilia, James alifahamu mahali alipolazwa Patra, Neema akawa anaelekea huko pasipo kujua kua ndiko aliko Patra, lakini baadaye akabadilisha uelekeo kitu ambacho kilimfanya James ashushe presha yake. Neema alikua makini sana tena akionekana ni mwenye kujiamini kabisa, James hakutaka kukubali kushindwa akataka kujua ni jambo gani limempeleka Neema Hapo Hospitalini.
Matilda akiwa katika chumba chenye giza, hakujua mahali hapo ni wapi isipokua alijua kua alikua amehamishwa kutoka pale alipokua zamani, alimfikiria sana Binti yake, akawa anasikia walinzi wakizungumza, tena wakibishana masuala ya Mpira, Chumba alichopo hakikumpa ruksa ya kuona kilichokua kikiendelea nje isipokua aliisikia kelele za hao walinzi pekee, alijua yupo mafichoni, akaanza kupiganisha akili ili ajue anaweza vipi kutoroka hapo.
Basi, James akaendelea kumfwatilia Neema taratibu tena kwa umakini huku akiwa na maswali mengi sana kichwani. Neema naye akazidi kuongeza mwendo huku lengo likiwa kufanya kama ambavyo Babu yake alimwambia, alipofika katikati ya Hospitali, akageuka huku na kule huku James akijibanza mahali ili aone Neema anaelekea wapi.
Akazuga kidogo kabla ya kuingiza mkono kwenye Mkoba kisha akatoa hicho alichopewa na Babu yake alafu akakitupa na kukificha kwa Majani kwa kutumia Mguu wake, James alikua akiona kila kitu, baada ya kumaliza akaangaza tena huku na kule kisha haraka akageuka na kurudi alipotoka, akampita James bila kumwona kisha akaelekea Kwenye maegesho lakini wakati anatoka hapo akaliona gari la James ndipo akapata uhakika zaidi kua Patra yupo hapo Hospitalini, akatabasamu kisha akampigia simu Babu yake na kumwambia kua ameshamaliza, kweli Babu yake alipoangalia tena alimwona Patra kisha akacheka na kutengeneza bomu kwa ajili ya kummaliza Patra
James akafikiria sana ni kitu gani ambacho Neema alikiweka pale, hakutaka kukipa uzito sana badala yake akarudi nyuma kisha akaelekea ilipo wodi ambayo Patra amelazwa, kumbuka ndani ya wodi hiyo alikuwepo Mama yake Mzazi
Basi James akasogea hadi mlangoni, Patra alilazwa katika wodi ambayo ilikua ya hadhi kubwa sana, kitendo cha kufika tu mlangoni alifanikiwa kumwona Mama yake Mzazi akiwa anazungumza na Mchungaji, alimwona kupitia kioo cha hapo Mlangoni, akashtuka sana, Mara akashikwa bega
Akageuka na kukutana na Daktari ambaye alikua amezungumza naye na kumwambia kua kwa lolote litakalo hitajika basi amweleze, na ndiye aliyekua akimweleza kuhusu hali ya Mtoto
“Oooh Mr. James….Karibu sana” Alisema Daktari kisha akampa mkono James ambaye alikua katika butwaa zito sana
“Ndiyo unakuja au unaondoka?” akauliza Daktari huyo, Bado James alikua kwenye Butwaa maana hakutegemea kumwona Mama yake pale Wodini.
“Nili….kua…Naondoka” Akasema James kwa kujiuma uma
“Basi sawa, namshukuru Sana Mungu hali ndiyo kama ulivyoiyona, Mtoto anaendelea vizuri kwasasa” Akasema Dakatri kisha akafungua mlango na kuingia wodini, Haraka James akaondoka
“Mmemwona Mfadhili?” akauliza Daktari, wote wakashangaa “Mfadhili?” akauliza Mama yake James
“Ndiyo…..si alikua hapa kumwona Mtoto, ametoka sasa hivi nimepishana naye hapa Mlangoni”
“Hapana Dokta, Hakuna Mtu aliyefika hapa wodini tokea ulipotuacha” Akasema Mama yake James, ikampa Mshangao Dokta, akaelekea mlangoni kumwangalia James lakini hakufanikiwa kumwona tena
“Mbona nimekutana naye mlangoni akanambia kua ametoka hapa wodini, yeye amekua akichangia pesa za matibabu ya Mtoto” Alisema, kisha akatoa Kadi ya Biashara ambayo alipewa na James, akamwonesha Mama James, ndipo Mama James naye alipogundua kua James alikuja Hospitalini na bila shaka alimwona Mama yake, lakini kilichomshtua Mama James ni kusikia kua James anachangia matibabu ya Mtoto.
Muda huo tayari James alishaondoka Hospitalini, alikua Barabarani akiendesha gari yake kwa sapidi sana kuelekea nje ya Jiji ambako alimwacha Matilda, hakujua kua Matilda alishaondolewa. Alitumia masaa zaidi ya mawili hadi kufika, alipoingia ndani ya jumba hilo lililo msituni hakumwona Matilda pia hakukuta Mtu yeyote yule kitu ambacho kilianza kumchanganya. Akaingia tena kwenye gari na kurudi Mjini
Wakati huo Matilda akiwa bado anapiganisha akili anawezaje akatoroka hapo ili kunusuru Maisha yake, Walinzi walikua wakikagua chumba chake mara kwa mara kuhakikisha haondoki hapo kama ambavyo Neema alikua ameagiza, ilimpa wakati mgumu sana Matilda
Mama yake James aliporudi nyumbani kwake alihisi mwili ukipata moto, kwanza kujua tu kua James amshamwona pale Hospitalini kulimpa mashaka makubwa sana sababu hakutaka ajuwe chochote lakini kingine kilichomuwazisha zaidi ni pale aliposikia kua James alikua akitoa pesa za matibabu ya Mtoto, maana yake ni kwamba James alikua na mapenzi na Patra.
Siku iliyofuata mapema sana, taarifa mbaya ilianza kuenea kwenye simu, ilikua ni kuhusu hali ya Patra ambayo ilibadilika ghafla sana, tena ikidaiwa kua mapigo yake ya moyo yalikua yakishuka kwa kasi kitu ambacho kilikua kinaashiria kifo kwa Mtoto huyo, miongoni mwa waliotumiwa ujunbe huo alikua ni James, Mama yake James, Mama Naomi, Jack na Mchungaji George
Haraka wote wakafika Hospitalini isipokua James ambaye alikua akifikiria ni namna gani ataingia hapo kwa ajili ya kumwona Patra, ilionekana wazi kua Patra anaweza kutangazwa kua amefariki muda wowote, Mchungaji alijitahidi sana kufanya maombi lakini Mishale ya saa nne Asubuhi Patra alifariki Dunia, Daktari akathibitisha hilo
“Poleni sana, tumejitahidi kuokoa uhai wake lakini juhudi zetu zimegonga mwamba” Akasema Daktari huku akishuhudia mvua ya vilio, Mchungaji George akashindwa kuvumilia akakimbilia kulia nje kama Mwanaume, ilikua ni huzuni kwa kila aliyesikia. Mama James hakuona kama kulikua na sababu ya kuendelea kulificha hilo sababu alihitaji msiba ukafanyike nyumbani kwake, akampigia simu James na kumwambia kua anahitaji kuonana naye
Haraka James akaenda nyumbani kwa Mama yake, akamkuta Mama yake akiwa mwingi wa huzuni, akaketi kando ya Mama yake kabla ya kumuuliza kiunyonge kilichopelekea huzuni hiyo
“Amekufa” Alisema Mama yake James huku chozi likizidi kumvuja, James akashtuka sana, moja kwa moja akajua ni Patra lakini akajikaza huku akizidi kumuuliza Mama yake
“Nani huyo Mama”
“Mtoto wako, Kwanini ulifanya siri James, Mtoto ameteseka Mno hadi amefariki” Akasema Mama yake James huku akiangusha kilio, chozi likambubujika James, hakua na la kufanya, hakuweza kubeba ukatili wa kukana mbele ya Mama yake
“Kisa ulemavu James umegeuka kua Mnyama, Mama wa Mtoto hadi sasa hajulikani yupo wapi….James, hapana shaka upo nyuma ya hili jambo, nakuhakikishia kua Patra hatozikwa kama Mama yake Patra hatopatikana” Alisema Mama yake James, kila jambo lilikua tayari limefunguka, hapakua na siri tena. James akainamia chini
“Kama kuna siku nimeumia katika Maisha yangu James basi ni leo, James wewe ni katili sana Mwanangu, hustahili kuitwa Binadamu, Nenda kamlete Mama yake Patra hapa” Akasema kwa hasira Mama yake James, Basi James akawa kama Budi akasimama asijuwe aingilie wapi kumtafuta Matilda, akatoka huku chozi likiendelea kumbubujika, alipofika getini alipishana na gari iliyowabeba Mchungaji, Mama Naomi na Jack
Alipotoka hapo James akaelekea Baa, akaagiza pombe kali na kuinywa kama anakunywa maji, alihisi kufanya hivyo kungeondoa Mawazo yote, licha ya kua na pesa nyingi ambazo wengi huamini kua na pesa kunamaliza matatizo lakini upande wa James ilikua tofauti, pesa ndiyo iliyoleta matatizo kwake.
Giza liliingia huku James akiendelea kuagiza moja baridi, moja moto hadi akalewa kabisa na kushindwa kujitambua, akasaidiwa na baadhi ya waliomjua sababu alikua maarufu, akarudishwa nyumbani kwake.
Usiku huo tafrani ikawa nzito nyumbani kwa Mama James, Mchungaji aliomba Patra azikwe lakini Mama James aligomea kabisa akihitaji kwanza Matilda afike ili amshuhudie Binti yake, wakambembeleza sana lakini akagoma huku akiwaambia James atamleta Matilda sababu anajua ni wapi alipo na kama hatomleta basi Patra hatozikwa. Mama Naomi na Mchungaji wakatoka kwa ajili ya kuzungumza
“Huyu Mama anamaumivu makali sana, amemjua Mjukuu wake tu na Mjukuu amefariki, hali aliyonayo ni ngumu sana kuelewa chochote kile, cha Msingi kukipambazuka tumtafute James pengine anajua ni wapi alipo Matilda” Akasema Mchungaji, Asbuhi mapema sana wakampigia simu James, wakapanga waonane ili kuweka mambo sawa, James hakua na ujanja akawaelekeza mahali anapoishi, walipofika walikuta mazingira ya hovyo sana sbaabu wafanyakazi wote waliondolewa na Neema, aliyebakia alikua ni mlinzi tu ambaye alikua hafanyi usafi
“Kilichotuleta hapa ni kuhusu Matilda, Mama yako amekataa kumzika Mjukuu hadi pale Mama yake Patra atakapofika, James kama unapajua alipo Matilda tafadhali tuambie ili tumsitili yule Mtoto” Alsema Mchungaji, Mama Naomi akawa anafuta chozi lake
“Mchungaji kiukweli sijui mahali alipo Matilda,, Nimehangaika sana kumtafuta bila mafanikio yoyote yale, ilipofikia nimekata tamaa” Akasema James, hakutaka kabisa kusema kua Neema ndiye anayejua mahali alipo Matilda, sababu alihofia usalama wa Neema kwakua alikua Mjamzito
“Mbona Macho yako yanasema ukweli lakini mdomo wako unaongopa James, wewe ndiye ulimshtaki Matilda, akaenda polisi lakini akatoweka katika Mazingira tata, unajua alipo..” akadakia Mama yake Naomi kwa hasira sana
“Jamani ningekua najua alipo ningemleta lakini sijui alipo, nawaahidi nitaendelea kumtafuta” Akasema James huku akikuna nywele zake
Mchungaji akasimama na kusema
“Kumbuka kua Mtoto hatozikwa kama Matilda hatopatikana” Alisema kisha akaongoza nje, Mama Naomi akamwambia James
“Hadi kifo kinamchukua Mtoto ukiwa unaendelea kumkana, hakika wewe ni miongoni mwa matajiri wajinga sana Duniani” Alisema kisha naye akaondoka hapo, James hakua na jeuri tena sababu alikua katika nyakati ngumu sana
Walipoondoka Mchungaji na Mama Naomi, James akaingia kwenye gari yake, akampigia Jack kua asimamie majukumu ofisini kisha akawasha injini ya gari na kutimka hapo, kichwa chake kilijaa mkanganyiko, zilipita siku mbili bila kuzungumza na Neema, akili yake ikawa inawaza atafanya nini ikiwa Neema ndiye anayemshikilia Matilda.
Injini ya gari ikazima katika geti la Nyumba ya Neema, Mlinzi akatoka na kumwambia James kua hapaswi kuingia ndani
“Hivi unajua unamzuia Nani, Mimi ndiye niliyeinunua hii nyumba, hebu pisha” Akasema James kwa hasira, alihitaji kuzungumza na Neema
“Hii siyo amri yangu, nimeambiwa nikuzuie James” Akasema Mlinzi
“Bali ni amri ya Nani?” akahoji James, Mlinzi akachungulia ndani kisha akamwambia
“Neema”
“Neema? hebu nipishe..” Akasema James huku akijikuta akisukumana na Mlinzi pale getini mara gari ya Neema ikafika, Neema alikua ndani ya gari hiyo, hakutaka kushuka, James akasogea kisha akamwambia Neena
“Shuka nahitaji kuzungumza nawe” Licha ya James kusema kwa jazba lakini Neema hakutaka kutii amri hiyo, alishajua nini kimemleta James nyumbani kwake, James akafungua mlango na kumchomoa Neema
“Wewe vipi kwani kuna ulazima wa kuzungumza na Mimi?” akahoji kwa dharau Neema, James akampiga kibao Neema, ilikua ndiyo mara ya kwanza James anampiga Neema, wakati huo Mama yake Neema alikua ameshatoka ndani, akamsukuma James
“Wewe una Kichaa? unampiga ulimzaa wewe huyu?” akauliza Mama yake Neema huku akimtaka James ajibu
“Mama, Neema ananiletea dharau wakati nataka kuzungumza naye”
“Kwahiyo ukidharauliwa ndiyo umpige Mtu, adabu ya wapi hiyo wewe Kijana, hujui kama upo nyumbani kwa Neema, tena siyo tu kwa Neema bali Mimi nikiwepo alafu unampiga?” Neema akawa anajiliza
“Mama nataka kujua Matilda yupo wapi” Akauliza James
“Matilda, ndiyo Nani…si nakuuliza wewe huyo Matilda ni Nani?” akahoji Mama Neema
“Ni Mwanamke niliyezaa naye, Neema anajua yupo wapi!”
“Hivi wewe una utimamu wa akili, yaani Mwanamke uzae naye wewe alafu uje umtafute kwa Neema, Dunia itakushangaa kwa uzuzu wako, kama Matajiri wote Duniani wana akili kama yako basi kua na pesa siyo kua na heshima, alafu si ulisema huna Mtoto, leo unakubali kua una Mtoto tena umekuja kwa Neema kumtafuta Uliyezaa naye” Akasema Mama yake Neema, James akawa mpole na mwenye kunywea, Mama Neema akamshika mkono Neema kisha akaingia naye ndani
“Simtaki huyo Mtu, tafadhali muondoe” Mama Neema akatoa maagizo kwa Mlinzi. James akaingia kwenye gari kisha akaondoka, Baada ya kusikia kua James ameondoka…Neema akamwambia Mama yake kama si yeye aliyekua akijiliza
“Mama umemyoosha sana”
“Ndiyo dawa yake, mwache tu. Hawezi kufanya chochote kile sababu anajua una ujauzito wake, atakapo kuja kufunguka kiakili utakua umemaliza kila kitu, cha Msingi huyo Msichana Mshikilie hadi mwisho.”
“Asante Mama kwa ushauri wako unanisaidia mno”
“Nisipokusaidia wewe nimsaidie Nani tena”
“Nahitaji kujisaidia” Matilda alipaza sauti yake, mara kiatu kikasikika kikija chumba alichokua amefungiwa, kikafunguliwa, akaingia Mwanaume mmoja..
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya TISA Ya PIGO TAKATIFU Msisahau COMMENTS Ziwe Nyingi
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx Pigo Takatifu xx
11 Comments
Jamani, mbona inahuzunisha
Ni hataree
ℳumetisha xaba
Mtunzi upo vzr unajua kugusa hisia za watu
Alooooh🙌🙌
Tamu ial fupi sana jamani
😨😨😨😨
Upo vzur san
Daaah maskini akipata matako hulia mbwata mbwata mbwata 😗
Patra kufa cjapenda😪
Nimeipendq coz
inatufundisha sanaaa