Ilipoishia ” Nilimsimulia kila kitu cha siku ile tu lakini, sikugusia mambo ya nyuma.
βDu! Kwa hiyo mimi nikusaidieje?β
βNaomba tuingie wote ndani, nataka nikachukue simu yangu tu nimpigie huyo jamaa.β
βDa! Itakuwa ngumu kidogo, unajua mimi nina haraka sana leo,β alijitetea yule mtu ambaye kwa umbo ni bonge la mtu. Nilijua ni uoga tu, hakuwa na kuwahi wala kuchelewa “
Endelea SEHEMU YA NANE (08)
Alipopita, akatokea mwingine, mzee mmoja, kichwa chote kilichafuka kwa mvi. Nilimsalimia huku nikimwonesha ishara kwamba nataka kuzungumza naye.
βMzee samahani sana.β
βBila samahani kijana.β
Naye nikamsimulia tukio la siku ile,Β lakini wakati ananisikiliza, mara nilimwona anatupia macho dirishani na mimi nikageuka kuangalia, sikuona mtu.
βUmeona nini mzee wangu?β
βNimeona msichana ananizomea.β
βKweli?β
βEe. Ndiyo hayo mambo unayosema?β
βNdiyo hayo mzee.β
βTwende,β alisema, nikaanza kutangulia mbele, mzee akanifuatia kwa nyuma. Hatukuwa tukiongea chochote, najua sababu. Kila mmoja alikuwa anaiwaza hatari ya mbele.
Tuliingia ndani, tukafika sebuleni, lakini sikuiona simu kwenye kochi.
βOna sasa mzee, simu niliitupia hapa, lakini haipo.β
βAu unayo mfukoni kijana?β
βHapana, nina uhakika,β nilisema huku nikijipapasa mifukoni, hakukuwa na simu.
βNitajie namba nijaribu kuibipu,β yule mzee aliniambia huku akitoa simu yake mfukoni. Nilimtajia namba zote, akawa anaziandika, kisha akapiga huku simu akiwa ameiweka kwenye sikio lake la kulia. Nilishtuka sanaΒ kusikia simu yangu inaita kutokea kwenye chumba cha wale wapangaji wenzangu.
βSi hiyo?β yule mzee aliniambia akiniangalia kwa mshangao.
Mzee alikata kisha akapiga tena, ikaita tena kutokea kulekule, nilizidi kuogopa, nikamwambia tutoke lakini uzee kweli dawa, aliniambia hakuna haja ya kutoka dawa ni kupambana tu.
Alinisogelea na kuniambia kwa sauti ya chini:
βNiwagongee mlango?β
βSi watakasirika?β
βSasa kama unaogopa watakasirika, unadhani simu yako utaipataje?β
βHaya wagongee. Lakini subiri, kwa nini tusiende kwanza chumbani tukajua nani alikuwa anachungulia nje?β
βKijana unaonekana muogamuoga sana, we mwanaume bwana, jifunze kukabiliana na hali kama hii, sawa?β
βSawa mzee.β
βHaya twende huko chumbani kwako unakotaka tukaone huyo msichana.β
Tulifungua mlango wa chumbani, hakukuwa na mtu, ila shuka nililoliacha kitandani asubuhi silo, lilitandikwa jingine pia la kwangu.
βKhaa!β nilishangaa.
βNini?β
βHili shuka.β
βLimefanyaje?β
βSilo nililolitandika asubuhi.β
βLakini la kwako?β
βNdiyo langu.β
Niliangalia mazingira mengine ya mle ndani na kubaini kwamba, kuna vitu vingi sana vilikuwa ndivyo sivyo.
βSi umeona hayupo?β yule mzee aliniuliza, nikamjibu ndiyo, akasema twende tukachukue simu yetu kwenye kile chumba ambacho ilikuwa inaita.
Moyo wangu ulikuwa mzito sana, nilihisi kizunguzungu, nilitamani kukaa chini na kumwomba yule mzee asichukue uamuzi wa kuifuata ile simu, lakini ningeipataje simu yangu wakati ina namba kibao?
βKijana, ngoja nikuoneshe dawa moja ya hao viumbe wasiotaka kuonekana,β alisema yule mzee, nikamuuliza ni ipi hiyo.
βTulia wewe,β alisema huku akiingiza mkono mfukoni na kutoa kimfuko kidogo, akakifungua akatoa kitu. Nilipomuuliza ni nini akajibu:
βNi bangi.β
βSawa kabisa, hiyo ndiyo dawa, ngoja nikupe kiberiti.β
Katika mambo yaliyonishangaza ni hilo, tulitafuta kiberiti chumbani hadi sebuleni lakini hakikuonekana, mbaya zaidi mimi nilikuwa na kawaida ya kununua viberiti bunda zima, lakini pia sikuona popote.
βKweli una kiberiti ndani?β yule mzee aliniuliza.
βKiberiti kipo na uzuri ni kwamba, nina bunda zima, pia silioni.β
Nilimwona yule mzee akisimama wima na kunyoosha mikono juu kama mtu anayeomba dua kwa Mungu.
βKijana nimejua sasa, ngoja kidogo,β alisema huku akitoka na mimi nikimfuata kwa nyuma.
Wakati tunapita kwenye korido jirani na vyumba vile vya wenzangu, nikaisikia simu yangu ikiita.
βMzee mzee, hiyo bwana,β nilisema, mzee akasimama na mimi nikasimama nyuma yake, tukasikia sauti ya mwanaume ikipokea simu yangu:
βHalooβ¦Jumaβ¦Juma gani wewe? Nakuuliza Juma gani maana mimi ndiyo mwenye simu hii, huyo unayemsema simjui na wala hajawahi kumiliki simu hii,β sauti ya kiume ilisema, ukapita ukimya kidogo kisha sauti hiyohiyo ikasema:
βKama unabisha siyo simu yangu ongea na mke wangu huyu hapa.β
Mara nikasikia:
βHalooβ¦ni kwa nini mnapenda sana kumfuatafuata mume wangu, mara mzungumzie bangi, mara mtusemee kwa watu.β
Nilitamani sana kumwambia asiniache katika safari yake maana kwangu kwa muda ule palishaharibika, ningeuawa na watu wasioonekana.
βWewe nisubiri kijana,β mzee aliniambia akiendelea kwenda nje sikukubali.
βMzee humu ndani mimi sikai, nimeshajua sasa.β
βUmejua nini?β
βHuyo Juma anayetajwa hapo nafanya naye kazi na ilikuwa aje na bangi kwa ajili ya hawahawa watu wa humu ndani.β
Mzee aliniangalia, akaniuliza:
βWewe kijana unaye Mungu?β
βNinaye.β
βHuwa unakwenda kusali?β
βSana.β
βLini umekwenda mara ya mwisho?β
βUngeniambia tatizo ni kusali au?β
βSi hilo tu, ila una matatizo mengi. Hivi hapa tumesimama, nyuma yako nimemuona yule msichana amekuinamia akikungβongβa kama mara tatu kwa harakaharaka.β
Nilitimua mbio kuelekea kusikojulikana, nikaenda kufunga breki kwenye mtaa mmoja ambao ukienda kushoto kwangu unakwenda kutokea kwenye barabara ya kwenda Kigogo Mbuyuni.
Baadhi ya watu walioniona nilivyo walitambua nina tatizo zito kichwani, mzee mmoja aliniuliza kama nakimbizwa nimefumaniwa.
βSijafumaniwa mzee, lakini kwa tatizo langu afadhali ningefumaniwa.β
Huyu mzee alikuwa amebeba kibegi kidogo mgongoni, alivaa suti nyeusi huku akionekana ni mzee mwenye heshima kubwa katika jamii inayomzunguka.
βTatizo nini, hebu nisimulie kidogo tu,β alisema huku akinivutia pembeni. Nilimsimulia kila kitu, alichokuwa akinishangaza sasa, kila hatua ya maelezo yangu alikuwa akiachia tabasamu hata pale nilipoamini kwamba ninachokisema kwa wakati huo asingetabasamu na uso wake ungeonesha kushtuka.
Nilipomaliza nikanyamaza na kumwangalia kwa woga, nilitaka kuamini ni yule mwanaume aliyepokea simu yangu kule nyumbani amenibadilikia ili nisiweze kumtambua.
Moyoni nilisema kuwa, kama kweli ni yeye atakapojidhihirishaΒ tu kwangu nitoke mbio na kwenda kuingia kwenye nyumba ya mtu yeyote mbele yangu.
βTatizo ni hilo dogo tu?β aliniuliza.
βNi hilo tu mzee wangu. Ukiweza kunisaidia nitashukuru sana.β
βNyumba yenyewe iko wapi?β
βKule nyuma nyuma.β
Nilimwona akiingiza mkono mfukoni na kuchomoa simu nyeusi ndogo, wengi wanaziita za tochi kisha akabonyezabonyeza na kuiweka sikioni. Moyoni nilisema yaleyale.
βSi ajabu anawasiliana na yule mwanamke wa kule nyumbani.β
Β Nikamsikia akiuliza:
βIsdory, bado mpo hapo?β
Nadhani huyo jamaa alisema yupoyupo maana nilimsikia huyo mzee akisema: βUnaweza kuja na akina Tino hapa kwenye kibanda tulichotuma pesa asubuhi ya leo? Haya njooni.β
Niligeuzageuza kichwa na kukiona kibanda cha kutuma pesa kwa kupitia mitandao mbalimbali ya simu. Nikajua amewaita watu waje pale.
Baada ya dakika kama tatu, wakafika watu kama saba, wanne wanawake, watatu wanaume akiwemo Isdory na Tino.
βHuyu bwana anaitwa,β alianza kusema yule mzee akiniangalia nikajua anataka nijitambulishe jina mimi mwenyewe, nikafanya hivyo. Nilipomaliza, ndipo yule mzee akawaambia wenzake kisa chote cha kwangu, mwanzo hadi mwisho kama nilivyomsimulia awali.
βNdugu, sisi wote walokole, kazi hiyo tunaimudu kwa vile mara nyingi huwa tunatumia jina la Bwana na Mwokozi wetu kufukuza uchafu kama huo, sasa itabidi utupeleke kwenye hiyo nyumba,β alisema yule mzee.
Nilianza kutembea mimi na wao wakawa wananifuata kwa nyuma. Wale wanawake niliwasikia wakizungumzia mwanamke mmoja aliyeangushwa chini na mapepo akawa anataka kupigana na wale waliokuwa wakimwombea. Moyoni nikasema:
βLeo huko sijui.β
Tulifika nje ya nyumba, kitendo cha kwanza ambacho si cha kawaida, nilimwona yule kijana muuza maji akitoka ndani. Alivaa kama siku alivyokuja nikamwingiza ndani.β
Nilishtuka sana, yeye hakushtuka, ila aliponiona akaniambia:
βBro nashukuru sana wamenilipa pesa zangu.β
Sijui ni nini kilinipata nilijikuta nikisema sawa, sikuongeza neno jingine lolote lile.
βNi humu waheshimiwa,β niliwakaribisha wale watu nikiwa nimeshapishana na yule kijana.
Waliingia wote ndani, wakasimama katikati ya korido kisha wakawa wananiangalia, yule akaniuliza:
βHivyo vyumba ni vipi?β
Sikumjibu kwa sauti, nilinyoosha mkono kuelekea kwenye vyumba vyote viwili. Vilioneshwa kufungwa kwa ndani lakini hakukuwa na sauti ya muziki wala maongezi yao.
βBaba katika jina la Yesu,β yule mzee alianza ghafla.
βAmiiiin,β walijibu wote aliofuatana nao, tena walijibu kwa sauti ya juu kisha wakatulia kimya.
Akaanza kusali akitaja maneno ya kutisha, nilimsikia akisema, choma moto roho mtakatifu, mara Malaika Michael shuka na panga likatalo kuwili.
Kifupi yule mzee alisema maneno ya ki-Mungu kwa jinsi nilivyoelewa mimi. Ikafika mahali akasema:
βPaaza sauti yako.β
Ndipo wengine nao wakapokea kwa kila mmoja kuomba kivyake. Wengine walisikika wakisema wanaangusha na kuvunja ngome za ibilisi, wengine wanachoma moto makazi ya shetani, wengine wanamwagia damu ya Yesu pale ndani. Nilianza kuhisi amani iliyoje, niliamini ukombozi umefika tayari kwani sauti tu niliisikia ikipenya hadi kwenye mbavu zangu.
Waliomba sana, kuna wakati mimi nilihisi kuchoka lakini wao waliendelea tu hadi moyoni nikasema kweli ni watu wa Mungu.
Ghafla nilianza kuona moshi mweusi ukitoka chini ya milango yote ya wale ndugu, mlango wa sebuleni kama sikikosei na mlango wa chumbani. Moshi ulikuwa mzito kiasi kwamba, kuna wakati nilihisi kupaliwa na kukohoa kwa nguvu lakini wao hawakuonesha dalili ya kusumbuliwa na moshi huo. Nini Kiliendelea? Usikose sehemu ya 09
Tafadhali Unapomaliza Kusoma Acha Na Comment Yako Hapo Chini
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
Una Enjoy Nyumba Ya Majini? Mtumie ADMIN Ahsante
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMΒ
Wewe Ni Mwandishi? Unapenda kuendeleza Taaluma yako ya uchambuzi kwenye masuala ya michezo? Mtandao wa uchambuzi wa michezoΒ kijiweni.co.tzΒ unakupa uwanja wa kuendeleza kipaji chako na kufikia maelfu ya wapenzi wa michezo Tanzania na nje ya Tanzania.
Tutumie makala au uchambuzi wa michezo katika barua pepe hiiΒ editor@kijiweni.co.tzΒ Β
29 Comments
Dooh atatoboa tu
Admin tuma nyingne kesho asubuiiiiiii
Hii ipo safii admin
sio powa kutoka kwenye bangi paka maombi
Hadithi inatosha sana na pole sana mtu wa mungu
Adimin kitu ni cha moto sana
Hongera
Jina la Yesu ni tiba ya kila jambo
Hao watu wa roho mtakatifu nao wameyatimba yani apo hatoki mtu
Atatoboa kweli??
Daaah! Kama ni ukweli basi dunia kweli ina mambo! Sema admin unazingua π weka hata mbilimbili kila siku aisee..
Washampiga sana kizinga sasa wameyatimbaπ€£π€£π€£π€£π€£π€£ sema ninaogipa hadi kuamka prepo kusoma kisa adith
Admin upewe ninileo ili utowe muendelezoπ π π
Naimani hii ni true storyπ₯Ί
Watu wameanza kuungua tayari
Admin achia nyingine usiku huuπ₯π₯π₯
Yaan naogopa kutoka njeπππππ
Admin unatutumia usiku ili na sisi wengine ni waoga, ah admin punguzaa sisi wengine tupo peke yetu, mimi naeka kiporo bana
Mungu mwema let’s go another episode π
Kumekucha
Mtunzi nimekuelewa zaidi unapo ikwepa bangi katika kutumiwa big na haijatumika police pia walimpa onyo kali kuhusu bangi unafundisha pia licha tu kua ni story yakuchangamsha ubongoπ
Dah simulizi tamu sana
You are incredible things
Nataman ingetengenezewa movie natumain ingeuza zaid hap nchini na hata nje ya nchi
πͺππππni nin lkn mie adii naogopa ahahaha siwaamini wapangaji wenzangu ani baada ya kusoma hii story naota otaπ€£π€£… yaaniii nkiamka asubuh nawaangalia wapangaji wenzangu mara mbili mbili
duuuh! yaan nguvu ya kurudi sijui ningetolea wap???
n zaidi ya maono ya kidunia
πππ m nikajua labda akifika pale atakosa zile nyumba (atakuta nyumba hazipo) π€£π€£π€£ ila admini ww upo kama LAMATA yaan unatoka nje ya fikra zetu kabisa π π π tunaomba uachie mwendelezo mapema sana.
Duh!atatoboa kweli
π Hallelujah
Hii imekaa vzr Sana π₯π