“A Good dancer must know when to Leave a Stage. // 𝑀𝑡𝑢𝑚𝑏𝑢𝑖𝑧𝑎𝑗𝑖 𝑚𝑧𝑢𝑟𝑖 𝑎𝑛𝑎𝑡𝑎𝑘𝑖𝑤𝑎 𝑘𝑢𝑗𝑢𝑎 𝑛𝑖 𝑤𝑎𝑘𝑎𝑡𝑖 𝑔𝑎𝑛𝑖 𝑤𝑎 𝑘𝑢𝑜𝑛𝑑𝑜𝑘a 𝐽𝑢𝑘𝑤𝑎𝑎𝑛𝑖..
Ni Maneno ya hekima kutoka katika kinywa cha Patrick Loch Otieno Lumumba.”
Ni maneno machache sana aliyoandika Ali Kamwe kuhudhihirishia uma kuwa anaachia nafasi yake pale kwenye Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga SC, lakini mpaka sasa siamini kwamba ndiyo anaondoka na hatokuwa Msemaji wa klabu hiyo hapa nchini kwa msimu ujao 2024/2025.
Amehudumu tu kwa miaka miwili kwenye kiti hicho alichoaminiwa na viongozi wa Yanga SC kupeleka Taarifa ya klabu yao pendwa kwa uma wa watanzania 60M+, bado siamini kuwa Kamwe ni kweli ameondoka Yanga SC labda niko usingizini ni kilichoandikwa siyo cha kweli, labda niko sahihi kufikiria hivyo lakini bado napata ukakasi kurudi kwake maana hata kwenye wasifu wake kwenye akaunti yake ya Instagram amefuta kuwa siyo Msemaji tena.
Labda kwanza nikupitishe kidogo huku kisha nitarejea kwa kijana mwenzetu, Tasnia ya habari kwa vilabu hususa mpira wa miguu nchini ilianza 2000, lakini mwaka 2015 umaarufu wa neno Msemaji wa klabu ulianza kukua na hapo ndiyo vilabu mbalimbali kadri miaka inaenda navyo vikaanza kuajiri na kuwekea mkazo eneo ilo haikuwa rahisi lakini lilifanikiwa pakubwa sana tena kwa kasi.
Nikurejeshe tena kwa Ali Kamwe, wengi hawakuamini kuwa kama angetangazwa kuwa Msemaji mpya wa Yanga SC, na hata alipotangazwa wapenzi wa neno Soka waliumizwa sana na uamuzi huo wakiamini kuwa klabu hiyo ilimchukua mtu muhimu sana kwenye upande wa uchambuzi wa michezo na nchi ilizizima kwa utambulisho huo, ni dhahiri haikuwa rahisi ila ilipaswa kukubalika na kuwa hivyo ndivyo ilivyo na inapaswa kuwa hivyo.
Taratibu ikazoeleka na Kamwe akatolewa kuitwa Mchambuzi hadi Msemaji wa klabu kubwa nchini na kadri muda unaenda akabatizwa majina mpya ikiwemo Mwenyekiti wa Wasemaji.
Inaweza ikawa ngumu kukubaliana naye kwa maamuzi hayo ila Wacha nikupitishe kwenye mambo aliyoyafanikisha akiwa Yanga SC.
Ali Kamwe ndiyo Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu nchini ambaye amefanikiwa sana MOJA NI , eneo la kimtandao, wakati anatangazwa klabu pekee iliyokuwa kubwa mtandaoni ni Simba SC ila utambulisho wake ukawa ndiyo mwanzo wa kuhidhohofisha Simba Mtandaoni kuanzia Instagram, Facebook na Youtube.
Ukiongelea sasa klabu yenye wafuasi wengi YouTube basi ni haraka sana utaitaja Yanga SC, aliingia klabu ya Yanga ikawa na wafuasi (Subscribe) chini ya 180,000 ila mpaka sasa anatangaza kuondoka ina wafuasi 636K.
PILI NI, ubora wa kimaudhuii klabu ya Yanga SC ndiyo klabu kwa sasa yenye maudhui bora sana mtandaoni hususa kwenye picha mjongeo “Video” namna yanavyozalishwa kwa sasa kila klabu inatamani iwe hivyo kwa upande wake picha na video zenye ubora na kuvutia.
TATU NI, kuwa klabu ya Kwanza kupitia Idara yao ya Habari kuandaa “Documentary” inayozungumzia mafanikio makubwa ya klabu hiyo kwa msimu mzima ikielezea historia na Kumbukumbu mbaya na nzuri zilizotokea kwa msimu husika.
NNE NI, kuifanya Idara ya habari kuwa kitengo muhimu ambacho kinahitajika kufanyiwa kazi na watu wengi na siyo mtu mmoja au wawili. Ali Kamwe alituonyesha kuwa Idara hiyo inapaswa kuwa na wafanyakazi wa kutosha na ilo lilipeleka uzalishaji wa maudhui yenye ubora na mpangilio mzuri, kwani kila kitengo alikifanya kuwa na mtu wake aliyebobea Mfano eneo la picha na video ina vijana walibobea kwenye eneo ilo, picha, uendeshaji wa akaunti pamoja na utengenezaji wa picha mjongeo.
TANO NI, kuwapa nafasi vijana wenzake kuonyesha uwezo wao na hata wale waliyokuwa tayari wameonyesha uwezo wao basi aliwavuta upande wao kuendelea kuboresha idara hiyo, ikumbukwe kuwa alivyoingia tu alimuongeza Alwatani Abdulaziz Kisha wengine akiwemo Muvibe na wengineo.
SITA NI, kuifanya Idara ya Habari kuonekana ni Idara muhimu kwenye klabu ambayo inapaswa nayo kuwa Chanzo cha mapato kwa klabu hiyo kwani kupitia Idara hiyo klabu imenufaika na kuingiza pesa nyingi kupitia Mitandao yao ya Kijamii, kutengeneza Fedha kupitia Documentary pamoja na uandaaji wa Kumbukumbu bora ya klabu hiyo tokea imeanzishwa kupitia kitabu cha historia ya Yanga SC ambacho nacho kimeiingizia hela klabu hiyo.
Mwisho, ni pongezi zangu kwake kwani yeye ndiyo Afisa Habari pekee aliyefanikiwa kuibadilisha Idara hiyo na kuwa ni sehemu ya hamasa ya mafanikio kwa wapenzi wa Soka na mashabiki wa klabu hiyo, ila ikumbuke kuwa umeacha Kumbukumbu bora sana ndani ya Yanga SC utakumbukwa daima.
Ombi langu kwako ni moja tu usituache kama ambavyo uliamua kuondoka kwenye uchambuzi na kuingia kwenye klabu basi hivyo hivyo urudi kwenye uchambuzi tuendelee kufaidi ubora wako kwenye kiwanda hiki cha Michezo hususa Soka, kila la heri Mpare wa Moshi Kilimanjaro.
SOMA ZAIDI: Chama Clatous Na Kumbukizi Ya Kurasa Za Ajibu
8 Comments
Ni kweli inasikitisha Ally Kamwe kuondoka katika idara yake ila kiukweli ukiangalia haikuwa nafasi yake alichukua kutoka kwa manara kutokana na mambo ambayo yalijitokeza
huyu aliyeandika hivi Hana kazi ya kufanya au analipwa na yanga maani sioni cha maana hapa
Proud of him🤝 despite of being simba follower, respect much ally
Kwann wazeee kustafu n wagumu
N mda wa vijan bn ye aka promote nguo za gms bas
Kameogopa kufa 8/8 tu akoo hakana jipyaaa etyi mtumbuizaj bora hujua mada sahihi wa kuondoka jukwaani despite amefanya makubwa ila kashaona motooooo ulioko ubaya ubwelaaaa
Ally kamwe atabaki kuwa MTU muhimu sana kwenye mafanikio ya young African kwenye upande wa habar
Karibu msimbazi kaka tunajua ulienda huko kwa sababu TU ya maslah
Karbu unyamani 🦁🦁🦁🦁
Pingback: Hiki Ndio Kipindi Ambacho Afrika Inaiogopa Simba Na Yanga