Ilipoishia βSijapata kumwona Mwanadamu Mbishi na Mgumu kama huyuβ aliutupa mkono wakeΒ uliojaa damu kwa hasira sana kisha akarudi kuketi kitini akitafakari ni namna gani afanye iliΒ apate taarifa nyeti. Haraka akanyanyuka kutoka kitini kwa hasira akamfwata tena Elizabeth,Β akamwambia
βUkiendelea kuwa jeuri utamfuata Rais alipoβ alisema kisha akaondoka ndani ya chumbaΒ hicho, haraka Elizabeth akatambua fika kua Rais alikua ameshauawa na kilichokua kinaendaΒ kufanyika ni Uasi mkubwa wa kuitawala Nchi.Β
Elizabeth akiwa ananingβinia akaukumbuka Usiku wa Heka Heka. EndeleaΒ
SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO
MSATA. SAA TANO USIKUΒ
Elizabeth alifika Msata akiwa amebadilisha mwonekano wake kama Msichana mwenyeΒ mambo mengi mjini, aliweka kope Bandia, akaweka kucha, alivalia gauni fupi lenye mgβao,Β juu aliweka Wigi fupi ambalo lilimfanya aonekana kama siyo yeye, eneo ambalo alielekezwaΒ na Zagamba wakakabidhiane Nyaraka M21 lilikua ni Msituni.Β
Akaiweka gari kando ya Barabara kisha taratibu akaingia Msituni, Hapo aliambiwa kuaΒ atakutana na Mtu wa Zagamba aliyepewa kazi ya kupeleka Nyaraka kwa Zagamba, alipoanzaΒ kukaribia aliona tochi, akajua ndiye anayepaswa kuonana naye hapo. Akaiweka sawa BastolaΒ yake ndogo aliyoitoa kutoka kwenye mkoba wakeΒ
Akatembea taratibu tena kwa tahadhari kubwa sana, hakutaka kumwamini yeyote. MkononiΒ alivalia kifaa chenye GPS ambayo ilikuwa inamwezesha Muhonzi kuona mitembeo yaΒ Elizabeth na kujua yupo wapi. Alipofika hapo alikutana na mwanaume mmoja aliyevalia kotiΒ jeusi, ndani zaidi ya Msitu mzito wenye kiza kizito kisicho na nuru kabisaΒ
Chini ya Mti mmoja ndipo alipokuwepo Mtu huyo.Β
βUna mzigo?β aliuliza Mwanaume huyo, Elizabeth akamjibu kwa umakini βSiwezi kukupa mzigo bila kuona namna utakavyonipa pesaβΒ Β
βBinti, Bilioni 30 ni ngumu sana kutembea nazo hata kama zipo kwemye mfumo wa Dola.Β Nimeziacha ndani ya gari, naomba nione hizo nyaraka kwanza ndipo nikupe pesa yakoβΒ Mazungumzo haya yalikua Mubashara kwa Muhonzi.Β
Elizabeth akatoa Flashi akampatia Mwanaume huyo asiye mfahamu, kisha Mwanaume yuleΒ akawasha kifaa chenye mfanano na Kompyuta Mpakato akaiingiza Flash na kuhakiki, akatoa tabasamu la kuchanua ambalo lilimpa ishara Elizabeth kua Mtu huyo hakua na lengo zuriΒ kwake, hakuishia hapo aliangusha kicheko.Β
Haraka Elizabeth akaichomoa Flash kutoka kwenye kompyta kisha akamnyooshea BastolaΒ Mwanaume huyo.Β
βPesa nikupe Nyarakaβ alisema, mkononi alikua na tocho ndogo lakini alipommulika vizuriΒ alimwona Mwanaume huyo akiwa na mavazi ya Usalama wa Taifa, akajua wazi kua alikuaΒ ameingia Mtegoni.Β
βOooh taratibu Elizabeth, pesa yako ipo ndani ya gari. Ok, ongozana na Mimiβ alisemaΒ Mwanaume huyo, Elizabeth akaongeza umakini wa kutosha baada ya kugundua hapo MsituniΒ hapakua eneo salama kwake.
Akayaangaza macho yake kama Paka mwizi, kisha akamsukuma mbele yule Mwanaume iliΒ amtumie kama chambo cha yeye kutoka pale Msituni, akilini mwake alishaiuwa Biashara yaΒ Nyaraka zile za siri baada ya kuona dalili za uwepo wa hatari. Hatua za yule MwanaumeΒ zilikua za mahesabu makali sana, Elizabeth alishaligundua hilo sababu alikua JasusiΒ
Sauti ya Muhonzi ikasikika Masikioni mwa Elizabeth, ikamwambiaΒ
βNaona uwepo wa Watu zaidi ya Mmoja hapo Msituni, haraka Ondokaβ alisema kishaΒ Elizabeth akajibu kwa Ukimya huku sauti za Majani makavu yaliyokanywagwa zikiendeleaΒ kusikika. Moyo wa Elizabeth ukaanza Riadha ya haraka, nywele zikamsisimka vya kutoshaΒ huku vipele vidogo vidogo vya Tahadhali vikianza kumtoka.Β
Hatua ya sita ya yule Mwanaume ilimfanya Elizabeth ashuhudie teke kali likimuelekea,Β kwakua tayari alishaanza kuzihesabu hatua za yule Mwanaume na kujua hatua hizoΒ alilikwepa teke kwa haraka huku akiukunja mgongo wake kuelekea mbele, aliporudiΒ alikutana na kipande cha mti kilichotua eneo la tumbo na kumjeruhi.Β
βMshenzi unafanya nini?β aliuliza Elizabeth, hapo akajua fika kua taarifa za yeye kua ndaniΒ ya Msitu zilishauzwa muda mrefu hivyo kituo kinachofwata ni kukamatwa na kuuawa kikatiliΒ na Wanaume hao wenye sare za Ikulu, kwa haraka akili yake haikuchekecha vyema na kujuaΒ ni Nani aliyeuza mpango huo, akajikaza ili atoke ndani ya Msitu.Β
Bastola ilikua imeshamtoka, kutokana na giza zito hakufanikiwa kuiyona mahali ilipoΒ dondokea, mkononi alikua na Flashi yenye nyaraka, akaisweka haraka ndani ya chupi naΒ kuifunga kwa zipu kisha akajiweka sawa kukabiliana na Mwanaume huyo aliyekua na tamboΒ za kutosha kua angemmaliza Elizabeth hapo Msituni.Β
Tochi ilikua pembeni, Elizabeth alipoutoa mkono tumboni alihisi uwepo wa damu MbichiΒ yenye harufu, ikampa hasira, akamvaa Mwanaume yule mwenye ngumi nzito.Β
Akashusha mvua ya ngumi nyepesi alizolenga sehemu moja, kisha akaachia pigo zito kwaΒ kutumia skuna yake iliyomtoboa yule Mwanaume eneo la shavu. Akatema damu hukuΒ akigugumia kisha akapiga filimbi ya kuita Watu wengine walio pale Msituni, dakika moja tuΒ alishajua kupambana na Elizabeth isingelikua kazi rahisi kuifanya.Β Β
Tochi zikaanza kutapakaa pale Msituni, Elizabeth akamshushia na teke takatifu lililomlazaΒ yule Mwanaume kisha akaanza kukimbia ili kuokoa Maisha yake huku akivuja damu, eneoΒ ambalo alikatisha lilikua na Miiba ya kutosha iliyomkwangua kila eneo la mwili wake naΒ kumchania nguo.Β
Alikatiza ndani ya Msitu wenye giza nene huku akijua fika kua hapakua na Umbali mrefuΒ kutoka hapo kuelekea Barabarani alipoacha gari yake, lakini haikua rahisi kufika Barabarani,Β ilimtaka atumie nguvu zake zilizoanza kumsaliti. Alikimbia huku akifukuzwa na WanaumeΒ kadhaa wenye tochiΒ
La haula!Β
Akafika Barabarani lakini hapakua na gari yoyote, eneo ambalo alitokea halikua lile eneoΒ aliloingilia, akaanza kuifukuza ile Barabara asijuwe anasonga mbele au anarudi nyuma, gizaΒ
lilikua la kutosha na hapakua na dalili ya kutokea kwa gari au Pikipiki, akamwambiaΒ MuhonziΒ
βSijui kama nitachomoka salama Muhonzi, hali yangu siyo nzuriβ akasema kisha akakitupaΒ kifaa chake cha Mawasiliano, Bahati nzuri akamulikwa na taa ya gari kutokea nyuma yake,Β akasimama na kupungia mkono gari isimame.Β Β
Ndani ya gari alikuwamo Benjamin Kingai, rubani wa Shirika la Air Tanzania aliyekuaΒ akitokea Arusha kwa Mpenzi wake, gari iliposimama akafungua mlango na kuingia harakaΒ kisha akamwambia yule dereva kuaΒ
βOndoa gari Harakaβ Benjamin akiwa mwenye taharuki akawaona wanaume wenye SilahaΒ wakitokea Msituni, haraka akaliondoa gari bila kuuliza swali lolote.Β
**Β
Ndani ya Ikulu. Saa 9 Alhasiri.Β
Waziri Mkuu Haji Babi, alielekea eneo la siri ambalo Rais alikua akitesa na kuuwa WatesiΒ wake, akaingia kwenye moja ya chumba ambacho alikuwamo Mke wa Rais Lucas Mbelewa,Β hakutaka kutangaza kifo cha Rais Bila kupatikana kwa Nyaraka za siri ambazo zilikuaΒ mikononi mwa Elizabeth.Β
Alipofika alimkuta Mke wa Rais akiwa ameketi sakafuni, Haji Babi akasogea naΒ kuchuchumaa mbele ya Mke wa Rais kisha akamwambiaΒ
βMasaa machache yajayo nitatangazwa kua Rais wa Nchi hii, hakuna Mtu wa karibu waΒ Lucas atakayebaki kua hai. Una nafasi moja ya kuishi, nieleze unafahamu nini kuhusuΒ Nyaraka M21?β alihoji Haji Babi akiwa amekaza macho yake kuelekea alipo Mke wa Rais. Hofu ya Haji Babi ni kua Nyaraka hizo zina siri zake pia kwani viongozi wengi wa ngazi zaΒ juu walikua kwenye nyaraka hizo.Β
Mke wa Rais alikua kimya huku akilini akijiuliza ni jambo gani lililomfika Rais, akiwa katikaΒ tafakari akanyanyuliwa na kupelekwa kwenye chumba kingine ambacho kilikua na jokofu laΒ kuhifadhia Maiti, humo ndimo mwili wa Rais Lucas ulikuwa umehifadhiwa.Β
Mke wa Rais akawa anatetemeka, ujanja wote akautia mfukono, waziri Mkuu Haji BabiΒ alionesha wazi kua alikua siyo Mtu mzuri, japo Mke wa Rais alihitaji Rais atoke madarakaniΒ lakini hakutegemea kama angetolewa kwa njia hiyo ya Uwasi, jokofu lilipofunuliwa akaambiwaΒ
βNenda kaangalie kuna nini ndani yakeβ alisema Waziri Mkuu, kisha akatoa tabasamu panaΒ huku akisigina kiatu chake sakafuni, Mke wa Rais akasogea hadi kwenye jokofu, aliiyonaΒ maiti ya Rais. Mwili huo ulikua na matundu ya Risasi, alijikuta akiishiwa nguvu, WaziriΒ mkuu akamdakaΒ
βSasa unapaswa kua upande wangu Mke wa Rais, nitayafungulia Maisha yako yaliyokuaΒ yamefungwa na Lucas, nyota yako itawaka tena kwenye Siasaβ akasema Waziri Mkuu hukuΒ akiwa anamwonesha tabasamu pana sana, alionekana kujua siri nyingi za Maisha yaΒ Marehemu Rais Mbelwa na Mke wake.
Akaagiza Mke wa Rais awekwe kwenye chumba kingine kwa uangalizi mkubwa, akawekwaΒ kwenye chumba kizuri ambacho alipewa kila kitu isipokua simu, Mpango wa Waziri MkuuΒ ukawa ni kutaka kuitawala Nchi, aliporudi ndani ya Ofisi ya Rais akampigia Simu MuuwajiΒ wake wa kuaminika, akamtaka awasili hapo Ikulu jioni hiyo ili ampe kazi ya kusafisha woteΒ anaowahisi watakua kikwazo kwenye Utawala wake.Β
**Β
Hatma!!Β
Baada ya kutoka Black Site akiwa amechoka sana Bi. Sandra alikua akiegesha gari lakeΒ kwenye jumba moja la ghorofa ambamo ndimo alimokua akiishi, Ulikua usiku umeshaingia,Β nywele zake alizozifunga kwa nyuma zilikua zikimfuata kila aendako.Β
Palikua kimya sana, kichwani alikua na mawazo tele, kwanza alihitaji hizo nyaraka za siriΒ ambazo Elizabeth alikua nazo na pia alifikiria sana kuhusu Mauwaji aliyoyafanya kwa RaisΒ Lucas Mbelwa. Kwa kiasi kikubwa alianza kujiona mwenye hatiaΒ
Akalisogeza gari hadi maegesho, alipomaliza alishuka ili aelekee juu ambako alikua akiishi,Β eneo la maegesho lilikua na magari mengi, pia palikua na giza la wastani lakini ambaloΒ haliwezi kuyashinda macho yake, akapiga hatua kadhaa lakini akahisi uwepo wa Mtu nyumaΒ yake, akasimama kisha haraka akageuka lakini hapakua na Mtu yeyote yule.Β
Akashusha pumzi nzito ya wasiwasi, palikua kimya kuliko kawaida. Alipogeuka mbeleΒ alimwona Mtu mmoja aliyevalia suruali ya Jinzi ya Bluu, shati jeupe alilolichomekea vizuri.Β Akapata ahueni, akatabasamu kisha akaendelea mbele.Β
Yule Mtu alikua Mwanaume aliyeenda hewani, mweusi mwenye mwili uliojengeka vizuri,Β alipokaribiana na Bi. Sandra alianza kutafuta kitu mfukoni mwake lakini kwa Bahati mbayaΒ aliangusha Karatasi alizokua amezibeba, akainama kuokota, Bi Sandra akajikuta tuΒ akimsaidia kuziokota maana zilikua zimetawanyika sana.Β
Namna ambayo Bi. Sandra alikua akiishi ni ngumu sana kugundua alikua Muuwaji waΒ kuaminika.Β
βOoh Ahsante sanaβ alisema Mwanaume huyo baada ya Bi Sandra kumpatia karatasiΒ alizokua ameziokota.Β
βSiku nyingine uwe makiniβ akasema Bi. Sandra akiwa anampa tabasamu Mwanaume huyoΒ aliyemzidi umri parefu sana. Alipotaka kuachana naye Mwanaume yule akamwambia Bi.Β SandraΒ
βSamahani Naitwa Skandaβ alisema huku akitabasamu kama Mtu aliyehitaji ukaribu na Bi.Β Sandra, hakujua Mtu aliyekua akizungumza naye alikua Mtu wa namna gani, haraka Bi.Β Sandra akajua Mwanaume huyo alihitaji ukaribu, alizungumza akiwa amempatia mkono Bi.Β Sandra.Β
Bila Hiyana Bi. Sandra alirudisha tabasamu pamoja na Mkono, akampa Mwanaume huyo.Β Sekunde moja tu ikabadilisha kila kitu, yule Mwanaume akaubana mkono wa Bi. Sandra kwaΒ nguvu huku akitabasamu,kwa kutumia ujuzi wake Bi. Sandra akajitoa
Alipojiangalia aliona ana tundu dogo linalotoa damu, kisha ghafla nguvu zilianza kumwisha,Β akachomoa Bastola yake ili amshambulie Mwanaume huyo aliyekua amesimama mbele yake,Β cha ajabu Mwanaume yule hata hakujitingisha, pale pale Bi. Sandra alianguka na kuanzaΒ kutapa tapa, yule Mwanaume akaangalia huku na kule kisha akauvuta mwili wa Bi. Sandra naΒ kuuingiza chini ya gari yake, halafu akajikungβuka vumbiΒ
Akaitoa simu kutoka mfukoni kisha akapiga mahali.Β
βNani anafuata?β akauliza Mwanaume huyo, Naaam!! Mpango wa Waziri Mkuu Haji BabiΒ ulianza kufanya kazi, tayari Muuwaji alikua kazini kufyeka wote anaowahofia kwenyeΒ Utawala wake. Maisha ya Bi. Sandra yakaondoka kizembe.Β
**Β
Waziri Mkuu Haji Babi, akaketi kwenye kiti cha Rais akiwa anagida mvinyo, muziki waΒ taratibu ukiwa unamburudisha huku Muuwaji wake akizidi kufanya Mauwaji Usiku huo,Β hakuishia kwa Bi. Sandra, akammaliza Balozi akiwa ndani ya gari kwa kutumia kitambaaΒ chenye Sumu.Β
Mauwaji haya yalifanyika kwa siri nzito na uharaka wa ajabu sana, kipaumbele sasa kikawaΒ ni kupata Nyaraka za siri zilizopewa jina la M21, akamtuma Muuwaji wake wa kuaminikaΒ kwenda Ilipo Black Site kumchukua Elizabeth Mlacha. Akampa ramani ya mahali ilipo BlackΒ Site, akaondoka Usiku huo huo na gari ndogo aina ya Carrina C4 kuelekea Black Site.Β
Kitu pekee kilichobakia kwa Waziri Mkuu ni kupata nyaraka ili kifo cha Rais kitangazwe,Β Upande wa pili ndani ya GodauniΒ
Muhonzi akafanikiwa kukata kamba alivyofungwa, giza lilikua nene ndani ya ChumbaΒ alichohifadhiwa, akajaribu kuchungulia dirishani kwa mtindo wa kuruka sababu dirishaΒ lilikua juu sana lakini hakuambulia kuona chochote kile, akajaribu kuitaΒ
βKuna nani hapo nahitaji Majiβ aliita kwa makusudi huku akifahamu fika kua eneo hilo linaΒ ulinzi mkali kuhakikisha yeye hachomoki, akaita tena, ndipo aliposikia hatua za kiatu zikijaΒ upande wake, akarudi haraka kuketi sakafuni alipokua ameketi.Β
Mara taa ikiwashwa, kisha akatupiwa maji aliyoyataka.
Nini kitaendelea?Β
Usikose SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost MSALA Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMΒ Β
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
MSALA xx MSALAxx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA
8 Comments
wakwanza kuisoma
Ni mimi
π₯π₯
πππ
Msalaa ππ
Weeeee weee hatar na nusu
Jaman masala ni moto wa quotes mbali admin umeweza
Nzuri