Ilipoishia “Muhonzi akafanikiwa kukata kamba alivyofungwa, giza lilikua nene ndani ya ChumbaΒ alichohifadhiwa, akajaribu kuchungulia dirishani kwa mtindo wa kuruka sababu dirishaΒ lilikua juu sana lakini hakuambulia kuona chochote kile, akajaribu kuitaΒ
βKuna nani hapo nahitaji Majiβ aliita kwa makusudi huku akifahamu fika kua eneo hilo linaΒ ulinzi mkali kuhakikisha yeye hachomoki, akaita tena, ndipo aliposikia hatua za kiatu zikijaΒ upande wake, akarudi haraka kuketi sakafuni alipokua ameketi.Β
Mara taa ikiwashwa, kisha akatupiwa maji aliyoyataka. EndeleaΒ
SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA
βNitakunywaje sasa na umenifunga kamba?β akauliza Muhonzi kwa ujanja huku akiwa tayariΒ ameshakata ile kamba, yule Mlinzi akamtazama sana MuhonziΒ
βNi kweli sasa nitakunywaje nina kiu sana Aaaaaahhhβ akazidi kusema Muhonzi hukuΒ akijibaraguza kama Mtu aliyefungwa mikono yake, yule Mlinzi ikamlazimu kufungua sasaΒ mlango wote kisha akaingia ndani ya chumba hicho, ndicho alichokua anakitaka Muhonzi.Β
Akaoneshwa Bunduki, kisha akaambiwaΒ
βHuwezi kufanya ujanja wowote, nitakupa majiβ alisema yule Mlinzi, akaiokota chupa yaΒ maji kisha akaifungua na kumsogezea Muhonzi ili amyweshe, hakujua kua alikuaΒ ameshafanya kosa kubwa sana, pale pale Muhonzi akamtandika ngumi nzito ya pua,Β
akamfwata kwa haraka na kumvunja shingo. Akaiyokota ile Bunduki kisha akaanza kutafutaΒ njia ya kutoka ndani ya Godauni.Β
Akatembea kwa taratibu kwa mahesabu mazito sana ili asije rudi mikononi mwa Zagamba,Β akasikia sauti ya TV, akajua fika kua Walinzi wengine walikua huko. Akasogea hadi eneoΒ hilo na kuwakuta walinzi wakiwa wanakunywa pombe na kuvuta sigara.Β
Hakutaka kusema nao, akatafuta kona nzuri akapita ili alifikie lango kuu la kutoka ndani yaΒ Godauni hiyo iliyojaa giza zito. Taratibu sana Muhonzi akalisukuma lango kisha akatoka njeΒ ya Godauni, muda ulivyozidi kwenda ndivyo ambavyo wale Walinzi walivyoshtuka baada yaΒ kuona mwenzao harudi, akatumwa mmoja wao kwenda kuangalia, akamkuta akiwaΒ ameshakufa. Msako wa kutafutwa kwa Muhonzi ukaaanza ndani ya lile Godauni, walipokujaΒ kugundua kua alishatoka ndani ya Godauni tayari Muhonzi alikua ameshafika mbali kabisa.Β
**Β
Baada ya kuchomoka mikononi mwa Watu wa Zagamba, akakimbilia kwenye jumba la siriΒ ambalo alikua akilitumia kufanyia kazi zake, kichwa chake kikiwa kinawaka moto kwanzaΒ alihitaji kujisafisha mwili mzima baada ya kukaa godauni kwa siku kadhaa.Β
Maji ya Baridi yakakubali kuuufanyia Utakaso wa kutosha mwili wa Muhonzi, akili ilipokaaΒ sawa akawa tayari kujua ni wapi alipo Elizabeth, bado aliamini kuwa alikua hai. Jambo laΒ kwanza alilolifanya baada ya kuketi na kuwasha mitambo yake ni kuanza kusaka mara yaΒ mwisho simu ya Elizabeth ilizimwa wapi.Β
βPicha ya Ndegeβ ndiyo sehemu pekee ambayo simu ya Elizabeth ilizimwa kwa mara yaΒ mwisho, aina ya simu aliyoitumia ilionekana lakini uzuri simu hiyo bado ilikua Hewani,Β Usiku ulikua mwingi, akajipumzisha kwanza Kitandani ili akiamka aendelee na upekuziΒ wake kwa njia ya Mtandao, masuala hayo ndiyo yaliyokoleza ukaribu wake na ElizabethΒ Mlacha.Β
**Β
Saa 3 Asubuhi, TanzaniaΒ
Muuwaji wa kuaminika alikua akipata chai ya asubuhi sehemu fulani ya Tanzania, safariΒ yake ya Usiku mzima ilikomea kwenye moja ya Hoteli, alipumzika hapo ili afanye safari yaΒ kuelekea eneo nyeti la Black Site.Β
Baada ya kumaliza, aliingia kwenye gari kisha akaendelea na safari yake ya Masaa matatuΒ baada ya Chai, sasa aliushika Msitu mmoja, akaisweka gari eneo fulani, akachukua begi lakeΒ na kupandisha kilima kimoja. Alionekana ni Mtu anayejua anachokifanya, kazi aliyopewa naΒ Waziri Mkuu ni kuhakikisha anamchukua Elizabeth kutoka Mikononi mwa Walinzi wa BalckΒ Site.Β
Begi alilolibeba lilikua na silaha moja ya masafa marefu pamoja na Darubini, aliketi juu yaΒ kilele cha kilima hicho, huku macho yake akiyaelekeza eneo la umbali wa Kilomita Nane,Β hapo ndipo ilipo Black Site.
Akatoa Ramani ya jengo la Black Site, ramani hiyo ilichukuliwa Ikulu baada ya Waziri MkuuΒ kuikamata Ikulu, muuwaji akatabasamu. Kisha akalala usawa mzuri na kuiweka Bunduki yaΒ Masafa marefu vizuri, akachukua Darubini na kuanza kulikagua jengo hilo kwa uzuri.Β
Akajifunika kofia nyeusi, kisha akairejesha Darubini ndani ya Begi, akaanza kuitumiaΒ Darubini iliyo kwenye Bunduki yake, macho na hisia zake akayaelekeza ilipo Black Site,Β eneo alilolala alikua akilitazama jengo hilo lenye vioo kwa uzuri sana.Β
Aliona na kuhesabu idadi ya Walinzi walio ndani ya Jengo ambao ni Makomandoo waΒ kuaminika aliokua akiwatumia Rais Lucas Mbelwa, alihitaji kuwamaliza kwanza. Ndani yaΒ jengo palikua na zaidi ya Makomandoo hamsini. Wote aliwapigia mahesabu, kisha akaikunjaΒ Bunduki yake na kuizamisha ndani ya Begi, akarudi chini ya Kilima na kuanza kutembeaΒ kwa kutumia barabara ya vumbi iliyokua ikielekea Black Site.Β
Muuwaji huyo, alipokaribia aligundua kwa haraka uwepo wa ulinzi maalum wa NyayaΒ nyembamba za Umeme ambazo ndizo zilizokua zikilinda eneo hilo, alishajiandaa sababu siriΒ za ulinzi wa ndani na nje ya Jengo alikua amezipata.Β
Akachomoa kifaa kidogo chenye mfanano na Simu, kisha akauzima umeme huo ndani yaΒ sekunde ishiri akawa amezivuka nyaya hizo. Taratibu akakimbia na kujificha nyuma ya ukutaΒ wa jengo la Black Site, kuhusu idadi ya walinzi wa ndani ya Jengo hakua na wasiwasi naoΒ sababu alishawapigia mahesabu makali sana.Β
Akasimama hapo kwa mahesabu mazito, kisha akachungulia, jengo hilo lililokua na viooΒ vingi ambavyo vingefanya urahisi wa Muuwaji kujulikana kua amefika, akapiga hatua zaΒ haraka na kuuwahi ukuta wa pili, akajificha kisha akatoa kamba kutoka ndani ya Begi lake,Β akairusha kamba kuelekea juu, iliponasa akawa na zoezi moja tu la kuifuata paa ya jengoΒ hilo.Β
Kisha taratibu akatembea juu ya paa la jengo huku akiwa anapiga mahesabu yake vizuri,Β alikua na ramani nzima ya jengo hilo la Black Site, ilikua rahisi kwake kujua ni wapi atawekaΒ kambi hapo juu ya paa ya Jengo, akafika mahali ambapo palikua na pambo kubwa la saa,Β eneo hilo lilikua karibu na mlango Mkuu wa Kuingia ndani ya Jengo hilo, kando ya jengoΒ ndimo walimokua wakikaa makomandoo.Β
Kwake hao ndiyo kikwazo kikubwa kufanikisha kazi ya Kumchukua Elizabeth, akaiwekaΒ vizuri kofia yake kisha akalala kwa ustadi mzuri huku akilitazama jengo ambaloΒ Makomandoo walikua wakipatikana.Β
Akaishusha Bunduki yake ya Masafa marefu kutoka ndani ya Begi lake kisha, akaitega vizuriΒ kuelekea kwenye jengo, kichwani alikua na ramani yote. Kitu pekee alichohitaji kukifanyaΒ hapo ni kuufunga mlango wa Umeme ambao ndio uliokua ukitumika na Makomandoo hao,Β mwendo wa dakika ishirini awe tayari ameshamchukua Mateka wake kwani kupambana naΒ Makomandoo hao haikua kazi rahisi kwake.Β
Akafunga kiwambo cha kuzuia sauti, kisha akalenga kitasa cha Umeme ambachoΒ kingemfanya atenganishe kati ya Makomandoo na Walinzi wa kawaida wa Black Site,Β umbali wa jengo hilo ni zaidi ya Mita sabini.
Dakika moja na nusu ilimtosha kujihakikishia kua risasi atakayoiachia hapo itaenda kukataΒ mawasiliano ya jengo la Makomandoo na jengo la Black Site. Akavuta hewa nyingi kishaΒ akaiachia taratibu na kukaza mikono yake kisha kidole kikafanya kazi ya kusukuma risasiΒ Β
Haraka Alam ikalia kuashilia kua palikua na hitilafu mlangoni, hii ni baada ya Muuwaji huyuΒ kukita risasi mlangoni. Haraka walinzi wa Black site pamoja na Makomandoo walio ndani yaΒ jengo lililopigwa risasi wakawa kwenye taharuki nzito, akasubiria kwa sekunde kadhaa iliΒ Mlango wa Black Site ufunguliwe, alipousikua umefunguliwa akajirusha mithiri ya NyaniΒ mzeeΒ
Akatua chini kama Buibui, haraka akaachia pigo takatifu la Risasi za mahesabu naΒ kusambaratisha walinzi watatu waliokua eneo la Mlango kisha akaingia ndani ya Jengo hilo.Β
Elizabeth aliposikia Alam ikilia kuashiria kuna tatizo alishaanza kuhisi ujio wa Mtu mbayaΒ ndani ya Jengo la Black Site, japo alikua amechoka sana lakini akaweza kumwambia MlinziΒ kua amfungue kwani eneo hilo siyo salama kabisaΒ
βUsipofanya hivyo Utakufaβ akakazia Elizabeth huku akijitingisha kwa nguvu chacheΒ alizobakiwa nazo, yule Mlinzi hakutaka kumwelewa Elizabeth hadi pale aliposikia risasiΒ ikisikika karibu na Mlango wa chumba cha Mateso ambacho Elizabeth alikua amehifadhiwa.Β
βNifungue tafadhaliβ alisema Elizabeth, lakini akili ya yule Mlinzi ikajikuta imezubaaΒ kidogo, ghafla akapigwa risasi ya Kichwa, kisha Mlango ukafunguliwa, akaingia Muuwaji,Β akamtazama Elizabeth kisha akatoa tabasamu la kufanikisha kazi yake.Β
Hakutaka kupoteza muda akamzimisha kwa kumchoma sindano ya Usingizi, akamfungua naΒ kumweka begani, maiti za Walinzi zilikua za kutosha sakafuni, akatoka hadi nje ya Jengo laΒ Black Site wakati huo Makomandoo wakiwa wanahangaika namna ya kufungua ule MlangoΒ wa Umeme ambao kwa kawaida hufunguka baada ya dakika ishirini endapo utapata Hitilafu.Β
Akauvuka uzio wa Umeme kisha akaanza kuzikata Kilomita kuelekea lilipo gari lake aanzeΒ safari ya kurejea Ikulu, mara zote alikua akiitazama saa yake kwa maana zikitimia dakikaΒ ishirini wale Makomandoo watatoka ndani ya jengo na kuanza kumsaka kila kona. AkaianzaΒ riadha baada ya kugundua kua alikua amebakisha dakika tatu kumalizika kwa ule mudaΒ aliokua ameupangilia kulifanya tukio la kuvamia Black Site.Β
Ndani ya jengo tayari makomandoo walishajiandaa kutoka huku wakisubiria muda muafakaΒ ambao Mlango huo wa umeme utakapokua umefunguka, Muuwaji alikua akikimbia naΒ Elizabeth aliyepoteza fahamu, akapandisha kilima kidogo lakini kwa Bahati mbaya akaterezaΒ na kujikuta akimtupa Elizabeth ambaye akavingirika na kutumbukia kwenye korongo, kwaΒ Bahati nzuri akanasa kwenye Mti.Β
βShit!!β akasema Muuwaji, akaanza harakati za kutaka kumtoa Elizabeth, lakini kelele zaΒ Makomandoo zikasikika, akatazama saa yake na kuona tayari muda ulikuwa umekwisha naΒ tayari Makomandoo walikua wakija kwa kasi mahali ambapo Muuwaji alikua amesimama.Β
Kwanza akatafuta mahali na kujificha ili Makomandoo wasiweze kumwona, akaangalia risasiΒ zilizopo kwenye Bastola yake, kisha haraka akaenda mbali na eneo lile, akauzunguka mlimaΒ mmoja na kwenda kujificha huko kisha haraka akaitoa Bunduki yake kutoka ndani ya Begi.
Akaielekeza eneo ambalo Elizabeth alikua ametumbukia, alikua akihema kutokana naΒ kukimbia kwa muda mrefu, Makomandoo wakalipita lile eneo kisha walipofika mbeleΒ walitawanyika ili kumsaka kwa uzuri adui yao baada ya kugundua adui yao hakuitumiaΒ Barabara ya vumbi bali alizama Msituni.Β
Muuwaji akautumia Mwanya huo kuuzunguka Mlima mdogo na kisha kutokea nyuma yaΒ Makomandoo kisha akapiganisha akili namna ambavyo anaweza kumchukua ElizabethΒ kutoka juu ya Mti ulio korongoni, mara akasikia mlio wa gari ukija kutokea Upande wa kuliaΒ ambapo ndiyo palikua na njia ya kutoka Black Site, haraka akajitupa Korongoni na kutuaΒ kwenye ule Mti ambao Elizabeth alinasia kisha kwa haraka akamsomba na kushuka nayeΒ chini ambako palikua Na Msitu wa kutosha.Β
Akajipigiza bega kwenye jiwe, kila mmoja akatua upande wake lakini hakuna HataΒ Komandoo mmoja aliyeshtuka kua Adui yao alikua Korongoni, wenge zito likamzongaΒ Muuwaji akiwa anajitafuta, akayaruhusu macho yake kutulia, akamwona Elizabeth akiwaΒ mita kadhaa kutoka alipo yeye.Β
βAgggghhhβ akagugumia kwa maumivu makali huku akinyoosha bega lake, lililo jaa damu,Β kisha akajisomba na kumsogelea Elizabeth. Akasimama na kuvuta hewa ya kujituliza vyemaΒ halafu akaangaza juuΒ
Jua lilikua likiwaka, ndege wa Msituni walikua wakipiga kelele za hapa na pale, PurukushaniΒ eneo la juu zilikua za kutosha kisha akajishika kiuno chake na kujinyoosha vyema, hakuishiaΒ hapo akachana tisheti lake na kujifunga eneo la Bega, kisha akiwa amebakiwa na vest nyeusiΒ akajitwika Elizabeth, akaanza kuisaka njia ndani ya Msitu wenye giza.Β
Haikua rahisi kwake kujua alikua akielekea upande upi kwasababu alikua ameshapotezaΒ mwelekeo sahihi, akajikuta akisambaa Msituni kwa muda mrefu hadi pale Helkopta za BlackΒ site zilipoanza Msako kila kona ya Msitu.Β
**Β
Kelele za popo na sokwe zilianza kusikika ndani ya Msitu wa Magoroto, hatua kubwa zaΒ vishindo zilimfanya Benjamin Kingai aliye ndani ya pango atoke, kwanza alikutana naΒ Zandawe akiwa amevaa nguo za ngozi za wanyama. Pili alikua ameongozana na kundiΒ kubwa la Popo waliozingira eneo la juu ili kumpa kinvuli.Β
Tatu, alikua ameshikilia Mkuki aliouchomeka chini, vyote hivi vikamfanya BenjaminΒ ashangae, lakini tabasamu la kuchanua lilikua likiongezeka kwenye sura ya Malkia Zandawe.Β Taratibu Benjamin alisogea karibu na Zandawe na kumuuliza kwa utaratibuΒ
βKuna nini?β alihoji kwa sauti ya chini ili adokezwe lakini Malkia Zandawe akajibu kwaΒ sauti.Β
βLeo ni siku ya Ukombozi Benjamin, siku ambayo unaenda kurudisha kila ulichokipotezaβΒ alisema kisha alikaa kimya, akamfanya Benjamin atupe swali jingineΒ
βUnamaanisha nini kusema kila nilichokipoteza?β akauliza Benjamin Kingai, kisha akamezaΒ funda zito la mate huku kivuli cha wale popo ambao ndiyo jeshi la kuaminika la MalkiaΒ
Zandawe likiwa linamsaidia pia Benjamin kuikimbia mionzi ya jua ambayo ilianza kuaΒ Mikali.Β
βUmepoteza familia, umepoteza haki ya kuishi ndani ya Nchi yako, pia Mtoto na MpenziΒ wako.β Benjamin akatoa tabasamu lenye Maswali mengiΒ
βUnamaanisha……β kabla hajamaliza kusema alikuja ndege mpelelezi wa Zandawe kishaΒ akatua chini na kusema kwa Lugha ya ndege kisha Zandawe akamjibu BenjaminΒ
βEneo uliloteswa imevamiwaβ alisema Kama vile Mtu aliyejua haswa anachosema, taarifaΒ zote alipewa na ndege wake mpelelezi, hii ilimshtua sana Benjamin akajawa na taharukiΒ
βVipi kuhusu Mtoto na….βΒ
βMpenzi wakoβ akadakika Zandawe kisha akasemaΒ
βInatupasa kwenda sasa hivi huko kujua kinagaubaga, huo uvamizi hatuna hakika unafanywaΒ kwa lengo gani, lakini yupo Msichana aliyetoroshwa hukoβ alisema Malikia Zandawe kishaΒ alisubiria jibu la Benjamin, kabla hajajibu chochote Benjamin akamtazama yule ndege kishaΒ akainama na kumwambia ndege huyoΒ
βAhsanteβ aliposimama akamuuliza Malikia ZandaweΒ
βTunafikaje huko?βΒ
Malikia Zandawe akatabasamu kisha akamjibu kwa kumwambia nifuate, aliposema alikuaΒ tayari amegeuka na kuanza kutembea huku wale Popo wakimfuata kwa juu, akamsogeza hadiΒ eneo la wazi ambalo lilikua halina Miti kabisa ila lilizungukwa na Msitu mkubwa waΒ Magoroto.Β
Katikati ya eneo hilo palikua na kitu kilichofunikwa Majani mengi makavu, Malkia ZandaweΒ akasogea hadi hapo kisha akaanza kuondoa yale Majani yaliyokuaa yamerundikana,Β Benjamin alipata Mshangao mkubwa baada ya kuona Helkopta ikiwa ndiyo iliyokuaΒ imefunikwa hapo.Β
Pale pale kabla hata hajamaliza kushangaa akaletwa Mtu mmoja aliyefungwa mdomo wake kwa kitambaa, aliletwa na Sokwe Mkubwa ambaye ni rafiki wa Malkia Zandawe, Mtu huyoΒ alikua na mavazi ya Urubani, alionekana wazi kua ndiye aliyekua rubani wa Helkopta hiyo.Β
βNitakuacha Huru ukinifikisha nitakapoβ alisema Malkia Zandawe kisha akamtoa kitambaaΒ eneo la Mdomo.Β Β
βSiyo Mtu mbaya, ila mmenifanya nimekua Mbaya kwasababu hamtaki kuuheshimu naΒ kufuata Misingi na mila za Msitu huuβ alisema Malikia ZandaweΒ
βNaomba tafadhali, mateso niliyopata yametosha kua funzo kwangu, naomba niendeΒ nitawaeleze ukweli kuhusu huu Msitu, naamani hakuna mwingine atakayetia mguu kwenyeΒ huu Msitu.β Alisema yule rubani huku chozi likimbubujika, Malkia Zandawe akainama naΒ kumwambia
βNimeshakwambia kua sina ubaya na wewe, hamkutaka kusikiliza onyo langu, ukawe chanzoΒ cha wengine kuupa heshima huu Msituβ Alisema kisha aliposimama akamwambiaΒ
βNaamini hili litakua funzo kubwa kwenu, sikutaka kukuuwa kwa maana nilikua na UwezoΒ wa kukufanyia ubaya kama niliowafanyia wengine walioingia ndani ya Msitu bila kufuataΒ utaratibu. Kuna viumbe vinaishi humu, vinahitaji utulivu n amani kama ambavyo nyinyi kilaΒ siku mnapiganiaβ alisema Malikia Zandawe, kidogo akaanza kulengwa na Mchozi.Β
Benjamin akamsogelea Malkia Zandawe na kumtuliza kwa kumshika bega, hata yule rubaniΒ wa Helkopta ya Kijeshi aliona wazi kua Binti huyo alikua akizungumza kwa hisia kali iliyomuumiza. Malkia Zandawe akafuta chozi lake kisha akamwambia ndege wake mweupeΒ aongoze njia, akamtaka na Benjamin aingie ndani ya Helkopta hiyo pamoja na sokwe wakeΒ ampendaye.Β
Kitendo cha ndege kuruka kiliwafanya na Popo kuzama Msituni zaidi kwa kukimbia kwaΒ spidi kali kisha Benjamin, rubani, Malkia Zandawe na Sokwe wakaingia ndani ya HelkoptaΒ hiyo tayari kuelekea ndani ya Black Site kuikomboa familia ya Benjamin Kingai. DakikaΒ tano baadaye Helkopta ikawa angani ikimfuata ndege mkubwa mpelelezi aitwaye Gola.Β
Nini kitaendelea?Β
Usikose SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost MSALA Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMΒ Β
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
MSALA xx MSALAxx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA
9 Comments
Hatareee, mambo ni π₯π₯π₯π₯
nice sasa kwel ubaya ubwela , ila prime ministerππ
Wooow mambo yanzd kuwa mamboπ₯π₯
Tuwekee na sehemu inayofata ya 27 leo saa 3 π
Konki
ππ
π₯π₯π₯π₯
Admin kazi nzuri ππ
π₯π₯π₯π₯