“Ilipoishia” Roho ya Elizabeth ilifukuta kwa maumivu Makali sana, hapo alipaswa kufanya kazi mbili, moja ni kumwokoa MUHONZI Kutoka mikononi mwa mwenyekiti wa chama cha Upinzani na pili alipaswa kutoisalimisha ile flash Muhimu aliyoificha kwenye chupi yake.
Dakika Moja walizungukwa kila upande βMikono juuβ ilisema sauti komavu iliyojaa hasira, ilikua ni sauti ya Brigedia Antony, kila upande walizungukwa na kikosi kazi, Hatimaye Elizabeth aliamini ameshafikia mwisho baada ya siku Tatu za Hekaheka nzito.Β Endelea MSALA SEASON 3Β
SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA
Chozi liliendelea kumbubujika Elizabeth, alishakiona kifo mbele yake, mwili wa MsichanaΒ huyu ulitweta ghafla. Alikosa nguvu, Moyoni alimwona Mzee Kimaro kama Msaliti, alionaΒ Mzee huyo hakupaswa kujisalimisha kirahisi vile, Uamuzi ule ndiyo ukapelekeaΒ Makomandoo kuzidi kuwazunguka kila kona.Β Β
Brigedia Antony alikua wa kwanza kusogea hapo akiwa na Bunduki yake mkononi,Β alishachoka dharau na kebehi za Bi. Sandra, alijawa na hasira. Alilizunguka Jiwe naΒ kuwakuta Mzee Kimaro pamoja na Elizabeth wakiwa wameketi. Macho ya Brigedia AntonyΒ hayakutulia, kwanza alistaajabu kumwona Msichana mwenyewe, alikua Mdogo siyo waΒ kuwasunbua kwa Muda wote huo, pili ni Mtu aliyekua akimsaidia Msichana huyo,Β alimtazama kama Mzee Goigoi asiyeweza lolote.Β
Akachuchumaa akimkodolea macho Elizabeth, mara akaja Komandoo mmoja kabla hataΒ Brigedia Antony Kesi hajasema chochote.Β
βTuna maagizo ya kumchukua sasa hiviβ alisema Komandoo huyo aliyemsimamia BrigediaΒ Antony kwa nyuma, Brigedia alipogeuka alikutana naye uso kwa uso, mazungumzo yalikuaΒ yakifanyika kwa sauti kubwa kwasababu ya kelele ya panga boi za Helkopta zilizotanda juu.Β
Brigedia Antony hakua na sauti, akasimama ili Elizabeth achukuliwe japo aliona kamaΒ amedharaulika mbele ya wanajeshi wengine lakini alijua maelekezo hayo yalitoka Ikulu kwaΒ Rais, hakuna aliyekua na taarifa kua tayari Rais aliuawa.Β
Makomandoo waliwaswamba Mzee Kimaro na Elizabeth ili wawaingize kwenye Helkopta,Β Elizabeth akaweka ngumu baada ya kusimama mbele ya Brigedia kisha akamwambiaΒ
βUnafanya kosa kubwa sana, utalijutia siku mojaβ baada ya kusema hivyo alisukumwa kwaΒ nguvu kuelekea kwenye Helkopta, Hatimaye Elizabeth na Mzee Kimaro walinaswa. TaarifaΒ ya kunaswa kwao ilifika Ikulu kwa Waziri Mkuu Haji Babi mwenye tamaa na Madaraka,Β nyuso za Tabasamu ziliwajaa.Β
Dakika moja, Helkopta zilianza kuondoka eneo hilo la mpaka wa Kiluvya, Uelekeo ukawa niΒ Black Site kupitia Msitu wa Magoroto Mkoani Tanga, mahali ilipo Black Site ni siri nzitoΒ sana. Mara moja wakapigwa na kupoteza fahamu ili wasijuwe wanapopelekwa.Β
**Β
Gari nyeusi isiyo na namba ya Usajili iliyokua ikitumiwa na Zagamba ilifika eneo laΒ Godauni, mshale wa saa yake ulikua ukisoma saa 11:15 Alfajiri, Dakika kadhaa baada yaΒ
tukio la kunaswa kwa Elizabeth. Uso wake ulijawa na Hasira sana, akaelekea kwenyeΒ chumba alichohifadhiwa Muhonzi.Β
βUnasikia wewe Mshenzi, Elizabeth amenaswa Muda mchache uliopitaβ alisema ZagambaΒ akiongea kwa hasira kisha akamwonesha video ya kunaswa kwa Elizabeth, moja ya AskariΒ walio eneo la tukio walimtumia video hiyo kwa siri sana. Muhonzi alishtuka sana,Β alichokiona kilimduwaza, akajikuta akipepesa macho yake kama fundi saa aliyepoteza nati.Β
Hakujua aseme nini, mikono yake ilifungwa kwa nyuma hivyo hakuweza hata kunyanyuaΒ chochote. Alijitingisha lakini hakuweza hata kusogea, mara akavutwa kwa nguvuΒ
βSema ni wapi ilipo M21!β Alingβaka Zagamba akilihitaji faili la siri la Rais Lucas Mbelwa,Β Mara simu ya Zagamba iliita, alimkata jicho kali Muhonzi wakati anaitoa simu yakeΒ mfukoni. Kisha aliondoka eneo hilo kwa ajili ya kuzungumza na SimuΒ
**Β Β
Jua lilikua tayari limeshatua, palionekana kua na hali ya kawaida sana siku hiyo lakiniΒ palikua na siri nzito juu ya kifo cha Rais Mbelwa, Waziri Mkuu Haji Babi na washirika wakeΒ walifanya kikao cha siri ndani ya Ikulu, kikao hicho kilikua na ajenda kuu moja, ni jinsi ganiΒ watafanya mapinduzi baada ya kifo cha Rais Mbelwa, kitu cha kwanza walichokipaΒ kipaumbele ni nyaraka M21 ambayo ilikua na siri nyingi za Rais Mbelwa na baadhi yaΒ viongozi wengine wa ngazi za juu akiwemo Bi. Sandra ambaye alikua Mshirika mkubwa waΒ Rais Mbelwa, hata yeye Waziri Mkuu kuna siri zilikuwamo ndani ya Nyaraka hiyo kumhusu.Β
Jukumu la kupatikana kwa nyaraka akakabidhiwa Bi. Sandra ambaye aliaminika kua ni MtuΒ hatari sana, akaondoka Ikulu asubuhi hiyo kwa Helkopta tayari kuelekea Kitengo nyeti chaΒ Black Site.Β
**Β
Jua lilikua linawaka kwa wastani, asubuhi tulivu ilimkuta Benjamin Kingai akiwa ameketiΒ juu ya jiwe moja ndani ya Msitu wa Magoroto, mazingira hayo yalimfanya Benjamin ajisikieΒ vizuri, mbele yake palikua na bwawa dogo ambalo alikua akilitupia vijiwe vidogo vidogoΒ ambavyo vilikua vinatoa sauti nzuri vinapoingia ndani ya Maji.Β
Mara alikuja Malkia Zandawe na kuketi kando ya Benjamin, hakua na hofu tena na BintiΒ huyo baada ya kuona mambo makubwa ambayo Binti huyo aliyafanya.Β Β
βUnajisikiaje?β aliuliza Zandawe akiwa ni mwenye kutabasamu, Benjamin naye aliachiaΒ tabasamu lisilo na uhakika wa kipi anachokifurahia, akamjibu Malkia ZandaweΒ
βVizuri, nipo ndani ya Msitu wakoβ kisha alisindikiza kauli yake na kicheko kidogo, akatupaΒ tena vijiwe ndani ya bwawa.Β
βUsiwe na wasiwasi Benjamin, utaondoka ndani ya Msitu muda siyo mrefu, kwasasa angaliaΒ zaidi kuhusu hatma ya Maisha yako baada ya kutoka hapaβ akasema Malkia Zandawe hukuΒ naye akitupa vijiwe, wakaufanya huo kua ni mchezo kwao.
βAsante kwa kusaidia Maisha yangu, sijui bila kunisaidia ningekua wapi sasa hivi, pengineΒ ningekua nimeshauawa.β Akasema Benjamin akiwa analengwa na choziΒ
βUnafikiri ni kwanini huyo Msichana alikua na hizo nyaraka? Na hizo nyaraka zinahusu niniΒ hasa?β akahoji Malikia Zandawe akiwa anamtolea macho zaidi BenjaminΒ
βInaonekana kuna taarifa za siri sana kumhusu Rais, lakini sijui kwa hakika zaidi ni kwaniniΒ aliziibaβΒ Β
βBasi huyo Msichana kama atakua hai basi atakua sehemu ya hatari zaidi, kwa Msako uleΒ sidhani kama atapata mahali pa Kujifichaβ akasema Malkia ZandaweΒ
βLakini yule Msichana anaonekana kua zaidi ya Msichana, si Mtu wa kawaida. Ana mamboΒ mengi ya siri anayoyaficha, kingine ni mjuzi wa mbinu za kivitaβ alisema, pakawa na ukimyaΒ wa kutosha kisha Zandawe akatupa swali lingineΒ
βUmewaza kuhusu Hatma ya Mtoto wako na mpenzi wako, nyuma yako kuna niniΒ kitawakuta?β swali hili lilimpa nyakati ngumu Benjamin, akashindwa kulizuia choziΒ likamtoka likashuka hadi kwenye mashavu yake Madogo.Β
βKuwaza hatma yao ni sawa na kusema hakuna kifo, nachelea kusema pengineΒ wameshauawa huko waliko, roho yangu inanisuta ni kwanini niliwakimbia, nilikua mbinafsiΒ nikasalimisha Maisha yangu bila kuangalia ni Jambo gani litawafikaβ Alipoimaliza hii kauliΒ aliangusha kilio Benjamin, Malkia Zandawe akajawa na huzuni sana akamwambia BenjaminΒ
βHata ukilia kwasasa haitokua na Msaada, kikubwa ni kujua ni wapi walipo, na je wapo hai?βΒ Β
βKujua walipo ni jambo gumu sana, ile sehemu ni hatari, ni sehemu ya siri sana. Ni ngumuΒ kujua nini kimewafika, naweza kusema wameshakufaβ akasema Benjamin kisha akajiinamia.Β
βNitalichunguza hilo Benjamin, subiriaβ akasema Malkia Zandawe kisha akatoka spidiΒ kuzama Msituni, Benjamin hakuelewa ni kitu gani kilimfanya Zandawe azame Msitumi kwaΒ kasi namna ile.Β
Msichana Zandawe, alizidi kukimbia hadi alipofika eneo la Bwawa, hapo aliangaza huku naΒ kule, eneo hilo ndilo ambalo Benjamin alikua amejitupa Siku ile kwa lengo la kuokoa MaishaΒ yake kutoka juu ya Helkopta ya Kijeshi.Β
Akasogea hadi chini ya Mti mmoja, hapo chini aliziona kamba ambazo alifungwa nazoΒ Benjamin, kisha akazichukua kamba hizo akakimbia kurudi alipomwacha Benjamin, alikuaΒ msichana wa Msituni anayeutawala Msitu huo hatari unaowasumbua wengiΒ
Alifika alipomwacha Benjamin akiwa anahema sana, kisha akamwonesha Benjamin zileΒ kamba, haraka Benjamin akazikumbuka, akashuka kutoka juu ya jiwe hadi aliposimamaΒ Zandawe.Β
βUnataka kufanya nini?β
βSubiria uoneβ akasema Zandawe kisha akapiga mluzi mkali, ghafla ikasikika sauti ya ndegeΒ mmoja akija walipo, ndege huyo alikua mweupe anayefanana na njiwa mzuri wa kufugwa,Β alipofika hapo alitua juu ya jiwe ambao Benjamin alilikalia muda mchache ulio pitaΒ
βHuyu ni rafiki yangu anaitwa Gola, ni mpelelezi mzuri anayenipa taarifa nyingi kuhusu haliΒ ya Msitu, nataka kumtumaβ alisema Malkia Zandawe, kila alichokisema kilikua kama ndotoΒ kwa Benjamin, alijikuta akitabasamu.Β
Mambo kama hayo aliyasoma kwenye kitabu, ni Mfalme Suleiman pekee ndiye aliyekua anaΒ uwezo wa kuzungumza na ndege lakini Msichana Zandawe alikua na uwezo kama ule waΒ kuzungumza na ndege.Β
βUmtume wapi?βΒ Β
βHuko mahala pa siri, nataka kupajua. Nataka kujua hatma ya Familia yako BenjaminβΒ alisema Malkia Zandawe kisha alimsogelea ndege Gola, akazungumza naye kwa lugha zaΒ ndege kisha akampatia ile kamba kama alama ya wapi ilipo Black Site. Kisha ndege huyoΒ akaruka kwa spidi, akiwa ameishikilia ile kamba mguuni.Β
βGola ataleta majibu ni wapi ilipo Black Siteβ akasema Malkia Zandawe kisha akampaΒ tabasamu zito Benjamin ambaye alijawa na Bumbuwazi zito, midomo yake ikawa mizitoΒ kiasi kwamba hakuweza kusema chochote.Β Nini Kitaendelea?
Usikose sehemu ya ishirini na mbili ya MSALA SEASON 3 Kujua kama Elizabeth alipona kwenye Msala huu
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost MSALA Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMΒ Β
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
MSALA xx MSALAxx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA
11 Comments
Kubabekiππ.
Mwandishi upewe maua yako..π₯π₯
Hii story unaisoma huku unaiona movie. Mungu azidishe kipaji chako.
wa kwanza kuisoma
Watu kusoma
Mambo hayo moto π₯π₯π₯
π₯π₯π₯
πππππ
bonge moja la story ningekuwa muigizaji ningeandaa movie
Hakika mwandishi unatuleteaga story kali lakini hii ni zaidi ya story kali hongera sana admin mungu akupe maisha marefu
Story inanikumbusha vitu vingi na venye nasoma Kwa picha
Ni π₯π₯π₯π₯πΊ kongole adimini mkeka ukitiki hii msala ni kali mno..utakula 3k