Ilipoishia “Huko mahala pa siri, nataka kupajua. Nataka kujua hatma ya Familia yako Benjaminโย alisema Malkia Zandawe kisha alimsogelea ndege Gola, akazungumza naye kwa lugha zaย ndege kisha akampatia ile kamba kama alama ya wapi ilipo Black Site. Kisha ndege huyoย akaruka kwa spidi, akiwa ameishikilia ile kamba mguuni.ย
โGola ataleta majibu ni wapi ilipo Black Siteโ akasema Malkia Zandawe kisha akampaย tabasamu zito Benjamin ambaye alijawa na Bumbuwazi zito, midomo yake ikawa mizitoย kiasi kwamba hakuweza kusema chochote. Endeleaย
SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI
Elizabeth na Mzee Kimaro wakiwa wamepoteza fahamu waliswekwa ndani ya chumbaย kimoja, walikua sakafuni wakiwa hawajitambui. Elizabeth alikua wa kwanza kugutukaย kutoka kwenye Usingizi mzito, mahali alipo hakufanikiwa kupajua lakini kwa hakika alijuaย amewekwa sehemu nyeti kwa ajili ya mateso.ย
โMzee Kimaroโ aliita Elizabeth huku akimtikisa Mzee Kimaro ambaye aliamka haraka baadaย ya kutikiswa. Wote walistaajabu namna eneo hilo lilivyo kimyaย
โTupo wapi?โย
โUnafikiri tupo Mwambisi? Kwanini ulijisalimisha?โ Bado Elizabeth alikua akijiuliza swaliย hili, Mzee Kimaro akamwambia Elizabethย
โTungefia pale kwa mashambulizi makali Elizabeth, hatukua na silaha za kutosha zaย kupambana na kikosi kile, ilikua ni sawa na kazi Bureโ alisema Mzee Kimaro akiwaย anajikagua mikononi, alikua na alama nyingi za kamba.ย
โUngekamatwa wewe, Mimi nikasonga mbele, sasa sote tumenaswa ni nani atatusaidiaย kutoka hapa, kama ulikua hujui hapa ndiyo tumejichimbia Kaburi, mwisho wetu ni hapaโย akazidi kusema kwa hasira na lawama Elizabeth.ย
Mazungumzo yao yalikatishwa na sauti ya kufunguliwa kwa mlango wa chumba hicho, kilaย mmoja alipeleka macho yake mlangoni kuona ni Nani aliyekua akiufungua mlango huo,ย tokea wamefika hapo hawakupata kumwona Mtu yeyote wala kusikia sauti yeyote ile.
Wote macho yao yalimwona Mwanamke wa shoka, Bi. Sandra akiwa amevalia gauni refuย jekundu, wakajikuta wakimdadisi Mwanamke huyo aliyegoma kuzeeka kabisa, kwanzaย alikua akitabasamu huku akitembea kwa madaha kama anashiriki shindano la kusakaย walimbwende.ย ย
Mwisho alisimama karibu nao, kisha akachuchumaa, kwa sauti ya mapozi iliyojaa kebehiย nzito akawasalimiaย
โHatimaye tumeonana marafiki zangu, natumaini mmeyapenda makazi yenu mapyaโย alipomaliza kusema alijikungโuta vunbi kama vile alikua ameingia stoo ya vyakula, akaagizaย kitambaa ili ajifute vizuri kisha akawaambiaย
โHapa mlipo siyo sehemu nzuri, mtapata mafua. Nyinyi ni wageni muhimu sana hapa hivyoย hampaswi kua hapa, oooh! Sijui ni nani aliyewaweka hapa, naomba tafadhali muwatoe hapaโย akasema kwa kebehi kisha mwisho akamalizia kwa kuikaza sauti yake.ย
Halafu yeye akatangulia mbele wakati huo walinzi wakiwatoa akina Elizabeth ndani yaย chumba hicho, wakaingizwa kwenye chumba kimoja chenye visima vidogo viwili katikati,ย minyororo mikubwa ikiwa inaningโinia kwenye kila kisima.ย
โHebu waweke wanapostahiliโ akasema Bi. Sandra huku akiwa anaketi kwenye kiti, chunbaย hicho kilionekana kua ni chumba cha mateso kwa namna ambavyo vitu vilikuaย shaghalabaghala tena pakionekana kua ni eneo hatari sanaย
Michirizi ya damu ilikua imetapakaa kila kona ya chumba hicho, nyoyo za digidigi hawaย wawili zilianza kwenda mrama, wakafungwa minyororo mikononi kisha wakatoswa ndani yaย visima, kila mmoja akatoswa kwenye kisima chake.ย
Visima vya duara vilivyojengwa kwa mawe, havikua visima virefu sana lakini vilitoshaย kuwatesa, maji yakafunguliwa kisha yakaanza kujaa ndani yake, taratibu walianza kujikutaย wakianza kutapatapa. Kisha Bi. Sandra na walinzi wengine wakatoka ndani ya chumba hicho,ย minyororo haikuwapa nafasi ya kufanya chochote tena kibaya walifungwa kwa nyuma.ย
Bi. Sandra akaagiza kahawa na kuketi nje ya jengo la Black Site akiwa anautazama msituย ulioizunguka kambi hiyo ya siri, macho yake yakatua kwenye Mti mmoja, mti huo ulikuaย mrefu kiasi na ulikua karibu zaidi na jengo hilo lililojengwa kwa kiasi kikubwa na viooย vigumu.ย
Alikua akimtazama ndege mmoja mkubwa mweupe, ndege huyo alikua na kamba miguuni,ย alitabasamu kumwona ndege huyo ambaye baada ya muda mfupi aliruka. Namna alivyorukaย ilimpa tabasamu Bi. Sandra, ndege huyo alikua ni Gola.ย
Ndege aliyetumwa na Malkia Zandawe kwa lemgo la kuichunguza Black site, kwanza kujuaย mahali ilipo sehemu hiyo nyeti ambayo Benjamin alimwacha Mpenzi wake, kisha Bi. Sandraย akarejea ndani hadi kwenye chumba cha mateso.ย
Mzee Kimaro alikua akielea tu ndani ya kisima hicho, ueleaji wake uliashiri Mzee huyoย alikua tayari amefariki kutokana na maji kumzonga, uzee wake haukumfanya awe na nguvuย ya kukabiliana na adhabu hiyo, kisha akakitazama kisima cha pili, bado Elizabeth alikuaย akihangaika namna ya kujinasua na mtego huo wa kifo.
โOoh masikini, Mzee wako ameshindwa kuhimili, yeye ameaga mashindano mapema sana.ย Namtakia mapumziko memaโ alisema huku Walinzi wakiutoa mwili wa Mzee Kimaroย kutoka ndani ya Maji. Akaagiza pia Elizabeth atolewe ndani ya maji, kisha akaangalia saaย yake na kuona alitumia dakika kumi na tano kuwaacha wawili hao ndani ya maji.ย
Elizabeth alikua amechoka vibaya mno, maji yalikua yakimvuja. Kisha akakalishwa juu yaย kiti kimoja cha chuma. Alikua amelegea sana, Masikini alikua akitapika maji mengiย aliyoyanywa. Mwili wa Mzee Kimaro ulitiwa ndani ya mfuko maalum kisha walinzi haoย waliondoka na mwili wa Mzee kimaro wakaupeleka hadi ndani ya chumba kimoja.ย
Wakautia mwili huo kwenye moto mkali uliokua ndani ya Pipa moja kubwa, wakaufunikaย humo ili kuupoteza mwili na mabaki yake, Maisha ya Mzee Kimaro yakaishia ndani yaย Kitengo hicho cha Siri kilicho ndani ya Msitu mmoja.ย
โElizabeth, najua unajua ni kwanini upo hapa, sasa tafadhali usije ukanisumbua. Nipatie M21ย na utando wote unaohusiana na M21โ alisema Bi. Sandra, hata sura ya Mama huyuย ilibadilika, alinyoosha mkono wake ili apatiwe M21. Elizabeth alipokua katika Dudumizi laย maji mazito yenye mateso, ndani ya kile kisima alikutana na Malaika Mtoa roho, kisima kileย kilikua ni zaidi ya shimo refu lenye moto mkali unaowaka bila kupunguza makali, badoย masikio yake yalisikia zaidi sauti za Maji yaliyomtesaย
โUnanisikia?โ akafoka Bi. Sandra, akaitoa sauti yake kali aliyokua akiificha muda wote, sautiย iliyopasua ngoma za Masikio ya Elizabeth. Kisha Bi. Sandra akamwambia Elizabethย
โVita vyote umevipigana ukiwa ndani ya hilo dela? Najiuliza mengi yasiyo na majibu kuhusuย wewe, ni Jasusi kutokea wapi?โ Bi. Sandra akazidi kumchimba Elizabeth lakini ukimya wakeย ulimjaza hasira akampa kibao kikali kilichomkwarua shavu lake la kulia kwa pete ya Bi.ย Sandra. Damu nzito ikamvuja mdomoni Elizabeth, kwa hasira akamtusi Bi. Sandraย
โMalaya weweโ alisema kwa hasira sana, haraka Bi. Sandra akaagiza Elizabeth ateswe zaidiย ndani ya Jengo hilo la siri. Mateso Makali yalimfanya apige ukunga ambao uliwafanya ndegeย walio karibu na Jengo hilo kuruka.ย
**ย
Mwili wa Rais Mbelwa ukawekwa kwenye Jokofu ndani ya eneo lake la siri la mateso, badoย siri ya kifo cha Rais ikabaki Ikulu, hakuna Mtu aliye nje ya Ikulu aliyeifahamu siri hiyo, hataย viongozi wengine wakubwa wa Serikali hawakuweza kuitambua siri hiyo, walinzi woteย waliokua wakiilinda Ikulu waliondolewa, Waziri Mkuu Haji Babi akaweka walinzi wapyaย kutoka Kitengo cha Black Site.ย
Upande wa pili, Muhonzi alikua akiteseka ndani ya Godauni, Zagamba alimshikilia ili aipateย Nyaraka M21 kutoka kwa Elizabeth, Alikua ndani ya chumba kimoja chenye dirisha dogoย tena liko juu sana, hewa ilikua nzito lakini kibaya zaidi alipaswa kujisaidia ndani ya Chumbaย hicho, Mikono yake ilifungwa kamba ili asifanye ujanja wowote ule.ย
Akili yake ilishashtuka mapema kua kuna lililompata Elizabeth ndiyo maana Zagamba alikuaย mwenye hasira sana, tumaini la yeye kuendelea kua hai aliliona kua finyu kabisa, akaanzaย kutafuta namna ya kujisaidia hapo ili aweze kuokoa uhai wake.
Kabla hajafanya chochote akakumbuka tukio moja… Ni Tukio Gani? Usikose SEHEMU YA ISHIRINI NA TATUย
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost MSALA Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
MSALA xx MSALAxx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA
12 Comments
Leo wa kwanza nilikua nimeisubili kwa hamu kweli kweli
๐ฅ๐ฅ๐ฅ
Mambo ni faya hongera sana mwandishi Kwa uandishi mzuri na utunzi wa story Yako
Well done
Good
Winnie mambo vp?
Duuu!! Mbona kikosi Kazi kutoka mapogoro hakifiki ninaugwadu admine
Admin mitano tena ๐๏ธ
Admini upewe maua yako sema tunaomba ziwe zinatoka mbili
Admin chukua maua yako ๐น๐น๐น๐น๐น
Well done
Story tam lakin Bora zitoke mbili kwa siku