Nafiriki tunavyoendelea kukuuza huu mjadala tunazidi kumchanganya mchezaji, tungechagua kunyamaza ili tumsaidie Dickson Job nadhani tutakuwa tumechagua njia sahihii.
Siyo yeye aliyeachwa kwenye kikosi cha Stars yapo majina makubwa kama Shomari Kapombe na tumekubali, vipi Mbwana Samatta aliyeomba kutokuitwa pengine ndio ungekuwa mjadala mzuri zaidi kuliko huu ambao unaendelea.
Kama watu wake walishatolea ufafanuzi kuhusu hili sasa kwanini tunaendelea kuhoji hili, nani mfaidika au nani muathirika, jibu ni mchezaji mwenyewe. Kwanini tumchonganishe na Viongozi wa soka kupitia hili, tufunike kombe Mwanaharamu apite zake ndugu zangu.
Kila kitakachochambuliwa kuhusu Job kwasasa itakuwa ni kama tumechagua upande wengine Kwa mchezaji wengine Kwa ile kamati iliyoamua kumpumzisha juu ya yeye kuitumikia Taifa Star. Kumsaidia mchezaji ni kuachana na mijadala ya namna hii. Hapo mbele kuna mechi kubwa tu dhidi ya Mamelodi Sundown, nadhani kwake ndio jambo kubwa kuliko hili.
Kama tunaamua kumzushia mchezaji tusitumie nyingine ya namna hii, yaani Dickson Job aitwe timu ya Taifa kisha akatae eti kuambiwa atacheza full beki. Binafsi nitakuwa mtu wa mwisho kulikubali hili.
Kwanza lazima tuangalie nani anashirikiana na kocha Adel Amrouche katika kuita wachezaji kwenda kuitumikia timu ya Taifa, hapa inaweza kutusaidia kujua nini tatizo.
Kwa kiwango cha beki wa kati kwa sasa, kama Ibrahim Bacca, basi ni Dickson Job kwa wachezaji wazawa, ndio yupo kepteni Bakari Mwamnyeto lakini ni kama kiwango chake kimeshuka kiasi.
Tuendelee kuwapigia kelelee watu ambao wamekuwa wakifanya machaguo ya wachezaji wawe wanaangalia umuhimu na uhitaji kwenye kikosi cha Taifa Star siyo tu kuita wachezaji kwasababu una maslahi nao.
Tumsaidie mchezaji tusimdidimize.
SOMA ZAIDI: Barua Ya Wazi Kwako Dickson Job “Big Brain Defender”
3 Comments
I do not even know how I ended up here but I thought this post was great I dont know who you are but definitely youre going to a famous blogger if you arent already Cheers.
Hi i think that i saw you visited my web site thus i came to Return the favore Im attempting to find things to enhance my siteI suppose its ok to use a few of your ideas
Pingback: Kwa Matukio Haya TFF Na Bodi Ya Ligi Mjitafakari - Kijiweni