Wachezaji wengi walipaswa kumchukua MKUDE kisha kulifanya darasa huru huyu kwani ni mchezaji wa pekee sana na sijawahi kuwaona wachezaji wa namna hii kwa kipindi kidogo, mwamba alisaini mwaka mmoja Yanga SC kutokea Simba SC.
Nungunungu kama wanavyomuita alikubali mkataba wa mwaka mmoja ndani ya Yanga SC wala kwake halikuwa jambo gumu hata kidogo, Jonas Mkude anasaini vipi mkataba wa mwaka mmoja huku akiwa ametokea kwenye timu ambayo status yake kubwa kama hii ya Yanga?
Maisha ya Mkude ndani ya Yanga ni ya kuvutia sana, kama ikitokea kocha amempa nafasi ya kucheza ni sawa na isipotokea ni sawa pia kwake kwasababu hakuna maneno. Kukaa benchi kwa mchezaji mkubwa kama yeye siyo jambo dogo lakini amechagua kukubali matokoe na hivi ndivyo mchezaji unapaswa kufanya.
Ondoka yake Simba SC inaweza kuwa rahisi kurudi kwani hakuna KERO wala chuki ameipandikiza, hajawahi kuwakera watu wa Msimbazi kwa namna yoyote ile, ni ukimyaa na upole tu. Leo ukitaja Legend wa Simba SC huwezi kuliacha jina la Jonas Gerald Mkude Nungunungu, huu ni ukweli ambao upo wazi kabisa.
Ni muda sahihii kwa wachezaji wengine kujifunza namna ya kuzihama timu zao, ukiondoka kwenda sehemu nyingine basi unachagua NIDHAMU siyo majigambo kwani hiyo haitakujenga hata kidogo bali itakuharibia sifa yako maishani mwako. Mkude ni kioo kwa wanaomtazama.
Bila shaka yoyote sitoshangaa kusikia akiongezewa mkataba mwingine ndani ya Yanga SC, nidhamu, kujituma hivyo vyote vinampa uhalali wa yeye kuendelea kuitumikia Yanga SC. Kila la kheri kaka Yanga SC ichukue iwe yako tembea nayo kaka itakufaa sana.
SOMA ZAIDI: Wachambuzi Wanamuingiza Feitoto Kwenye Chuki
7 Comments
Ni kweli mtupu haina kupingwaaaa
Bwana Bwana Bwana Bwana ଆପଣାଆପଣା
Huyo ndiye mtu pekee anayejua thamani yake na utu wake na sio kujidhalilisha na kuwadhalilisha wengine kwa kujivuna
Ngoja nimtumie Link ya kijiweni yule mtoto wa michenzani kizmkazi unguja kwa machupa aje asome darasa huru 🤢
Ukimya ni silaha
Alijua kutafuta jinsi ya kuvaa medali
💪💪🤗
Kabisa ukiskia mchezaji anaueshem mpira ndo vitu anavyo onyesha mukude ni vyema wachezaji wenzake kujifunza