Timu yoyote duniani inahitaji mchezaji ambaye anarahisisha kazi za timu kiwanjani kwa wenzake hata kwake binafsi basi Clatous Chama anarahisisha kazi za wenzake pale Msimbazi.
Benchikha aliwahi kusema Clatous Chama ni jini kabisa wa mpira kwani sifa zake kiwanjani ndizo zinampa majukumu kwanza ukiangalia namna anavyotoa pasi zake hurahisisha hatua inayofuata kwa wenzake (Counter Movement)
Simba kuna wakati wanakuwa wakiwa na mpira utawaona 3-1-5-1 ambapo anapata leseni ya kushambulia kutoka pembeni zaidi na kuingia ndani, huangalia njia za kupita na kutumia nafasi kupita kwakuwa ni mchezaji anayeweza kukokota mpira vyema na ni bora sana kwa sasa.
Nafikiri Benchikha anamjua zaidi Chama kuliko Mimi, atakuwa na njia nzuri ya kumpa leseni ya mafanikio kwa mechi zifuatazo kupitia Chama na wenzake kwani pasi moja ya Chama ni hatari na inaweza kubadili mchezo, maamuzi sahihi na akili yenye kasi zaidi kwenye mpira.
SIFA ZAKE
1: Dribbler (anajua kupiga chenga: kushinda 1v1 za mabeki kwa ufanisi wa akili na mwili )
2: Passer (anajua kutengeneza njia ya kupita kwa mpira, kutumia nafasi kupitisha mpira : pasi fupi na ndefu )
3: Ni slow lakini sio speed sana (suala hili humpa one touch power la kulisogelea lango la mpinzani juu ni kuathiri vitendo vya kiufundi)
Cha kuzingatia zaidi ni kwamba Clatous Chama anajua jinsi ya kuungana na wenzake wakati wa utulivu na kupita nyuma ya mpinzani ili kushinda mipambano : suala hilo huwa na adhari kwa mpinzani na kuwafanya attack wenzake kuwa deadly mita 20 ya mwisho
SOMA ZAIDI: Kuhusu IHEFU Na Umiliki Wa Siri, TFF Mnaniwazisha Mno
1 Comment
Pingback: Yanga Akimfunga Mamelodi Kwa Mkapa Anafuzu Nusu Fainali - Kijiweni