Manchester City imeandikisha mafanikio makubwa katika msimu wake wa hivi karibuni, ikipata mapato na faida kubwa kuliko wakati wowote ule.
Mapato yao ya £748.2m yanaizidi rekodi ya Manchester United ya £648.4m iliyowekwa mwezi uliopita na inawakilisha ongezeko la £99.8m ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Faida ya City ya £80.4m imepanda kutoka rekodi ya awali ya klabu ya £41.7m mwaka uliopita.
Matokeo haya yanajiri baada ya msimu ambao walikuwa klabu ya pili ya England baada ya Manchester United mwaka 1999 kushinda Premier League, FA Cup na Champions League.
Mapato haya bado ni chini ya €990m (£861.43m) Barcelona iliyorekodi mwaka 2019, ingawa uhalali wake umekosolewa kutokana na jumla ‘isiyotarajiwa’ iliyochanganywa na mapato yao.
Mwenyekiti wa City, Khaldoon al-Mubarak, alisema, “Baada ya ushindi wetu wa Champions League huko Uturuki na kukamilisha ‘The Treble’, swali nililoulizwa mara nyingi zaidi lilikuwa, ‘Vipi mnaweza kuzidi hilo?’ Jibu ni kwa kuzidisha falsafa na mikakati iliyothibitika ambayo imetuletea mafanikio haya na kujiwekea changamoto ya kuendelea kubuni daima ili kufikia viwango vipya vya ufanisi, uwanjani na nje ya uwanja.”
Aliongezea kusema, “Tutaendelea kuhoji viwango vyote vya tasnia, kutathmini mafanikio yetu na kujifunza kutokana na mapungufu.
“Mafanikio leo yanamaanisha uwekezaji zaidi kwa kesho. Afya yetu kifedha na mafanikio uwanjani yanamaanisha kila mtu aliyeunganishwa na Manchester City anaweza kutazamia kwa hamu ya siku zijazo. Mafanikio yetu pamoja yaninipa uhakika mkubwa kwamba pamoja tunaweza kufanikisha mengi zaidi miaka ijayo.”
Mapato ya matangazo yaliongezeka kwa 20.2% hadi £299.4m, ikiwa ni “haswa” kutokana na mafanikio yao katika Champions League na FA Cup.
Ripoti pia inataja “hatari na kutokuwa na uhakika ambao unaweza kuwa na athari kubwa kwa utendaji wa klabu” ikiwa ni pamoja na utendaji wa kikosi cha kwanza, mabadiliko ya sheria, na mashtaka 115 ya kifedha yaliyotolewa dhidi yao na Premier League mwezi Februari.
City walituhumiwa kwa kukiuka sheria za kifedha za ligi kuanzia 2009 hadi 2018 na pia kutofuata ushirikiano tangu uchunguzi ulipoanza Desemba 2018.
Tume huru inayosimamia kesi hiyo inaweza kutoa adhabu ikiwa ni pamoja na faini, kupunguzwa kwa pointi au kutolewa nje ya Premier League.
Klabu hiyo daima imekana kufanya udanganyifu wa kifedha.
“Mwezi Februari 2023, kujibu mashtaka, klabu ilitoa taarifa ya umma kwamba inakaribisha ukaguzi wa suala hili na Tume huru, kuchunguza kwa usawa ushahidi kamili uliopo kwa kusaidia msimamo wake,” ripoti hiyo inasema.
Gharama za mishahara ya City zilipanda kwa karibu £70m hadi £422.89m na klabu imetenga zaidi ya £262m katika “ada za uhamisho, ada za kusajili na bonasi za uaminifu” ikiwa hali fulani zitatimizwa.
Klabu ilipata faida ya £121.7m katika biashara ya wachezaji katika mwaka wa kifedha wa 2022-23 na inasema jumla ya uhamisho uliofanyika baada ya tarehe 30 Juni 2023, ambao ulijumuisha kuwasili kwa Jeremy Doku, Mateo Kovacic, Josko Gvardiol na Matheus Nunes, pamoja na kuondoka kwa Cole Palmer, Riyad Mahrez, Aymeric Laporte na James Trafford, uligharimu klabu takriban £84m.
Soma zaidi: Habari zetu kama hizi hapa