Tarehe 13/01/2024 bila shaka ni siku inayosubiriwa kwa hamu kubwa sana na mashabiki wa soka barani Afrika kwa lengo kubwa la kutazama timu zao za Taifa zikimenyana kumtafuta bingwa wa kombe la mataifa barani Afrika (AFCON) kwa msimu wa mwaka 2023 itakayofanyika nchini Ivory Coast huku kila timu ya taifa ina kocha ambaye anaandaa mbinu zake kwa ajili ya kuchukua ubingwa huu na hapa tutazame orodha ya makocha watano bora wanaopokea pesa ndefu zaidi kufundisha timu za taifa katika michuano ya AFCON msimu huu.
- HUGO BROOS (AFRICA KUSINI)
Kocha huyu kutoka Ubelgiji aliwahi kushinda AFCON akiwa na kikosi cha Cameroon mwaka 2017 na amekuwa akihudumu kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Afrika Kusini tangu 2021 huku mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2026, lakini hajawahi kuipatia timu hiyo taji lolote.
- WALID REGRAGUI (MOROCCO)
Ni miongoni mwa makocha bora barani Afrika kati ya makocha waliofanya vizuri kwenye Kombe la Dunia
mwaka juzi nchini Qatar akiifikisha nusu fainali Morocco, Walid anakunja Euro 60,000 kwa mwezi na ana mkataba wa kuifundisha Morocco hadi 2025.Mbali ya fedha pia ni mmoja kati ya makocha tishio wanaotarajiwa kuwepo kwenye mashindano ya mwaka huu.
- RUI VITORIA (MISRI)
Huyu ni mmoja kati ya makocha bora kutoka Ureno ambaye mfukoni mwake ana medali za ubingwa wa ligi nchini humo mara mbili. Kocha huyu ana mkataba wa kuitumikia Misri hadi mwaka 2026, na aliajiriwa mwaka 2022. Analipwa Euro 200, 000 kwa mwezi
- JEAN-LOUIS GASSET (IVORY COAST)
Wenyeji wa michuano hii nao si haba kwani kocha wao wanamlipa kiasi cha Euro 108,00 kwa mwezi akiwa na rekodi ya kushinda mechi 9 akisare michezo 3 na kufungwa mechi 2 kati ya mechi 14 alizoisimiamia timu hiyo toka mwaka 2022.
- DJAMEL BELMADI (ALGERIA)
Kocha huyu ambaye ni raia wa Algeria ndiye anaongoza kwa kuwa na mshahara mkubwa zaidi kwenye mashindano hayo. Mshahara wake wa Euro 208,000 kwa mwezi ameanza kuupokea tangu 2018 alipochukua mikoba ya kuifundisha timu hiyo. Belmadi ameisaidia nchi hiyo kushinda taji moja la Afcon mwaka 2019 na pia aliwahi kuifundisha timu ya taifa ya Qatar. Pia aliwahi kuchukua tuzo ya kocha bora wa mwaka wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) 2019.
Endelea kusoma zaidi kuhusu AFCON kwa kugusa hapa.