Ilipoishia “Ndani ya masaa matano Desmond alifanikiwa kufika Kijijini hapo.
Alikijua vizuri kijiji hicho sababu yeye ndiye aliyemfuata Sanga akawe mfanyakazi, alivalia kofia kisha alishuka kwenye gari yake, mbele aliona gari yenye nembo ya polisi hivyo alitambuwa fika kuwa polisi walikuwa wameshafika eneo hilo, alijitahidi kutembea kwa tahadhari huku macho yake yakiangaza huku na kule, bahati ilioje kabla hata hajafika nyumbani anakoishi Sanga alimuona Sanga akiwa amejificha sehemu, hapana shaka hata Sanga alihitaji kuwakwepa askari hao. Macho ya Sanga na Desmond yaligongana kisha haraka Desmond alienda hadi alipojificha Sanga
“Umefanya nini Sanga?” Alihoji Desmond akiwa amejificha hapo na Sanga. Endelea
SEHEMU YA TATU
“Ndiyo Desmond! Uchunguzi unaendelea hivyo ni lazima tutoe taarifa kila hatua” Alieleza askari huyo kwa njia ya simu, Desmond alitamani kumwambia Askari huyo asirushe chochote lakini alishindwa sababu angeulizwa kwanini anataka taarifa zisiruke alafu angekosa jibu la kumpa, alikata simu akairudisha kwenye mfuko wake.
Siku zilienda, Desmond na Noela walipanga kuvishana pete ya uchumba ili mahusiano yao yatambulike, japo Desmond alikuwa na Mke tena aliyefunga naye ndoa kanisani ila hakutaka kusema chochote kile, akili yake ilizidi kumwambia kuwa Mandy atakufa muda wowote ule, walipanga siku ya tukio hilo, hofu ya Desmond ikawa kwa Lucia kama atapewa hiyo taarifa alafu akahudhuria sherehe hiyo fupi ya kuvishana pete na kama unavyojuwa Lucia alikuwa akifahamu kuwa Desmond ana Mke tena yupo Hoi Hospitalini.
Miongoni mwa Watu ambao Noela aliwaarika alikuwa ni Lucia sababu alikuwa ni rafki yake wa zamani, Desmond alimwambia Noela hana sababu ya kuarika Watu wengi hivyo sababu ni sherehe fupi ambayo inawahusu wao na baadhi ya ndugu.
“Sijawahi kuvishwa pete katika Maisha yangu Joshua, wewe ndiye Mwanaume wangu wa kwanza kunipeleka kwenye ulimwengu huu hivyo ni fahari kwangu kuona marafiki zangu wanakuja hapa” Alisema Noela siku moja baada ya Desmond kulalamika kuwa anaarika Watu wengi.
“Najuwa Mpenzi wangu lakini tukio hili ni la kushuhudiwa na Watu wachache sana, Aaah…” Alisema Desmond huku bado akitafunwa na hofu ya Lucia kuarikwa
“Joshua nimearika marafiki wachache sana, usiwe na wasiwasi kuhusu hilo. Nakuelewa Mume wangu mtarajiwa” Alisema Noela kisha alisema
“Naenda chooni mara moja” Aliaga kisha aliondoka lakini aliacha Kitabu chenye majina ya Watu walioarikwa kwenye shughuli hiyo, haraka Desmond alikifunua, kama alivyofikiria ndivyo ilivyokuwa, Lucia aliarikwa kwemye shughuli hiyo, jina lake lilikuwa la tatu kutoka juu akimaanisha kuwa ni miongoni mwa Watu muhimu zaidi kwake, kijasho kilimtoka Desmond, alifikiria haraka haraka afanye nini ili kumzuia Lucia asiende kwenye tukio hilo la kuvishana pete maana kama Lucia ataenda basi mambo mawili yatajulikana, kwanza ni jina lake halisi ambalo siyo Joshua na pili ni kwamba ana Mke hivyo haruhusiwi kuowa Mke mwingine kwa mujibu wa sheria za dini ya Kikristo.
Walikuwa kwenye moja ya Bustani nzuri wakizungumza, Desmond alikaa kwenye kiti akiwa amechoka mwili na akili, akakumbuka Maswali aliyoulizwa na Lucia juu ya jaribio la kutaka kuuawa kwa Mandy, moja kwa moja alijuwa mambo mengi yanaenda kujulikana kama ataruhusu Lucia kuwepo kwenye Shughuli hiyo, akiwa anaendelea na tafakari Noela alirudi akamkuta Desmond akiwa katika hali ya mawazo sana
“Kulikoni Bebe?” Alihoji, kijasho kilikuwa kikimtoka Desmond, Noela alimpa kitambaa Desmond ili ajifute jasho
“Unaumwa?” Aliuliza tena Noela
“Ndiyo ghafla tu sijisikii vizuri, usijali nitakuwa sawa” Alisema Desmond kisha alijifuta jasho alafu akashushia maji ya baridi, Noela aliketi, aliona kitabu kimefunguliwa
“Au kwasababu umeona nimearika idadi kubwa ya Watu Joshua?” Aliuliza Noela akiwa mwenye wasiwasi huwenda Desmond ana hasira
“Hapana Noela ni tofauti na ufikiriavyo, ni ghafla tu najisikia vibaya” Alisema Desmond, Noela alisema
“Ngoja nimpigie rafiki yangu ni nesi”
“Rafiki yako nesi?” Alihoji Desmond akiwa katika hali tofauti kabisa hata Noela alishangaa maana Mtu ambaye alionekana kuwa na hali mbaya
“Mbona umeshtuka sana niliposema nampigia rafiki yangu nesi? Si wewe ulikuwa katika hali ya homa?” Kiukweli Noela alizidi kumshangaa Desmond
“Hukuwahi kuniambia kama una rafiki yako Nesi” Alisema Desmond, Noela alitabasamu akagundua ni kweli hakuwahi
kumwambia Desmond istoshe alikutana na rafiki yake huyo siku chache zilizopita
“Oooh ni kweli, ni rafiki niliyesoma naye. Tulipotezana muda mrefu sana ni majuzi tu ndiyo tumeonana. Hata hivyo nimemuarika kwenye shughuli yetu lakini nakumbuka kama niliwahi kukwambia, atakuja utamuona anaitwa Lucia” Alieleza Noela kisha alimpigia Lucia lakini kabla hata simu haijaita Desmond alimkatisha Noela
“Huna haja ya kumsumbua nitakuwa sawa tu” Alisema Desmond huku akitafakari kuhusu Lucia, aliona wazi vita kubwa inaenda kupigwana mbeleni
“Hivi unajua Joshua sikuelewi, unatokwa jasho namna hiyo lafu hutaki nimuite Lucia?” Aliuliza Noela
“Nimesema nitakuwa sawa, tunaweza ondoka hapa” Alisema Desmond kisha alisimama, Noela naye alisimama japo kwa kuchukia kisha waliongozana hadi kwenye gari ya Desmond, walianza safari ya kuondoka pale kuelekea nyumbani anakoishi Noela, baada ya kumaliza mizunguko yote alirudi kwenye nyumba aliyokuwa akiishi na Mandy.
Kuna dokumenti alizihitaji akaenda kufungua kabati la Mandy ambalo alikuwa akiweka baadhi ya vitu vyake muhimu kisha alitoa Mkataba wenye umiliki wa Mali za Mandy yakiwemo Mashamba, kampuni ya Kuuza Vipuri vya Magari na Mgodi mmoja.
Alipozipata nyaraka hizo muhimu alizipitia, alithibitisha ndizo alizokuwa akizihitaji kwa wakati huo, kisha alimpigia Mtu mmoja simu akasema
“Joel ninazo, nakuja ofisini kwako” Alisema Desmond kisha alikata simu, aliingia kwenye gari akaelekea kwa Joel ambaye alikuwa ni Mwanasheria wa Mandy.
Alifika ofisini kwa Mwanasheria huyo aliyeitwa Joel, alikuwa ni Mtu makini aliyefahamu kilichotokea kati ya Mandy na Mume wake Desmond, walitazmana huku nafsi zao zikizungumza, walionesha kujuwa hasa walichodhamiria kufanya. Haraka Desmond alizama kwenye mkoba wake akatoa zile nyaraka muhimu za Mandy.
Joel aliketi akazipitia kisha akamwambia Desmond baada ya dakika kadhaa za ukimya kupita
“Ni zenyewe” Alisema hivyo huku akizidi kutafakari jambo, Desmond aligundua kisha akamuuliza
“Unafikiria nini Joel?” Alimuuliza Mwanaume huyo mweupe mwenye mvi kiasi ambaye umri wake ulienda kidogo
“Nafikiria kuhusu Mandy, tunachofanya ni kumzika akiwa hai, nakumbuka mengi ya zamani” Alisema Joel huku akifuta chozi jicho moja
“Wewe ni mshamba sana Joel, hukuzaliwa kuwa masikini. Huoni aibu? Huhisi haya machoni pako? Mwaga wino hatukuanza leo” Alisistiza Desmond huku akizidi kumshangaa Joel, basi Joel alichukua peni akaiweka juu ya nyaraka hizo akamwambia Desmond
“Hiki ninachokifanya kinaenda kubadili kila kitu katika Maisha yangu, uadilifu na uaminifu wangu kwa Mandy unazikwa baada ya kutia saini nyaraka hizi Desmond. Natamani kurudi nyuma na kuzuia hili lisitokee” Alisema Joel huku akizidi kujilaumu
“Mandy ni wa leo wa kesho, unataka afe ili nihangaike na familia yake si ndiyo?” Alisema Desmond kisha alimlazimisha Joel kutia saini ya makubaliano kuwa Mandy amempa mali hizo Mume wake Desmond, kwa Mamlaka aliyonayo Joel alitia saini
“Ooooh!! Sasa umefanya kwa upande wako, kilichobakia ni kule Hospitali, twende tukamalize mchezo” Alisema Desmond kisha alisimama
“Desmond una uhakika kuwa Mandy atakufa?” Joel aliuliza
“Asipokufa atakuwa na mapungufu kwenye ubongo wake, ni lazima atapoteza kumbukumbu tu” Alisema Desmond kwa kujiamini
“Baada ya hapa nitakupatia kiasi kikubwa cha pesa kisha utakuwa na jukumu la kuitunza siri hii” Alisema Desmond kisha walitoka wakaelekea kule Hospitalini.
Walipofika walimkuta Lucia akiendelea kumuangalia Mandy maana ndiyo jukumu lake kuu alilopewa, Lucia aliwatazama Desmond na Joel Mwanasheria.
“Samahani Lucia kuna jambo Mwanasheria wa Mandy amekuja kufanya” Alisema Desmond, Lucia alishtuka akamuuliza Desmond
“Unahisi Mandy hatoweza kuamka?” Alihoji akiwa kama muuguzi namba moja wa Mandy, alihisi kuna jambo lisilo la kawaida ndiyo maana Mwanasheria huyo alienda Hospitalini. Desmond alimvuta pembeni Lucia akamwambia
“Siyo kila jambo linaendeshwa kimihemko Lucia, mambo mengine unapaswa kuyaangalia tu. Wewe ni nesi na utabakia kuwa nesi” Alisema Desmond kwa sauti iliyojaa ukomavu huku akiwa amemshika mkono kwa nguvu Lucia
“Hata kama Desmond, nimemungalia Mke wako kwa kipindi kirefu. Lipo tumaini ndani yake, kuwa na subra” Alijibu Lucia
“Unajuwa nini wewe Lucia? Unajuwa nini kuhusu familia yangu!? Kumuuguza Mandy ni jukumu lako sababu unalipwa msharaha hufamyi bure hapa” Alisema Desmond kwa sauti ile ile
“Desmond! Desmond vuta subra Mkeo ataamka tena” Alisema Lucia akionesha kuumizwa sana, mara nyingi Mtu anapokuwa mgonjwa sana alafu Mwanasheria akaja basi kunakuwa na uwezekano Mkubwa sana kuwa kuna mjadala wa mali za mgonjwa, Lucia aliligundua hilo
Basi Desmond na Lucia walirudi huku Lucia akitaka kusema kitu lakini Desmond hakutaka kumsikiliza Lucia, Mwanasheria Joel alitoa wino kisha alipakaza kwenye kidole cha Mandy. Akaweka saini kwenye zile karatasi, Desmond alikabidhiwa karatasi hizo kisha alizisoma tena, Lucia alichungulia kuona kulikuwa kumeandikwa kitu gani kwenye karatasi hizo.
Aliona maandishi yaliyosomeka
“MAKABIDHIANO YA MALI KATOKA KWA MANDY KWENDA KWA DESMOND”
Alishtuka sana Lucia, alimtazama mara mbili mbili Desmond, jinsi alivyokuwa amemchukulia Mwanzo aliona kabisa alimchukulia tofauti kabisa kwa jinsi alivyo sasa, alimuona Desmond kuwa ni mkatili na jambo ambalo alikuwa analifanya pale lilijaa tamaa za kutosha, alishindwa hata aseme nini. Baada ya kumaliza Desmond na Mwanasheria Joel waliondoka Wodini, Lucia alichoka roho na mwili huku akihisi kabisa viungo havifanyi kazi tena.
Alijikutana akikaa chini taratibu huku akijawa na mshangao mno, aliona kabisa kitendo kile kilifanywa bila ridhaa ya Mandy. Alifuta chozi lake lililoanza kumdondoka kisha alijishangaa ni kwanini alikuwa akilia, alinyanyuka kisha alimtazama sana Mandy, alimuonea huruma. Alitamani aamke ili ashuhudie kilichokuwa kinafanywa na Mume wake, akili ya Lucia ikamwambia
“Basi Desmond anaeeza akamuuwa Mke wake kama ameweza kumsainisha akiwa hoi kitandani basi anaweza akaondoa uhai wake” Akili ya Lucia ilifika ukomo wa kutafakari jambo hilo.
Usiku Lucia aliondoka Hospitalini akiwa hoi Bin taabani, alipitia baa akaagiza pombe akanywa maana jambo lile halikuwa la kawaida hasa kwa Mawanaume ambaye alimpenda ila hakuwahi kumwambia, aliona moyo wake ulikosea njia kisha alijicheka akiwa anaendelea kupata pombe taratibu, kisha baadaye alikodi Pikipiki ikamrejesha nyumbani kwao.
Mama yake alishangaaa sana kumuona Lucia akiwa amelewa kiasi kile, alikuwa amelewa kupita maelezo hata dereva wa pikipiki alimpa tahadhari Mama Lucia kuwa Binti huyo alikuwa amekunywa sana hivyo awe naye makini wakati anampeleka ndani.
Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA NNE
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya kuendelea kutuma SIMULIZI Mpya Na Kuipost HAPA Kwa kumtumia Chochote kupitia
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love &Pain Love & Pain
5 Comments
Nice
Pesa imekuwa adui na katili kupitiliza😥😢
Anyway Asante Kaka Mkubwa kwa stori nzuri yenye mafunzo maumivu ndani yake
More Love from Kenya ❤️
“Kuna mpango mkubwa unaoandaliwa na mataifa makubwa kuirudia na kuigawanya Africa kama walivyofanya katika mkataba wao wa Berlin miaka ya 1884-1885 na mara hii kutaka kuiangamiza kabisa…..
….Hatimaye msichana ambaye ana asili ya kiafrika anayechukua masomo yake katika mojawapo ya mataifa yao anagundua na ANAAMUA KUUZUIA MPANGO HUO!!!!”
Hahahah JE HII ITAKUA ZAIDI YA ILE YA MAYA WA ULAYA???? USIIKOSE HII KITU CHALII YANGU!!!
https://whatsapp.com/channel/0029VanxLVYJ93wbHawAAh3H/665
Like moja hapa kisha follow channel kama bado usiikose hii ….
hivi karibuni usiikose!!!
Mmmmh hatari pesa ni adui jamani
Lucia si achie ubuyu tuu
😆😆😆