Ilipoishia “Usiku Lucia aliondoka Hospitalini akiwa hoi Bin taabani, alipitia baa akaagiza pombe akanywa maana jambo lile halikuwa la kawaida hasa kwa Mawanaume ambaye alimpenda ila hakuwahi kumwambia, aliona moyo wake ulikosea njia kisha alijicheka akiwa anaendelea kupata pombe taratibu, kisha baadaye alikodi Pikipiki ikamrejesha nyumbani kwao.
Mama yake alishangaaa sana kumuona Lucia akiwa amelewa kiasi kile, alikuwa amelewa kupita maelezo hata dereva wa pikipiki alimpa tahadhari Mama Lucia kuwa Binti huyo alikuwa amekunywa sana hivyo awe naye makini wakati anampeleka ndani. Endelea
SEHEMU YA NNE
“Lucia kwanini umekunywa hivi Mwanangu jamani” alisema Mama Lucia akiwa anamuingiza Lucia ndani, alimpeleka hadi chumbani Kwake, alimuweka kitandani
“Lucia umepatwa na nini leo? Sijapata kukuona ukiwa umekunywa kiasi hiki” Alisema Mama yake Lucia huku Lucia akiangua kicheko kisha alisema kwa ulevi
“Ukiwa mzima kila Mtu atakupenda lakini kosa lako uumwe au ufe, kila Mtu atakuwa adui wa Maisha yako Mama” Alisema Lucia kisha alibeuwa kidogo, Mama yake alitamani kufahamu ni kwanini Lucia alisema hivyo
“Kwanini unasema hivyo?” Alihoji Mama Lucia
“Mama sisi Binadamu ni wabaya sana, tunacheka mbele kisha nyuma tunanuna ha!ha!ha!” Alisema kisha alicheka lakini Mama Lucia alihisi Mtoto wake pengine amekutana na jambo zito sana, ni kweli Lucia alikutana na janbo zito mno
“Pumzika Lucia tutaongea kesho” Alisema Mama Lucia kisha alitoka chumbani humo, baada ya Mama kutoka Lucia alichukua simu yake akampigia Noela, alihitaji msaada kutoka kwa Noela
Wakati simu hii inapigwa usiku huo, Noela alikuwa amelala na Desmond, Mara moja Noela alishtuka akaipokea huku akiwa mwingi wa Usingizi
“Hello?” Alisema Noela kwa sauti ya Usingizi, Desmond alikuwa amelala
“Noela nahitaji msaada wako” Alisema Lucia
“Msaada gani huo?” Aliuliza Noela huku akinyanyuka kitandani na kwenda dirishani ili tu asimpigie kelele Desmond
“Nataka msaada wa kisheria kwa mgonjwa wangu…ipo hivi….” Lucia alimuelezea Noela alichotaka kusaidiwa
“Hivi una uhakika na unachokisema? Unaonekana umelewa sana kwanini tusiongee kesho hili jambo?” Aliuliza Noela, Lucia alikubali kuzungumza na Noela kesho yake.
Simu ilikatika, kwa Mshituko Noela alipogeuka alimuona Desmond
“Eeeeh Joshua umeamka?” Alihoji Noela kwa mshtuko maana hakutegemea kama angemkuta akiwa amemsimamia nyuma
“Ulikuwa unaongea na nani?” Aliuliza Desmond
“Aaah ni mteja wangu alikuwa anahitaji msaada wa kisheria, usijali Mpenzi twende tukalale” Alisema Noela, hakujuwa kama msaada alioombwa na Lucia ulimuhusu Mtu aliyekuwa naye Usiku huo, Ndiyo!! Lucia alihitaji msaada wa kisheria kwa Mandy maana alichokiona pale kilimtisha sana.
Asubuhi mapema sana Lucia alienda Hospitalini kama kawaida yake, safari hii alikuwa makini zaidi na Mandy maana alijuwa kuna jambo linachezwa nyuma ya ufahamu wake, alitembea taratibu akizunguka kitanda cha Mandy huku akijiuliza afanye nini kuzuia jambo hilo kutokea au kuwa baya zaidi. Alipata wazo fulani, alimfuata Daktari Mkuu wa Hospitali akamuomba Mandy aongezewe Huduma zaidi ili kuharakisha afya yake irejee kama mwanzo maana ilionekana kuwa na uwezekano wa Mandy kupona japo haikujulikana atapona lini licha ya wasiwasi kuwa hata kama kiamka hatoweza kukumbuka chochote au anaweza kukumbuka lakini akawa hawezi kuzungumza wala kufanya chochote kile.
“Kwanini umekuja kuniomba kuhusu hilo jambo?” Aliuliza daktari Mkuu wa Hospitali
“Ni jukumu langu Kuhakikisha Mandy anakaa sawa haraka kuliko ilivyo dhaniwa, naomba sana” Alizidi kuomba Lucia
“Aah Lucia hilo jambo ni lazima tumshirikishe Mume wake, kama unavyojuwa yeye ndiye msimamizi wa kwanza wa Mandy” Alisema Daktari huyo
“Hakuna haja ya kumuleza Desmond kuhusu hili jambo, naomba asijuwe chochote kile” Alisema Lucia na kumfanya Daktari ashangae, akamuuliza
“Kwanini hutaki ajuwe?” Nani atazilipa hizo gharama za ziada?” Aliuliza
“Kumbuka Mandy ni mfanyabiashara mkubwa sana hivyo akiamka atalipia hizo gharama” Alisema Lucia katika hali ya kuendelea kumuomba daktari akubali.
“Asipoamka?” Aliuliza Daktari
“Jukumu letu namba moja ni kuhakikisha wagonjwa wanapona, ni lazima tufanye juu chini kuhakikisha tunasaidia Maisha yake” Alisema Lucia akiwa anamtazama Daktari huyo ambaye alionekana kuanza kumuelewa kidogo Lucia
“Nakuamini Lucia usiniangushe katika hili, nitafanya kama unavyosema” Alisema Daktari huyo, Lucia aliweka mikono mdomoni kwa furaha kisha akasema
“Asante sana Mkuu! Umenipa thamani kubwa sana” Alisema Lucia kisha alimuaga Daktari akaondoka zake, daktari huyo alikuwa Mzee na ilionesha ndiye mmiliki wa Hospitali hiyo
“Aaah” Alisema Daktari kisha alipiga simu alipopajua yeye akatoa maelekezo ya Mandy kupelekwa hatua ya pili ya matibabu.
•••••••
Baada ya siku kama tatu kupita ilipatikana taarifa kutoka kwa Askari polisi aliyekuwa akifuatilia kifo cha Mama Mandy, polisi huyo alimpigia simu Desmond akamwambia kuwa kuna gari iliyopatikana kwenye Bahari, gari hiyo ilikutwa na maiti ya Mtu. Desmond alichanganikiwa, alikuwa ofisini kwake akamuuliza polisi huyo
“Gari! Maiti! Imefahamika gari ni ya nani na maiti ya Nani?” Alihoji Desmond akiwa amesimama huku macho yakiwa yamemtoka pima, alijuwa tu ni ile gari yake aliyomuulia Sanga, haraka akiwa anasubiria jibu la Polisi huyo alijiuliza kama gari ile ikitambulika kuwa ni yake itakuwaje?
“Bado maiti imechukuliwa lakini kimekutwa kitambulisho cha yule mfanyakazi wako ambaye alikuwa ni mhisiwa namba moja wa Tukio la Mke wako ila mwili ulikuwa umeharibika hivyo imekuwa ngumu kumtambuwa kwa macho. Mwili unafanyiwa vipimo kubaini ni Nani” Alisema Polisi huyo
“Vipi kuhusu gari imejulikana kuwa ni ya Nani?” Aliuliza Desmond kama Mtu mwenye haraka ya kutaka kujuwa, polisi hakutia shaka sababu aliamini Desmond alihitaji kufahamu sababu Mandy ni Mke wake pasipo kujuwa Desmond ndiye aliyesababisha kila jambo na alikuwa akiwapiga changa askari ili wasijuwe chochote kile, hata huyo Sanga aliyekuwa akitafutwa ni yeye ndiye aliyemuuwa Hapo Baharini kwa kutumia gari yake.
“Kazi hiyo inafanywa na kitengo husika ili kubaini gari hiyo ilikuwa ni ya nani, ndani ya dakika kumi zijazo tutajuwa gari ni ya Nani pia tutapata taarifa juu ya mwili ule kama ni Wa Sanga au ni wa Mtu mwingine tu” Alisema Polisi huyo kisha alikata simu baada ya kuhakikisha kuwa alizifikisha taarifa muhimu kwa Desmond akiamini ni Mtu mzuri anayepaswa kujuwa kinachoendelea.
Ofisini kwa Desmond hapakukalika mchana huo kila alichofikiria hakikumpa jibu la moja kwa moja, alijuwa ni lazima gari itajulikana kuwa ni ya kwake na polisi watamuhisi kwa namna moja au nyingine jambo ambalo litasababisha aanze kuchunguzwa kuhusu matukio taliyotokea, alizunguka ofisini hapo huku akifikiria afanye nini.
“Oooshit itakuwaje?” Alijiuliza sana Desmond, aliketi akaamka akaketi tena huku akitazama saa ya ukutani, alihesabu hadi dakika kumi alizoambiwa na yule polisi mpelelezi zilipokatika kisha alishika simu yake huku akisubiria simu hiyo iite, punde simu iliita na mpigaji alikuwa ni yule polisi, muda aliosema kuwa atampa taarifa juu ya ule mwili pamoja na gari uliwadia, taratibu aliipokea kisha aliiweka sikioni akiwa amefumba macho yake
“Desmond! Mwili ni wa Sanga mshukiwa namba moja, kesi inazidi kuwa ngumu na kuhusu gari kuna fumbo zito sana hapa ambalo linahitaji umakini hasa ukizingatia gari ile…” alisema Polisi kisha Desmond alidakia
“Ni ya Nani?” Alihoji kwa hofu kubwa sana, ukimya ulitawala huku Desmond akisubiria neno kutoka kwa Polisi huyo, alisema
“Haijulikani, mfumo hauitambui gari hiyo” Alisema Polisi huyo kitu ambacho kilimshangaza sana Desmond, itakuwaje gari yake isitambulike? Kibaya zaidi alikumbuka kuwa hakutoa chochote kwenye ile gari ikiwemo kadi ya Gari kitu ambacho kingekuwa rahisi sana kufahamika, pia alipokuwa akifanya hivyo alijuwa wazi kina kile kirefu hivyo gari haiwezi kuonekana
“Gari haitambuliki?” Alihoji Desmond akiwa na presha
Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA TANO
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya kuendelea kutuma SIMULIZI Mpya Na Kuipost HAPA Kwa kumtumia Chochote kupitia
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOM
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love & Pain Love &Pain Love & Pain
10 Comments
Admin
Ongeza nyingne sahz admin mda umewadia jamani tumepooza sanaaa
Ebwanaeeeh si mchezoooo
Tuma na ingine Admini ooooh ni 🔥🔥🔥🔥🔥
Mbona sijasoma sanga alivyouuawa
Muda umewadia kukikaribisha kiza,jioni ya Leo tutakua na Simulizi zetu mpya Za Sofia Solo pamoja na NEGATIVE PLAN
Bila kusahau vipande vinne vya muendelezo wa Simulizi ya ZEE LA NYWILA,Simulizi isiyotabirika mpaka sasa…
Stay tuned kisha share sambaza upendo kwa uwapendao.
https://whatsapp.com/channel/0029VanxLVYJ93wbHawAAh3H/677
Mbona kama leo fupi san adimin
Nzuri sana🔥
Hee mbona nimesoma kwa dakika mbili leo
Sehemu ya 4 ni fupi hivi!!?
Afu Desmond kumbe alipoenda kijijini kwa kina Sanga kumbe alienda kumaliza uhai wake emmmah😢
Anyway Asante kwa stori nzuri yenye mafunzo na maumivu ndani yake.
More Love from Kenya ❤️
Katiri uyu
Muache awe na presha tuu