Usiku mmoja, Mwanaume mmoja alikuwa akitoka Hospitalini,Β alionekana kwenda hapo kwa ajili ya kumuona Mtu mmojaΒ aliyemfahamu sana tena alikuwa Mtu wa karibu sana kwake.Β Mwanaume huyo alionekana kuwa mwenye mawazo fulani kichwaniΒ pake, alikuwa amevalia koti la suti na jinzi chini akipigiliaΒ raba kali yenye mg’ao.Β
Ilitosha kujiridhisha kuwa Mwanaume huyo alikuwa na hela zaΒ kutosha, tembea yake ilikuwa ya taratibu mno, ukimtazamaΒ vizuri utagundua alikuwa na vita kichwani pake, alipofikaΒ kwenye korido aligeuka na kutazama nyuma kisha alitaja jinaΒ mojaΒ
“Mandy!” Alilitaja jina hilo kisha alihema kiasi, kishaΒ aliendelea mbele kuuelekea mlango wa kutoka Hospitalini hapo.Β Alikutana na nesi mmoja akiwa amebakisha hatua chache kutoka,Β nesi huyo alimuita Mwanaume huyo jina lakeΒ
“Desmond!!” Alipomuita ni kama alimzindua kutoka Mawazoni,Β Mwanaume huyo aliyeitwa Desmond alijichekesha kidogo kabla yaΒ kusalimiana na nesi huyoΒ
“Aaah!! Lucia, Habari yako!” Alisalimia DesmondΒ
“Nzuri mbona una mawazo hivyo au kuna taarifa yoyote mbayaΒ kumuhusu Mandy?” Aliuliza nesi huyo aliyeonesha kumfahamuΒ Vizuri DesmondΒ
“Aaah! Hapana hali yake ipo vilevile, nimechoka tu naΒ majukumu ya hapa na pale” Alisema DesmondΒ
“Pamoja na yote Desmond, wewe ni Mwanaume mzuri sana, unajaliΒ mno maana huishi kuja kumuona Mandy kwa kipindi chote ambachoΒ amekuwa hapa” Alisema LuciaΒ
“Ndiyo jukumu langu, nahitaji kwenda sasa” Alisema Desmond,Β waliagana hapo kisha Desmond aliondoka zake huku LuciaΒ akimtazama Desmond kwa jicho la kuhitaji kumwambia kituΒ lakini alishindwa.
Yalikuwa ni majira ya saa tano za Usiku, muda huo mvuaΒ ilianza kuchapa kidogo na kumfanya Desmond akimbilie kwenyeΒ gari yake, aliondoka Hospitalini hapo Usiku huo huku akiwaΒ kwenye gari alionekana kukumbuka jambo liliomuumiza, sauti yaΒ daktari ilijirudia kichwani pakeΒ
“Mandy anaweza kupata ufahamu ndani ya siku chache zijazo,Β hii ni habari njema Desmond” Alionekana kutofurahishwa naΒ taarifa ya Mgonjwa huyo kuwa sawa, alipiga usukani kwa hasiraΒ kisha alielekea moja kwa moja kwenye jumba lake la kifahariΒ lililopo karibu na fukwe, ndipo alipokuwa akiishi.Β
Alipoingia alitazama ukutani, aliiyona picha aliyopiga yeyeΒ na huyo Mgonjwa aliyeitwa Mandy, mgonjwa huyo alikuwa waΒ kike, picha hiyo ilieleza kuhusu Mandy na Desmond, Naam!Β Walikuwa ni wana ndoa, Desmond aliitoa picha hiyo akaitupaΒ kutoka juu ya ghorofa hilo hadi chiniΒ
“Mandy huwezi kuwa hai tena ni lazima nikumalize” AlisemaΒ Desmond kwa hasira na hisia kali huku akionesha wazi kuwaΒ kulikuwa na jambo ambalo lilijificha kuhusu Yeye na mke wakeΒ huyo aliyeitwa Mandy.Β
Alikunywa pombe sana usiku huo huku simu yake ikiwa bizeΒ kuita lakini hakuipokea kabisa, alikunywa na kulewa sanaΒ akawa hajitambui, alilala hapo sebleni hadi asubuhi.Β
**********Β
Ilikuwa ni asubuhi ya siku iliyofuata, ndani ya ofisi mojaΒ alikuwepo Mwanamke mzuri sana aliyeitwa Noela, Mwanamke huyuΒ alikuwa ni Mwanasheria. Alikuwa akifanya kazi yake hapoΒ ofisini huku akili yake ikionesha wazi kuwa haikuwa naΒ utulivu, mara zote alikuwa akijaribu kupiga simu bilaΒ kupokelewa, baadaye alikuja jamaa mmoja aliyeitwa Zanda,Β walikuwa ni marafiki waliokuwa wakifanya kazi ofisi moja yaΒ Wanasheria wa kujitegemea, mara moja Zanda aligundua NoelaΒ hakuwa sawa aliketi akamuulizaΒ
“Vipi Noela una tatizo?” Alihoji Zanda huku akimtazama UsoniΒ NoelaΒ
“Aaah! Nipo sawa Zanda usijali” Alijibu NoelaΒ
“Noela nimefanya kazi na wewe kwa muda mrefu hivyo nakujuwaΒ vizuri sana, leo haupo sawa” Alisistiza Zanda, NoelaΒ alimkubalia Zanda kuwa hayupo sawa ila ni mambo madogo tuΒ atayatatua.
Baada ya kupita muda kidogo Noela aliondoka ofisini akiagaΒ kuwa anajisikia vibaya. Zanda alimshangaa sana Noela,Β alimkodolea macho akiwa anaondoka na gari yake kishaΒ alitikisa kichwa chake, Noela aliendelea kupiga simu bilaΒ kupokea majibu yoyote yale hadi anafika nyumbani kwao,Β alikuwa akiishi na Mama yake Mzazi ambaye alipendelea sanaΒ kumuita MlamiΒ
Mama yake ( Mlami ) aligundua haraka kuwa Noela hayupo sawaΒ kifikra, alimuuliza akiwa amejilaza sofaniΒ
“Kuna nini Noela huonekani kuwa sawa kabisa, unaonekana niΒ mwenye mawazo mengi kichwani mwako” Alihoji Mama yake NoelaΒ huku akimkata jicho la udadisi binti yake huyo wa pekeeΒ ambaye alikuwa akimpenda sana baada ya Baba yake kufariki.Β
“Ni Joshua Mama, tokea jana hapokei simu zangu. Sijui yukoΒ wapi” Alijibu Noela kama vile alikuwa amechokozwa na MamaΒ yake, alimpigia tena huyo JoshuaΒ
“Ulijaribu kwenda kwake?” Aliuliza Mama yake, NoelaΒ alimtazama Mama yake kwa jicho la kukata tamaa kishaΒ akatikisa kichwa ishara ya kuwa hakwenda nyumbani kwa JoshuaΒ kisha alimwambia Mama yakeΒ
“Msichana wake wa kazi anasema hakurudi tokea alipotoka janaΒ asubuhi” Alijibu NoelaΒ
“Sasa atakuwa wapi na kwanini hapokei simu zako jamani”Β Alisema Mama yake NoelaΒ
“Mama tokea jana nimechanganikiwa kabisa, ngoja tuΒ nikapumzike maana nimeshindwa hata kufanya kazi leo kwasababuΒ yake” Alisema NoelaΒ
“Haya sawa Mwanangu! Usijali sana huwenda yupo bize” AlisemaΒ Mama yake Noela kisha Noela alionesha tabasamu feki akaelekeaΒ chumbani kwake.Β
Ndani ya jumba la kifahari la Desmond, alikuwa ndiyo anaamkaΒ kutoka usingizini, alikuwa amelala palepale sebleni kutokanaΒ na pombe kumzidia. Aliamka akiwa mchovu sana lakini alipoamkaΒ tu alitaja jina la Mke wake Mandy kisha alitafuta simu yakeΒ ambayo ilikuwa kando yake kisha akapiga Hospitalini kwa NesiΒ LuciaΒ
“Vipi hali ya Mke wangu” Aliuliza Desmond huku akiwa na hofuΒ sana
“Mandy anaendelea na matibabu, bado hajapata ufahamu Desmond”Β ilisikika sauti kutoka upande wa pili, ilikuwa ni sauti yaΒ Nesi huyo iliyotoka kwa kubembeleza sanaΒ
“Asante! Kwa lolote unitaarifu mapema sana” Alisema DesmondΒ kisha alikata simu bila kusikiliza kingine kutoka kwa LuciaΒ
“Mandy kwanini hukufa? Kwanini upo hai? Kwa vyovyote vileΒ huwezi kutoboa siri nitakuuwa tu” Alisema Desmond kwa jazbaΒ kisha alikagua vizuri simu yake, alikutana na simu nyingiΒ ambazo hazikujibiwa, moja ilikuwa ya Noela, alikutana naΒ meseji nyingi kisha alitabasamu tu. Akaelekea kuoga kishaΒ alitoka kwenye jumba hilo ambalo alikuwa akiishi hapoΒ
Safari ya Desmond ilikuwa ni kuelekea nyumbani kwa Noela,Β kitendo cha Mama kusikia mlio wa gari kilimfanya achungulie,Β alipoliona gari la Desmond haraka alikimbilia chumbani kwaΒ Noela akamwambiaΒ
“Joshua amefika” Alisema Mama huyo, Noela hakuaminiΒ alichokisikia naye alikimbilia nje, alimuona Desmond ambayeΒ yeye alikuwa akimfahamu kwa jina la Joshua.Β
Alimkimbilia na kumkumbatia kwa furaha sana kisha choziΒ lilimbubujika, alionesha ni wazi kuwa alikuwa akimpenda sanaΒ Mwanaume huyo kisha alimuulizaΒ
“Joshua nimekutafuta sana ulikuwa wapi Mpenzi, nimeingiwa naΒ hofu mno” Desmond alicheka kidogoΒ
“Nimeamini kuwa unanipenda sana Noela, nilifanya kusudi iliΒ nipime upendo wako” Alisema Huyo aliyefahamika kwa jina laΒ Joshua lakini kule Hospitali alijulikana kama Desmond, hebuΒ tusonge na Uhondo wa Hadithi hii.Β
Mama yake Noela alisimama akiwaangalia wapendanao hao, kishaΒ moyo wake ulikubali kuwa walikuwa wakipendana sana,Β alitabasamu alafu akatangulia ndani huku Desmond ( Joshua )Β na Noela wakifuatia.Β
Walishinda hapo pamoja siku hiyo, walikula, walicheza pamojaΒ na kupeana mapenzi motomoto kisha baadaye waliondoka naΒ kuelekea kwenye nyumba ambayo Desmond alikuwa akiishi, hiiΒ ilikuwa ni nyumba tofauti na ile aliyokuwa akiishi na MkeΒ wake.Β
TURUDI MIAKA KADHAA ILIYOPITA
Ndani ya Kijiji kimoja, kulikuwa na familia moja iliyoishiΒ kwa shida sana. Familia hii ilikuwa ya Watu wawili tu, BabaΒ na Mwanaye. Walikuwa wameketi nje ya Banda lao, ukimyaΒ ulikuwa umetawala sana hapo, Mtoto huyo mwenye miaka 11Β alimuuliza Baba yake.Β
“Baba tutaenda wapi?” Aliuliza akiwa anamtazama Bba yakeΒ aliyekaa juu ya gogo la MtiΒ
“Unafikiria tutaenda wapi Desmond? Kifo cha Mama yakoΒ kimeleta mkosi sana kwetu kila kitu kimeharibika” AlisemaΒ Baba huyo, Mtoto huyo aliyeitwa Desmond ndiye huyu ambaye niΒ Mume wa Mandy aliyeko Hospitalini, kumbe jina lake halisi niΒ Desmond na siyo Joshua.Β
“Usiseme hivyo Baba! Huwenda Mungu alipanga iwe hivi” AlisemaΒ Mtoto DesmondΒ
“Alipanga tufukuzwe hapa Kijijini? Una mawazo ya kipumbavuΒ sana, huu ni mkosi aliouleta Mama yako!! Leo utakula HizoΒ kauli zako” Alisema Baba yake huyo kisha aliondoka zake naΒ kumuacha Desmond akizidi kutafakari. Maisha yao yalikuwa DuniΒ sana, Desmond alidondosha chozi kisha alikimbilia kwenyeΒ kaburi la Mama yake ambalo halikuwa mbali na banda lao,Β alipiga magoti kisha alisemaΒ
“Mama si hujakosea si ndiyo? Kwanini Baba anakuhukumuΒ hivi….Mama nauchukia umasikini, nakuahidi sitokufaΒ masikini” Alisema Desmond kisha aliondoka kaburini hapo.Β
TURUDI MAISHA YA SASAΒ
Hiyo ilikuwa ni kumbukumbu ambayo Desmond alikuwa akiikumbukaΒ alipokuwa akiitazama picha ya pamoja aliyopiga na Mama yake.Β Aliichukua picha hiyo iliyo ndani ya waleti yake kishaΒ alisemaΒ
“Mama natamani ungekuwepo uone Maisha ninayoishi, nimekuwaΒ tajiri nina kila kitu ila sina Baba wala Mama, Baba yanguΒ alikufa kwa pombe kali….” Alipokuwa akiyasema maneno hayaΒ Noela alikuwa akiingia chumbani, Desmond hakushtuka kamaΒ Noela alikuwa ameingia, Noela alimsikia Desmond akisemaΒ
“Kipo kirusi Mama, nahangaika kukiondoa ili niwe huru zaidi”Β Alisema Desmond lakini ghafla alihisi kuna Mtu anamsikiliza,Β ni kweli alipogeuka alimuona Noela akiwa anamtazama, DesmondΒ alionekana kuwa mwenye siri nzito sana ndani yake, siriΒ Β ambayo hakutaka Mtu yeyote aijuwe huku lengo lake kuu likiwaΒ ni kumuuwa Mke wake.
“Kirusi? Ukiondoe?” Aliuliza Noela, Desmond alimtazama NoelaΒ kwa Makini sana akagundua alikuwa hajaelewa lakini macho yaΒ Desmond yalikuwa yakivujisha chozi, Noela alimpatia kitambaaΒ Desmond ili afute chozi hilo, aliketi akamuuliza tenaΒ
“Kirusi gani untaka ukiondoe?” Aliuliza Noela, DesmondΒ alifuta chozi kisha alimwambia NoelaΒ
“Mimi na marehemu Mama yangu tulikuweka ahadi kuwa nitakuwaΒ na pesa nyingi sana na pia nitaowa, pesa ninazo lakiniΒ sijaowa, kwangu nachukulia kama kirusi kwenye ahadi yangu”Β Alisema Desmond, Basi Noela alitabasamu tuΒ
“Kubali nikuowe Noela ili uwe wangu peke yangu, jinsiΒ ninavyokupenda nahisi Dunia yote nimeiweka kiganjani pangu”Β Yalikuwa ni maneno matamu sana aliyoyatoa Desmond iliΒ kumfanya Noela asihisi chochote kile, kweli Noela alihamaΒ kihisia akasahau kila kituΒ
“Naanzaje kukataa Joshua? Nipo tayari uniowe hata kesho.Β Nikikumbuka jinsi tulivyokutana moyo wangu unajawa na furahaΒ na amani sana. Nakupenda pia Joshua” Alisema Noela kishaΒ alimkumbatia Desmond.Β
Sura ya Desmond ilibadili taswira kutoka kutabasamu hadi kuwaΒ mtu aliye siriazi na jambo lililo akilini mwake.Β
Majukumu ya kazi yaliendelea kwa pande zote yaani kwa DesmondΒ na kwa upande wa Noela, kumpata Desmond kulimpa furaha sanaΒ Noela akawa anachapa kazi zake.Β
Mchana wa siku hiyo, Desmond alienda Hospitalini kamaΒ kawaida, alipewa nafasi ya kumuona Mke wake Mandy. Alikuwa naΒ hasira na Mwanamke huyo. Mandy alikuwa amepoteza fahamu kwaΒ zaidi ya miezi mitano hivyo kwa kipindi chote alikuwaΒ Hospitalini tu, Desmond alisogea akaketi kwenye kiti kimojaΒ ambacho kilikuwa kando ya kitanda cha Mke wake, alikunja nneΒ kisha akamwambia MandyΒ
“Nina uhakika unanisikia Mandy! Katika vitu sitamani kuonaΒ katika Maisha yangu basi ni uhai wako, natamani uwe umekufaΒ na usiamke tena hapo Kitandani” Alisema Desmond akiwaΒ amevalia suti nyeusi zilizomkaa vizuri, alikuwa kijana mwenyeΒ muonekano mzuri sana. Desmond alisimama kisha alimsogeleaΒ Mandy
“Siri unayoijuwa kuhusu Mama yako ibaki kuwa siri yaΒ Ulimwengu mzima, sipo tayari kuyaharibu Maisha yanguΒ kwasababu yako. Asante kwa utajiri mkubwa ulioniachia Mandy,Β nasikitika sababu uliyemuamini siku zote hakuwa na mapenzi naΒ wewe, sikuwahi kukupenda Mandy….Nilizipenda pesa zako tu”Β Alisema Desmond kisha alivuta pumzi zake huku choziΒ likimlenga, licha ya uamuzi huo mgumu bado alionesha kuumiaΒ ndani ya Moyo wakeΒ
Ghafla aliona Mandy akitingisha kidole, hii ilimshtua sanaΒ Desmond, miezi yote Mandy hakuwahi kutingisha hata kope zaΒ macho yake, ilionesha wazi hata alichokizungumza DesmondΒ alikuwa akikisikia. Akiwa anaendelea kushangaa Desmond alionaΒ macho ya Mandy yakifunguka huku yakibubujikwa na mchozi,Β Mandy alikuwa ni Mwanamke mzuri mwenye weupe wa asili, choziΒ la Mandy lilionesha wazi kuwa lilibeba maumivu makali sanaΒ
“Mandy umeamka? Ina maana siri yangu utaisema!! HapanaΒ Unakufa” Alisema Desmond ndani ya moyo wake huku akiwaΒ amevurugwa sana, aliangalia huku na kule kisha alichukua mtoΒ na kumziba pumzi Mandy ili afe pale kitandani. MandyΒ alihangaika kwa nguvu chache aliyokuwa nayo lakini hakuwezaΒ kufanya lolote zaidi ya kuziona pumzi zake zikifika mwisho,Β Desmond alidhamiria kumuuwa Mandy mchana huo ili hiyo siriΒ yake isijulikane.Β
Mara Desmond alisikia chupa ikivunjika, alipogeuka alimuonaΒ nesi Lucia akiwa anaokota vipande vya vyupa pale mlangoni.Β Haraka aliacha jaribio la kutaka kumuuwa Mke wake Mandy.Β Aliuweka mto pembeni, alikuwa akitokwa na jasho jingi kishaΒ alimtazama Mandy alionekana kuzima, Desmond aligeuza machoΒ alimuona nesi Lucia akisogea hapoΒ
“ooh Desmond” Alisema Nesi Lucia huku akiwa anaweka vifaa juuΒ ya meza iliyo pembe ya ukuta, alipomtazama vizuri DesmondΒ alimuona akiwa anatokwa na jasho jingi sana, alishangaa kishaΒ alipeleka macho yake kwenye AC, kisha alirudisha kwa Desmond.Β Alionekana kushangaa jasho la Desmond lilitoka wapi ikiwaΒ chumba hicho kilikuwa hakina joto kabisaΒ
“Kulikoni Desmond mbona unavuja jasho hivyo” Aliuliza NesiΒ Lucia akiwa anamtazama kwa makini DesmondΒ
“Aaah- aaah…Jasho….unajuwa!! Lucia sijisikii vizuriΒ naomba nipumzike nje” Alisema Desmond kisha alitoka lakiniΒ Nesi Lucia aliendelea kujiuliza maswali yasiyo na majibu,Β mwisho alipuuzia jambo hilo.
Alienda kumtazama Mandy, alionekana kupowa huku mapigo yaΒ moyo yakienda sawa kwa maana Desmond hakufanikiwa jaribio laΒ kuondoa uhai wa Mandy, alibadilisha dripu na kufanya mamboΒ mengine kisha naye alitoka. Hali ya Mandy haikujulikana kwaΒ wakati huo kuwa ataamka lini wala saa ngapi laiti kamaΒ taarifa ya kuamka kwake ingewafikia madaktari basi tumainiΒ lingekuwa kubwa sana.Β
Akiwa nje ya wodi ile, Desmond aliendelea kutafakari kuhusuΒ usalama wa Mandy, alifikiria kama Mandy alikuwa amekufa auΒ alikuwa hajafa na kama hajafa basi siri yake iliyojifichaΒ kuhusu Mama yake Mandy ingefichuka, akiwa hapo alisikia sautiΒ ikimuitaΒ
“Mr Desmond” Alipogeuka alimuona Mtu mmoja akiwa amemsimamia,Β alishtuka sana sababu hakutarajia kumuona Mtu huyo kwa wakatiΒ huoΒ
“Mbona umeshtuka au hukutarajia kuniona?” Alihoji Mtu huyoΒ aliyekuwa Mwanaume mwenye sauti nzitoΒ
“Hapana ila nilikuwa mawazoni ndiyo maana nimeshtuka” AlisemaΒ Desmond kisha aliketi vizuri ili Mwanaume huyo naye aketiΒ
“Hali ya Mkeo vipi?” Aliuliza Mwanaume huyoΒ
“Mke wangu anaendelea…Hali yake bado ipo vile vile” AlijibuΒ DesmondΒ
“Mkeo ni shahidi namba moja wa kifo cha Mama yake, mara yaΒ mwisho alituma ujumbe kituo cha polisi kuwa anamjuwa MuuwajiΒ wa Mama yake, baada ya hapo ndiyo tukio la wewe kupigwaΒ risasi na Mke wako kupigizwa ukutani lilipotokea, Mkeo ni MtuΒ muhimu zaidi katika kesi ile” Alisema Mwanaume huyo ambayeΒ sasa alitambulika kuwa ni askariΒ
“Yaah! Ni kweli, ilikuwa ni siku ngumu sana katika MaishaΒ yangu ni kama nilimpoteza Mke wangu tokea siku ile hadi hiviΒ leo” Alijikakamua Desmond kisha alijibu, huyu DesmondΒ alionekana wazi kutambua juu ya kifo cha Mama yake MandyΒ lakini kwanini hakutaka ukweli uwekwe wazi? Au yeye ndiyeΒ aliyemuuwa Mama yake Mandy? Kwanini Amuuwe? TUSONGE MBELEΒ
“Kwa lolote usisite kutujulisha Mr. Desmond” Alisema AskariΒ huyo kisha aliondoka hapo. Kumbe nesi Lucia alikuwaΒ anamuangalia Desmond akizungumza na polisi kisha alipoondokaΒ yeye alimfuata Desmond alipokaa
“Desmond najuwa unavyojisikia, najuwa unaumia sana lakiniΒ Mkeo atakuwa sawa tu siku moja mtarudi kuwa kama zamani”Β Alisema Nesi Lucia, Desmond alimtazama Lucia kisha alijisemeaΒ moyoniΒ
“Ungejuwa ninavyotamani afe wala usingesema hayo maneno”Β Kabla hajamjibu chochote Lucia alipokea simu ya NoelaΒ
“Hello” Alisema Desmond baada ya kupokea simu hiyoΒ
“Desmond nakusubiria Mgahawani” Alisema Noela kisha DesmondΒ alijibuΒ
“Sawa nakuja”Β
“Unaenda wapi?” Alihoji LuciaΒ
“Mjini”Β
“Hata mimi ninaenda huko kwa ajili ya chakula, tafadhali nipeΒ lifti” Alisema LuciaΒ
“Haya sawa!” alisema Desmond kisha waliongozana hadi kwenyeΒ gari ya Desmond na safari ya Kuelekea Mjini ilianza.Β
Wakiwa barabarani Nesi Lucia macho yake yote yalikuwa kwaΒ Desmond, alimpenda sana Mwanaume huyo lakini alishindwaΒ kumwambia sababu alikuwa Mume wa Mtu istoshe alikuwaΒ akimuuguza Mke wake huyo.Β
Desmond aligundua hilo akamuuliza LuciaΒ
“Kwanini unaniangalia hivyo?”Β
“Desmond wewe ni Mzuri sana, Hakika Mke wako anajivunia kuwaΒ na Mwanaume kama Wewe” Alisema Lucia kisha DesmondΒ alitabasamu kidogo alafu hakusema chochote kile hadi anafikaΒ eneo ambalo Lucia alikuwa akienda. Ilikuwa ni kwenye mgahawaΒ huo huo ambao Desmond alienda kukutana na Mpenzi wake NoelaΒ
“Eeeh ajabu kumbe nawe ulikuwa unakuja hapa?” AliulizaΒ
“Yaah! Kuna Mtu naonana naye mara moja kisha niendelee naΒ majukumu mengine”Β
“Haya asante kwa Lifti” Alisema Lucia kisha alishuka akaingiaΒ kwenye mgahawa huo ambao ulikuwa wenye hadhi kubwa na piaΒ ulikuwa mkubwa mno, Desmond alienda mahali ambapo alipangaΒ kuonana na Noela.Β
Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA PILIΒ
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya kuendelea kutuma SIMULIZI Mpya Na Kuipost HAPA Kwa kumtumia Chochote kupitia
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMΒ Β
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xx Love&Pain xxΒ
11 Comments
Hakika hujawahi kutuangusha
Well done
Love and Pain
Inaonyesha ni Story nzito yenye burudani na Mafunzo ndani yake.
Asante sana Kaka Mkubwa
More Love from Kenya β₯οΈ
NAOMBA KWA SIKU ZIWE SEHEMU 2.
Kali sana
Dah..imeanz kwa kusisimua san
Nice
π
Mr KIJIWENI uyo ni
Diamondi na Nandy
ππ
Mbona story nzur sana iih
well done
π¨πππππ πππππ₯π₯π