Ukizungumzia ligi bora Afrika mashariki na kati huwezi kuacha kutaja Ligi Kuu Tanzania Bara inayofahamika kama NBC Premier League inayoleta msisimuo mkubwa zaidi miongoni mwa mashabiki wa soka Tanzania kwani ni moja kati ya jukwaa la kuvutia la mchezo wa soka na shauku kubwa kwa mashabiki wa mpira wa miguu nchini. Hata hivyo, kama ilivyo kwa ligi nyingine duniani, changamoto za uamuzi wa waamuzi na utumiaji wa sheria mara nyingine zinaweza kusababisha utata na malalamiko kati ya timu, wachezaji, na mashabiki.
Kurejea kwa ligi kuu ni wazi kuwa waamuzi waliingia na kujifunza zaidi kupitia michuano ya mataifa barani Afrika namna ambavyo kumekua hakuna malalamiko juu ya maamuzi ambayo yalikua na yanendelea kutolewa katika michuano hiyo mikubwa zaidi barani Afrika kwa ngazi ya timu za taifa.
Waamuzi wanacheza jukumu kubwa katika mafanikio na heshima ya Ligi Kuu kwani kupitia uamuzi wao wa matukio mbalimbali unaweza kuathiri matokeo ya mechi na kujenga au kuvunja imani ya wachezaji na mashabiki lakini Ili kuhakikisha uwazi na haki ni muhimu kufanya jitihada za kuwajengea uwezo waamuzi na kuhakikisha wanafanya maamuzi kwa usahihi.
Kuwekeza katika mafunzo ya mara kwa mara na maendeleo ya waamuzi ni muhimu sana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaweza kushirikiana na vyama vya waamuzi kutoa kozi zinazohusu mabadiliko katika sheria za mchezo, mbinu za uamuzi na jinsi ya kukabiliana na changamoto za kiuamuzi ili kuhakikisha tunaendelea kupata ligi bora isiyo kuwa na malalamiko mengi.
Kuimarisha maadili na uadilifu wa waamuzi ni muhimu na kwa hili bodi ya ligi pamoja na TFF inaweza kuweka mfumo wa kuwachukulia hatua waamuzi wanaokiuka maadili au kuhusika katika vitendo visivyofaa. Hii itawapa waamuzi motisha ya kufanya kazi kwa ufanisi na kuhakikisha heshima ya mchezo inadumishwa.
Kuna wakati tuliambiwa kuwa kutakua na matumizi ya teknolojia ya kisasa kama vile mfumo wa VAR (Video Assistant Referee) inaweza kusaidia kupunguza makosa ya uamuzi na kuleta uwazi zaidi katika mchezo. Hata hivyo, ni muhimu kuhakikisha kuwa teknolojia inatumika kwa ufanisi na inazingatia muktadha wa soka nchini Tanzania.
Wadau wote wa mchezo ikiwa ni pamoja na timu, wachezaji, na mashabiki wanapaswa kuelimishwa kuhusu sheria za mchezo na jinsi ya kuheshimu maamuzi ya waamuzi. Elimu hii itapunguza malalamiko yasiyo ya lazima na kujenga utamaduni wa kuheshimu maamuzi ya uwanjani labda tu pale endapo patatokea changamoto ya makosa ya kibinadamu.
Nadhani kwa kushirikiana na kufanya mabadiliko haya basi Ligi Kuu Tanzania Bara inaweza kuwa na waamuzi bora na mazingira yanayofaa kwa mchezo wa kuvutia na haki. Ni wajibu wa TFF na wadau wote kuhakikisha kuwa mchezo wa soka unakuwa na sifa nzuri na unaendelea kuwavutia mashabiki wengi zaidi. Hatimaye, kwa kufanya hivyo, tutaweza kufurahia Ligi Kuu yenye ushindani na haki, na kuacha nyuma manung’uniko yasiyo na msingi.
SOMA ZAIDI: Chama amedhihirisha kuwa viongozi wa simba ni wababaifu
4 Comments
Pingback: Yanga Waliuhitaji Zaidi Ushindi Kuliko Kitu Chochote - Kijiweni
Pingback: Simba Wasijiamini Kwa Ushindi Wa Tabora, Azam Ni Bora Sana - Kijiweni
Pingback: Geita Gold vs Simba Ni Mchezo Mwepesi Wenye Presha Kubwa - Kijiweni
Pingback: Mayele Ana Laana Ya Ligi Kuu? - Kijiweni