Maswali ni mengi kwanini inazunguzwa sana mechi ya Yanga SC dhidi ya Mamelodi Sundowns na siyo Simba SC na Al Ahly? Jibu lake ni jepesi sana, KIBIASHARA bidhaa ambayo inauzika sokoni kwa hivi Sasa ni Yanga SC.
KWANINI?
Yanga SC ndio timu ambayo imeutawala mpira wetu kwenye kila kona ndani ya msimu miwili. Yanga SC Bingwa NBC mara mbili mfululizo, inashikilia rekodi ya kucheza fainali kombe la Shirikisho Afrika mwaka jana, lakini pia imefanikiwa kupata matokeo ya ushindi mnono dhidi ya Mtani wake Simba SC.
Ukija kwa upande wa Simba SC, ni kama wameondoka kwenye ule ubora wao, hakuna cha kujivunia zaidi ya timu kucheza robo fainali kitu ambacho kwao siyo mafanikio kwani tayari walishafanya hivyo zaidi ya misimu mitatu hadi minne. Ukame wa kombe la Ligi Kuu nayo inaweza kuongeza unyonge kwa wanasimba na kuona kama bado ipo haja kusikilizia jambo jipya.
WASHINDANI
Ukiitazama vyema Mamelodi Sundowns ambayo itakuja kucheza na Yanga SC, yenyewe imeshiba kwenye rekodi zake. Ukienda kwao Afrika Kusini utaiona ikiongoza Ligi na alama zake 46 katika mechi 18, PSL 2023-2024 kwaiyo haina tofauti sana kama ilivyo Kwa Yanga SC ambayo nayo inaongoza Ligi ya NBC.
Ndio timu ambayo imethubutu kuifunga Al Ahly mabao 5-2 Machi 11, 2023 katika ubora wake. Ikaitandika tena Oktoba 29, 2023 bao 1-0 na kisha Novemba 1, 2023 wakatoka sare tasa ya 0-0.
Yanga SC na Mamelodi Sundowns ni mechi yenye mvuto mkubwa kwa kipindi kulingana na wote kuwa kwenye kiwango bora zaidi. Wachezaji wapande zote mbili wana sifa zinazofanana.
Ukija upande wa Simba SC mechi inafifia kwasababu wao Kwa wao kucheza mara Kwa mara yaani ile hamu ni kama imeondoka ingawa huwezi kuondoa ubora wa mechi yenyewe kulingana na ukubwa wa Al Ahly katika michuano hii mikubwa Afrika.
SOMA ZAIDI: Barua Kwa Waziri Ndumbaro Kuhusu Jezi Na Uzalendo
1 Comment
That is true