Ulikuwa Mchezo mzuri kutoka kwa pande zote mbili yaani Simba na Al Ahly ukianza kwa kasi sana huku timu zote zikifunguka kwa dakika 15 za mwanzo jambo ambalo liliacha nafasi Ya kutengeneza mianya ya njia ambazo zilitumika kutengeneza nafasi kadhaa za magoli na moja kutumika vizuri.
Simba SC wakianza na 4-2-3-1 kama kawaida yao huku wakiwa hawana mshambuliaji halisia kwenye eneo la mwisho. Walianzaje kiuchezaji? Silaha kubwa ilikuwa ni kukabia kwa juu zaidi na kuwapa presha wapinzani wakiwa na mpira yaani “Press” na iliwapa nafasi mzuri zaidi kutengeneza nafasi na kuwashamulia Al Ahly wakipitia zaidi pembeni Kibu Denis Prosper akiwa kushoto huku Clatous Chama akitokea kulia na Kanoute pamoja na Ntibazonkiza kuwa katikati kitu ambacho kilipekea Simba SC kuwa wengi kwenye eneo la Al Alhy hususa pale wakiwa na mpira.
Kipi walikosea na kupelekea kuruhusu goli? Baada ya kuwa juu wakitengeneza nafasi ya kushambulia na kupoteza mpira walishindwa kuwa na “Marking” nzuri, ukitazama mkimbio wa Mchezaji pekee aliyekuwa na mpira akipokea pasi akiwa kwenye nusu ya Simba SC, Babacar Sarr alikuwa akikabia zaidi macho na kushinda kukimbia kuharibu na hata Mchezaji aliyepewa pasi na kumtoka Mohamed Hussein alipewa mgongo na Clatous Chama jambo ambalo lilimfanya Tshabalalah Kukimbia zaidi kumfata hata hivyo Shomari Kapombe alishindwa kukaba mfungaji wa goli na kuamua kukaba nafasi zaidi kuliko mfungaji jambo ambalo lilipelekea kazi aliyofanya Ayoub kuokoa kutokamilika na kuruhusu goli.
Yapi mazuri Simba SC waliyafanya? Kubwa zaidi ni kujitoa kwa wachezaji wao kuanzia nyuma mpaka mbele jambo kubwa walilokuwa wakikosa ni kushindwa kutumia nafasi zao nyingi walizotengeneza, namna walivyokuwa wanatoka nyuma kushambulia walifanya kwa usahihi japo walikuwa wakiacha nafasi na mianya mingi ila haikuwa na madhara sana kwao kwa Al Ahly kuwa chini zaidi wakijilinda muda mwingi wa mchezo.
Ubora wa Al Ahly ulikuwa wapi ? Kuamua kukaa chini na kuwaachia Simba SC mpira zaidi wakiwa wanashambuliwa walikuwa wengi jambo ambalo wakishindwa kupiga pasi nyingi na walikosa watu eneo la Simba SC pale wakishambulia na wakishambuliwa walikuwa wakimuacha Antony Modeste pekee yake huku Percy Tau na El Shahat wakiwa chini na hata ikitokea wamepoteza mpira Mara nyingi Simba SC walikuwa wakiishinda na kurejesha umiliki kwao.
Kipindi cha pili kilikuwa chini zaidi na Al Alhy waliamua kabisa kubaki nyuma huku muda mwingi Simba SC wakishambulia ila walishindwa kuwa wafanisi eneo kubwa kuanzia upigaji pasi za mwisho kukimbia sahihi na umaliziaji ukiwa mbovu zaidi. Na ilo walifanikisha Al Ahly kwa kuwashinda Simba SC kwa kukaba (kuweka ulinzi) mzuri zaidi.
NB: Kibu Denis alikuwa na Siku bora sana Kazini kuanzia upokeaji mpira, mikimbio yake na hata kukaba kwake changamoto kubwa na eneo lake la mwisho la shambulizi amekuwa siyo bora.
Namna Kipa wa Al Ahly ameonyesha “performance” yake Leo ni kama mashabiki wa Al Ahly kuamini wako kwenye mikono sahihi licha ya El Shanawy kuwa majeruhi, ni sehemu ya mtu aliyekuwa na kiwango bora zaidi baada Ya Kibu Denis.
Fabrice Ngoma ni kama ni kawaida kwake sasa kilichokosekana ni plan B ya kuamua kutumia zaidi pembeni kushindwa kufanya kazi pasi zake ndefu zilifika ili timu ilikuwa chini kwa kipindi cha pili
Antony Modeste alikuwa chini sana wala hata akuwapa presha na upinzani mkubwa mabeki wa Simba SC walikuwa huru na rahisi sana kumzuia Mshambuliaji huyo. Sema Rad Slim muda mchache kiwanjani ila kazi yake imeonekana mikimbio mizuri mtulivu sana akiwa na mpira.
SOMA ZAIDI: Simba Wakifanya Hiki Wanamfunga Al Ahly Mapema Tu
1 Comment
Pingback: Yanga Dhidi Ya Mamelodi Uchambuzi Wa Mbinu Na Vikosi - Kijiweni