Leo ndio ile siku ambayo macho na masikio ya wapenda soka barani Afrika wanasubiria kwa hamu droo rasmi ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika la TotalEnergies (AFCON2025) nchini Morocco, Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) limetoa rasmi taratibu za droo za mashindano hayo makubwa barani Afrika.
Droo hii ambayo itafanyika Johannesburg siku ya Alhamisi tarehe 04 Julai ambapo jumla ya mataifa 48 ya Afrika yatashiriki ili kubaini ni nani atakayefuzu kwa toleo la 35 la tukio kubwa zaidi barani Afrika.
Timu zitakazoshiriki zitawekwa katika vikapu vinne vyenye timu 12 kila kimoja.
Nchi zilizoorodheshwa juu zaidi kulingana na Viwango vya FIFA vilivyotolewa tarehe 20 Juni 2024 zitachukua nafasi ya Kikapu 1, na utaratibu huo huo utafanywa kwa Vikapu vya 2, 3 na 4 ili kuunda mataifa 48.
Droo ya kufuzu itakamilika kwa kuunda makundi 12 ya timu 4 (Kundi A hadi L), ambapo timu ya kwanza na mshindi wa pili katika makundi kumi na moja (11) yasiyohusisha wenyeji wa mashindano Morocco, watapata tiketi ya kufuzu kwa mashindano hayo.
Kwa timu zitakazomaliza za kwanza na za pili katika kundi linalohusisha Morocco, ambao kwa kuwa wenyeji wa mashindano hupata tiketi moja kwa moja, hali zifuatazo zitatumika:
Ikiwa wenyeji wameorodheshwa wa kwanza, wenyeji watafuzu pamoja na mshindi wa pili wa kundi hilo.
Ikiwa wenyeji wameorodheshwa wa pili, wenyeji watafuzu pamoja na mshindi wa kwanza wa kundi hilo.
Ikiwa wenyeji wameorodheshwa wa tatu au wa nne, wenyeji watafuzu pamoja na mshindi wa kwanza wa kundi hilo.
Taratibu za Droo za Kombe la Mataifa ya Afrika la TotalEnergies CAF Morocco 2025:
Mpira wa kwanza utachukuliwa kutoka Kikapu 4 na utaenda kwenye nafasi A4.
Utaratibu huo utafanyika kwa timu zilizobaki za Kikapu 4 ambazo zitaenda kwenye nafasi B4, C4, D4, E4, F4, G4, H4, I4, J4, K4 & L4 kulingana na mpangilio wa droo.
Utaratibu huo huo kama ulivyoelezwa hapo juu utafanywa kwa Kikapu 3, Kikapu 2 na hatimaye Kikapu 1.
Mataifa 48 ya Afrika yatashiriki kulingana na Viwango vya FIFA vya hivi karibuni vilivyotolewa tarehe 20 Juni 2024.
48 African nations to be engaged as per latest FIFA Rankings issued 20 June 2024
POT 1 | POT 2 | POT 3 | POT 4 |
Morocco (Host) | Cape Verde | Kenya | Niger |
Senegal | Burkina Faso | Mauritania | Zimbabwe |
Egypt | Guinea | Congo | Rwanda |
Côte d’Ivoire | Gabon | Tanzania | The Gambia |
Nigeria | Equatorial Guinea | Guinea Bissau | Burundi |
Tunisia | Zambia | Libya | Liberia |
Algeria | Benin | Comoros | Ethiopia |
Cameroon | Angola | Togo | Botswana |
Mali | Uganda | Sudan | Lesotho |
South Africa | Namibia | Sierra Leone | Eswatini |
DR Congo | Mozambique | Malawi | South Sudan |
Ghana | Madagascar | Central Africa | Chad |
SOMA ZAIDI: Al Ahly Na Maajabu Ya Jezi Namba 72 Kabla Ya Mechi
1 Comment
Kila laheri taifa langu Tanzania