Ilipoishia “ “Geuka taratibu mikono ikiwa juu” akapaza sauti Marcus huku akiamini moja kwa moja kua huyo Mtu si Mzuri ndiyo maana alikua akipekua kwenye Majokofu hayo. Mtu huyo akageuka huku kichwa akiwa amekiinamishia chini, Marcus akamtaka ainue kichwa chake.

Taratibu akainua kichwa akiwa anatetemeka, Marcus hakuyaamini macho yake” 

Endelea Sasa

Sehemu Ya Kumi Na Moja

 

Mtu huyo alikua ni Sofia Mama yake Adela tena akiwa kwenye mavazi tata yaliyomshangaza Marcus, Sofia alikua ndani ya Koti kubwa Jeusi lililofika hadi chini, mkononi akiwa na kisu kikali kilichokua kinang’aa sana. 

“Sofia?” akauliza Marcus kwa Mshangao, mavazi pekee yalitosha kumwambia Marcus kuwa Sofia ndiye Muuwaji mwenye koti jeusi ambaye Binti yake Adela alikua akimtaja kwa kuficha mara zote huku akisema kuwa hakuiona sura ya Muuwaji, pale pale Marcus akaivuta simu yake na kumpigia Hamza kaka yake Sofia, kwa namna mambo yalivyokua yakienda isingelikua rahisi kwa Marcus kupata uhakika kuwa anayemwona ni Sofia.

Simu iliita kisha ikapokelewa na Hamza, Marcus akamuuliza Hamza Swali moja tu bila hata salam. 

“Sofia yupo hapo?” jibu alilolipata lilizidi kumfanya aukaze mkono wake wenye Bastola. 

“Weka kisu chini” alisema Marcus, Sofia akadondosha kisu. Marcus akapiga mahesabu makali, 

taratibu tena kwa tahadhali akamsogelea kisha akamwambia

“Ongozana na Mimi, ukifanya ujanja wowote Maisha yako yataishia hapo.” Alisema kibabe sana, 

Sofia akasogea mbele Marcus akimfuata kwa makini kwa nyuma. Muda wote Sofia alikua kimya 

baadaye walipofika kwenye korido akamuuliza Marcus

“Ni wewe uliyenipigia simu muda mchache uliopita?” 

“Nenda mbele sihitaji mzaha Sofia, nitakuuwa” 

Sofia akacheka na kumwambia Marcus

“Unafikiria naogopa kufa Marcus, hapana. Kama nimeweza kuisambaratisha familia yangu siogopi chochote na hata kukamatwa kwangu hakutakua na msaada wowote kwasababu Watu wataendelea kufa tu” 

“Unamaanisha nini?”

“Mimi si Muuwaji pekee, yupo Muuwaji anayesimama kama kivuli. Huyo ni hatari sana” alisema Sofia, kauli ya Sofia iliashiria wazi kua alikua akimfahamu huyo Muuwaji mwingine.


Nyumbani kwa Bilionea Yusuf

Saa 11:25 Jioni, vilio vikiwa vimetanda nyumbani kwa Bilionea Yusuf baada ya taarifa ya Kifo cha Mtoto Adela. Hamza alidondosha chozi akiwa ameketi kwenye kiti muda mfupi baada ya kutoka Hospitali ambako waliuacha Mwili wa Adela.

Sofia alijifungia chumbani kwake akiwa anahema huku akilia kwa maumivu makali sana, akakumbuka namna kifo cha Binti yake kilivyotokea.

xxx

Daktari aliyekua akimtibia Adela alitoka chumbani na kufika kwenye korido akiwa amemkodolea macho Sofia, muda huo Hamza alikua ametoka anazungumza na simu nje, jicho la Daktari lilimshtua sana Adela akafikiria huwenda Binti yake amefariki.

 Akamfuata Daktari huku akiwa na wasiwasi

“Dokta Binti yangu anaendeleaje?” aliuliza Adela akiwa amemshikilia bega Daktari, Daktari akamvuta Sofia kando.

“Ni kweli umemuuwa Baba yako?” alihoji Daktari, sura ya kulia iliondoka kwenye uso wa Sofia, 

akahamaki

“Unasema nini wewe?” aliuliza, Daktari akamvuta Sofia na kuelekea naye Wodini, alipofika tu alijua ni kwanini Daktari alihoji vile.

“Mama yangu amemuuwa Babu yangu, Mama yangu Muuaji, Mama yangu amemuuwa Babu 

yangu…” Adela alikua akiyarudia maneno hayo akiwa hajitambui, hili lilimwogopesha sana Sofia

“Nini hiki Dokta?” alihoji Adela akiwa amechanganikiwa. 

“kitaalam hiki anachokisema akiwa hajitambui ndiyo kumbukumbu pekee iliyo kichwani pake, mara nyingi huwa kweli” muda huo huo Sofia alimkwida Daktari na kumwambia

“Mnyamazishe, sitaki kusikia hivyo. Nimesema Mnyamazishe sitaki kusikia” alisema Sofia akionekana kua kwenye kuchanganikiwa huku akivuja chozi

“Namnyamazishaje Dada yangu, hata hivyo atayarudia tena maneno hayo” alizidi kusema Daktari, Mara mlango uligongwa.

“Muuwe” alisema Sofia kwa hasira huku jicho likiwa jekundu. 

“Nimesema Muuwe nitakupa chochote unachotaka” alisema 

“niachie hilo, rudi kule”. Sofia alifuta chozi akiwa na uhakika kua Adela atauawa, aliporudi alipokua amekaa akamwona Kaka yake akiwa anarudi, akajikausha. Muda huo huo ndiyo Daktari akafika na kutoa taarifa ya kifo cha Adela.

Akiwa kwenye kumbukumbu za kifo cha Binti yake, anashtushwa na Mlio wa simu, kutokana na hofu yake alijikuta akiidondosha simu hiyo, akainama kuiokota, alipoangalia ni Nani anapiga aliona ni Daktari aliyekua akimtibia Adela, aliipokea haraka

“Dokta” aliita Sofia kwa hofu na mashaka makubwa, aliona wazi Maisha yake yanaweza kuishia 

pabaya.

“Samahani sana Dada, sikuweza Kumwua Mtoto wako. Nilimchoma sindano ya Usingizi tu” ilisikika sauti kutoka upande wa pili, Sofia alizidi kuchanganikiwa, mafua yalimtoka yakifuatana na chozi lililokua likimbubujika.

“Unasemaje wewe, na pesa si nilikupa?”

“Moyo wangu umeingiwa na huruma sana, samahani. Kama unaweza kumuuwa basi nenda 

mochwari daraja la kwanza” alisema Daktari

“Wewe ni mpuuzi eeeh, umefanya nini….Hello,,Hello” aliita Adela akiwa amechanganikiwa jioni hiyo, 

Alipojaribu kumpigia yule Daktari simu ilikua imeshazimwa, akafungua kabati lake alilokua akilifunga kwa kutumia funguo muda wote. Akayatoa mavazi meusi, koti jeusi na Buti jeusi, akaondoka hapo kwa kunyata bila kushtukiwa na yeyote yule akiwa ameyatia mavazi hayo kwenye mfuko kisha akaingia kwenye gari, geti lilikua wazi hivyo wakati gari inatoka Kaka yake alijiuliza maswali mengi ni Nani alikua anatoka na gari. 

Hata hivyo hakutilia maanani sababu alihisi Mdogo wake alikua amemwagiza Mtu atoke na ndinga hiyo. Safari ya Sofia iliishia Hospitalini, akiwa ndani ya gari ndiyo akayavalia yale mavazi kisha akaingia Mochwari daraja la kwanza na kuanza kuusaka mwili wa Binti yake ili ammalize huko Mochwari, ndipo alipokutwa na Mpelelezi Marcus.

*****

Miaka kadhaa, Shambani Dodoma.

Bwana George alikua hodari wa kulitunza shamba hilo kiasi kwamba hata wafanyakazi wengine 

walimpenda sana, sifa hizo zilimfikia Bilionea Yusuf. Akampa nyongeza kubwa ya Mshahara mara nne zaidi ya aliokua anampa, hata Bwana George alishangaa namna Maisha yake yalivyobadilika.

Kutoka kuishi Maisha ya chini, alijengewa nyumba nzuri ya Kuishi, alinunuliwa gari ya kutembelea akiwa msimamizi wa Shamba. Hakumhitaji Mke wake ajumuike naye huko Shambani, akampa uhuru wa kuendelea kuishi Dar na Mtoto wao Martha. Wakati huo penzi lilikolea kati ya Bilionea Yusuf na Mke wa Bwana George, alipewa marupurupu ya fedha ili azidi kupumbazwa asikumbuke kurudi Dar.

Siku moja Bilionea Yusuf alimtuma dereva wake apeleke pesa Shambani kwa Bwana George, kama walivyo Binadamu wengine kutoweza kuhimili kukaa na jambo Moyoni ndivyo ilivyokua kwa dereva, baada ya kumkabidhi Bwana George kiasi kile cha pesa kwa ajili ya kulipa vibarua, alijishika kiuno akimtazama Bwana George akiwa anahesabu pesa.

Akamrudia pale chini ya Mti mkubwa, Bwana George aliponyanyua kichwa alimwona Dereva akiwa hajaondoka. Namna alivyosimama alionekana kutaka kusema jambo ambalo nafsi yake ilikua ikimkataza. 

“Eti kuna nini, mbona huondoki?” alihoji akiwa ameshikilia Maburungutu ya pesa

“Kuwa makini, usiwe bize sana na shamba la Watu ukashindwa kulinda mifugo yako. Itachukuliwa na jirani yako, jioni njema” alisema kisha alipanda gari na kuondoka, kauli hiyo ilimwacha Bwana George akitafakari.

Siku tatu zilipita, kauli ilijirudia sana akashindwa kulitunza jambo hilo, akamtafuta kibarua mmoja na kumwomba atafsiri kauli ya yule dereva, kirahisi sana yule Kibarua akamwuliza

“Mara yako ya Mwisho kuwa na Mkeo ni lini Bwana George?”

“Mwezi uliopita” 

“Ndiyo mfugo wako huo” akasema yule Kibarua.

Jioni akiwa ameketi kando ya myumba anayoishi huko Shambani alipata wazo la kwenda Dar mara moja bila Mzee Yusuf kujua maana alikua ni msimamizi mkuu hivyo akiondoka mambo yatasimama.

Mchana wa siku iliyofuata akaondoka na gari yake ndogo aliyonunuliwa akafanya safari ya kwenda Dar.Alipofika aliiyona gari ya kifahari ya Bilionea Yusuf, ilikua ndani ya nyumba hiyo kwenye fensi ambayo ilikua haijaisha vizuri.

Ulikua ni Usiku mwingi na isingelikua rahisi kuliona gari hapo, akapata wazo la kuzunguka hadi 

dirishani maana Milango ilikua imekwisha fungwa. Hakuna alichofanikiwa kuona wala kusikia, nafsi yake ikamtaka awe mtulivu, akarudi kwenye gari kisha akaondoka hapo na kwenda kuliegesha mita kadhaa kutoka nyumbani kwake kisha akajipumzisha humo akiisubiria Asubuhi ifike.

Alikaa macho hadi mapambazuko yalipoingia, bado ile gari ilikua nje ya nyumba yake, akaamua 

kuufuata moyo na hisia zake. Akafika na kuugonga Mlango, aligonga kwa sekunde kadhaa hadi 

aliposikia sauti ya Mke wake ikiuliza

“Nakuja jamani, Nani?” Bwana George alitulizana kimya hadi Mlango ulipofunguliwa, Mke wa Bwana George alipomwona Mume wake akataka kuufunga mlango lakini George akamwahi na kumzuia, kisha akamwuliza

“Unaficha Nini Mama Martha?” 

“Mmh mmmh hamna kitu nimeshtuka tu umekuja ghafla” alisema akionekana kujawa na hofu sana akiwa amevalia Khanga moja tu.

“Na ile gari imefuata nini hapa? Hebu nipishe” alisema na kumsukuma Mke wake kisha akaishka 

Kordo na kuelekea Chumbani, wakati huo Martha alikua amekaa kwenye korido akitazama 

Majibizano hayo akiwa amechuchumaa.

Ugomvi Mkubwa ukasikika ndani, Sauti ya Bilionea Yusuf ilisikika humo kisha sauti ya risasi ikasikika, Ukimya ukatawala. Mama yake Martha akiwa anahema alijivuta taratibu kuelekea chumbani, Martha akamfuata Mama yake huko chumbani, wote wakauwona Mwili wa Bwana George ukiwa juu ya kitanda damu nyingi ikiwa imemwagika Kitandani. 

“OOOOOHH!! Umeuwa?” alisema Mama Martha, akashtuka kumwona Martha akiitazama Maiti ya Baba yake, haraka akamvuta na kumzuia asione

“Ningefanya nini Mama Martha alitaka kuniuwa kwa kunichoma na kisu, nikajitetea” alisema 

Bilionea Yusuf akiwa anatetemeka.

“Sasa tutafanyaje sitaki kuishia Polisi Mimi” alisema Mama Martha.

“Tukautupe huu mwili na kusema alifariki kwa ajali ya gari” Wazo la kwenda kuutupa mwili wa 

Bwana George asubuhi hiyo waliliafiki wote, Martha akaishuhudia Maiti ya Baba yake aliyeuawa na Bilionea Yusuf. Maiti ikavutwa hadi kwenye gari ya Bwana George iliyokua imepaki kando ya gari ya Bilionea Yusuf.

“Usiogope Martha hakuna kibaya kilichomkuta Baba yako sawa?” alisema Bilionea Yusuf kisha 

akaingia kwenye hiyo gari na kwenda kuitosa kwenye korongo, kifo cha Bwana George kikaandkwa kua ni Ajali ya Gari, lakini siri ya kifo chake ilikua ni Mauwaji.

xxx

Jua kali likiwa linaichoma ardhi ya Jiji la Dar-es-salaam. Sofia mwenye pingu mikononi alikua 

akitembea kwenye korido, nyuma yake kukiwa na Mlinzi mwenye Bunduki mkononi, aliamrishwa kuingia chumba kimoja cha Mahojiano, ndani yake akamkuta Marcus akiwa ameketi, akaagiza Sofia afunguliwe Pingu. 

Miongoni mwa watu waliosimama nyuma ya kioo kikubwa wakitazama Mahojiano hayo alikua ni Kaka yake Sofia aitwaye Hamza, tena akiwa na sura ya huzuni sana akiamini Mdogo wake alikua akisingiziwa kufanya Mauwaji hayo ya kikatili tena kwa Baba yake Mzazi, akamweleza Afsa aliye kando yake

“Mnapoteza muda bure, Muuwaji ni yule aliyehukumiwa na Mahakama. Sofia hawezi kumwua Baba yake Mzazi, hamjui namna alivyokua akiaminika na Baba hadi kumpa sehemu kubwa ya Usimamizi wa kampuni” alisema akimsotea kidole yule Afsa ambaye alikaa kimya kisha akampa ishara kua Mahojiano yalikua yanaanza.

Masikio ya wengi yalitamani kusikia mkasa huo

“Sofia Yusuf, unafahamu nini kuhusu kifo cha Baba yako Mzazi?” aliulizwa, swali ambalo hakutaka kulijibu kwa haraka. Kisha naye akauliza

“Unataka kujua nini Mpelelezi?”

“Wewe ndiye Muuwaji mwenye koti jeusi uliyemuuwa Baba yako?” 

“Ndiyo” alijibu Sofia haraka, macho yalimtoka Hamza kusikia Mdogo wake amekubali kuhusika na kifo cha Baba yake

“Ilikuwaje ukamwua Baba yako Mzazi?”

“Kwasababu alinitenda Unyama ulioishi ndani yangu kwa muda mrefu” alisema Sofia, akathibitisha 

rasmi kua ni Muuwaji, kesi ilianza kusisimua. Angalau Mpelelezi Marcus alionesha tabasamu la 

Matumaini huku akijikuta zaidi kusikia kuhusu Mkasa huo wa kutisha.

“Unyama upi?” akauliza, shahuku ya kila mmoja ikawa ni kusikia zaidi, Sofia akasimama. Polisi 

akataka kumzuia lakini Marcus akampa ishara kua amwache kwanza, Sofia akaenda kusimama mbele ya Kioo akitazama kama vile alikua akiwaona Watu walio nyuma ya kioo wakisikiliza Mahojiano hayo.

“Najua kila Mtu atanipa jina analoona linanifaa lakini hakuna kati yenu ambaye angeliweza 

kustahimili nitakacho waeleza. Atakaye niita Muuwaji ni sawa kwasababu nastahili kuitwa hivyo” Sofia akaanza kumsimulia Mpelelezi Marcus namna alivyogeuka kua Muuwaji.

Kwanini Aliamua Kuwa Muuaji?  Usikose Sehemu Ya 12

 

Jiunge WhatsApp Channel Ya KIJIWENI Ili Kuwa Wa Kwanza Kupata Updates Za RIWAYA Hii Kwa Kubonyeza Hapa 

SOMA Uchambuzi Na Makala Mbalimbali Kwa Kubonyeza Hapa

 

 

27 Comments

  1. Yaan mpaka hiyo kesho ifike naona ni mbali balaa🥵

    Mwandishi tunaomba kesho uiachie mapema sana tafadhali 🙏🥺

  2. Upcoming Billionaire on

    Naona mambo yanazidi kupamba moto aiseee sio poa ok muuwaji wapili mimi namjua njooni na hela niwakamatie 🤣

  3. Bac bila shaka hata Martha nae atakua anahusika katika mauwaji maana kabla bilionea mzee yusuph hajachomwa kisu alishapewa sumu

  4. “Kwasababu alinitenda Unyama ulioishi ndani yangu kwa muda mrefu”.
    Mwandishi mbona kama smuelewi?

  5. Pingback: KOTI JEUSI (Sehemu Ya Kumi Na Tatu) KOTI JEUSI – 13 - Kijiweni

Leave A Reply


Exit mobile version